Mke ana mimba ya baba mkwe

Kiluuj

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
692
277
Mpo wakuu?

Ninaye rafiki yangu. Baada ya kuwa nje ya nchi kwa miaka miwili amerudi nyumbani na kukuta mkewe wa ndoa akiwa na mimba ya miezi nane.

Kumwuuliza mwenye mimba mkewe amemwambia kwamba mimba ni ya baba mkwe.

Amekuja kwangu kuniomba ushauri kwani anapaswa kurudi tena wiki ijayo.

Alikuwa anataka kuwaua wote wawili ila nikamwambia hilo sio suluhisho. Amesema atarudi kesho kupata ushauri zaidi.

Nipeni ushauri wa haraka.
 
Apige chini mke arudi Somalia, kuua sio suluhisho ni kuongeza matatizo tu.
 
Mwambie aache jeshi ajiunge na panya road au sungusungu ili apate muda wa kumlea mdogo wake ajaye.
 
mwambie akatafute binti mzuri wa kisomali apoze machungu.ila ukimuacha duuuh atajiua huyo kwa mawazo
 
pole yake! awaache tu asiue mbona wanawake wapo wengi wazuri? ataumia kwa sasa lakini ipo cku atasahau na kufurahia maisha amwachie Mungu amlipizie kisasi
 
Nikawaida sana hilo jambo kwa wtu wa kaskazini,asifanye kitu alee au amuache
 
Mpe pole sana,mwambie hakuna jipya chini ya jua ila linapokukuta ndio hua tatizo kubwa,simwambii kua ni rahisi kuhimili jambo hili lakini ajikaze kiume na aongee na mzee wake kujua kama nikweli sio kawaida kwa mzazi kumfanyia mwanawe hasa wakiume,wala haina haja yakuyafanya yakawa makubwa yule ni mzee wake vyovyote itakavyo kua,mke unaweza pata mwengine lakini mzazi awe mzuri ni huyo huyo awe mbaya ndio huyo huyo,amuombe sana mwenyezi mungu ampe nguvu
na moyo wa subra..
 
Huyo sio baba tena..Ni mme mwenza..Hapo apige chini wote tu
 
Achane kabisa na hiyo habari arudi zake nje akirejea tena atafute mke mwingine huyo amwachie baba yake.
 
Mpo wakuu?

Ninaye rafiki yangu. Baada ya kuwa nje ya nchi kwa miaka miwili amerudi nyumbani na kukuta mkewe wa ndoa akiwa na mimba ya miezi nane.

Kumwuuliza mwenye mimba mkewe amemwambia kwamba mimba ni ya baba mkwe.

Amekuja kwangu kuniomba ushauri kwani anapaswa kurudi tena wiki ijayo.

Alikuwa anataka kuwaua wote wawili ila nikamwambia hilo sio suluhisho. Amesema atarudi kesho kupata ushauri zaidi.

Nipeni ushauri wa haraka.
Hasara rohoo. . Aondokee amwachie baba na asirudi kamwee
 
Ana uhakika gani kama mkewe kamwambia ukweli mpaka akamuue baba yake mzazi?. Mwambie kuna wanawake million 20 Tanzania wazuri na warembo kuliko huyo 'mama mdogo'. Kama ana uhakika ni baba yake anahusika basi bora atafute sehemu nyingine awekeze kwa maisha yake, atakuja home kwenye msiba!
 
Back
Top Bottom