Mke aliniibia katoroka leo anaomba msamaha arudi

Mke aliniibia katoroka leo anaomba msamaha arudi

bussness

Member
Joined
Nov 29, 2014
Posts
46
Reaction score
20
niliishi na mwanamke tukapata mtoto mmoja ikatokea cku moja nipo kazini kasomba vitu vyote katoroka siku hizi anabembeleza eti nimsamehe shoga yake ndo alimwambia atoroke karudi na mwanangu kwangu nikimfukuza ataondoka na mtoto anadai sitakuja kumpata huyo mtoto tena .kwa upande wa sheria bado anaharali ya kubaki na mtoto yaani mtt yk chini ya miaka saba naombeni ushauri nimtimue mtoto atakuja baadaye kunitafuta au nimsikilizie wakati namlea mtoto wangu? ushauri tafadha
 
Toka ameondoka ni muda gani?

Amesema vitu alivyoiba vipo wapi?

Kwani bado unampenda kwa dhati?

Umejiridhisha kuwa amejirekebisha?
 
Msamehe tu mradi kajua kosa lake na kajutia,sababu usipomsamehe utakuwa unamtesa mototo ambaye ni innocent,na bado ni MDOGO anahitaji mapenzi ya baba na mama,na isitoshe mtoto ana thamani kuliko vitu vilivyoibiwa na huenda mpaka sasa kuna vitu vingine ulishanunua kufidia,hivyo msamehe kwa faida ya mwanao!!!
 
Kumbuka watu wanavumilia mengi kwenye ndoa kwa SBB ya watoto!!watu wanasalitiwa lkn wanasamehe kwa faida ya watoto!cha msingi kama aliondoka kitambo hakikisha mnapima VVU!
 
As long as hujamuoa bali umeamua tu kuishi naye then mkapa mtoto ... kuwa tayari kwa yote! Huo ndio ushauri wangu ...
 
Tuambie kabila lake kwanza... Maana angekua Mchagga lazima ungemtangaza
 
Wanawake walimu wao ni vipofu walikuwa bubu na kipofu wakielekezana lazima wataharibu tu

Msamehe tu mlee huyo mtoto
 
Mwizi habadiliki hata afungwe miaka mia akifanikiwa kurudi anaendelea na kazi kwa sababu tayari amelaaniwa na kutwishwa zigo la wizi. Amerudi kuchukua tena ulivyonunua. Umenishangaza eti anakutisha na mtoto....Mwache amtunze kama nguvu zipo na akishindwa amrudishe.
 
hiyo kawaida mbona, we kama unampenda kubali yote, m namjua dada mmoja alkua anakaa na mwanaume bila kuoana wakagombana akasomba kila kitu ndani, badae akarud na mume kamuoa, na hawana hata motto, sembuse wew ulyezaa nae, mapenzi upofu babu eeh ukisema uangalie makosa yake hamtofika...
 
Nina tatizo kama lako kaka, ni kweli huyo mwanamke hafai kabisa tena ila kwa faida ya mtoto wenu, hakikisha mnapima vvu kwanza kisha msamehe na mumlee mwanenu, mie mpaka leo hajarudi nami najikaza kiume huku natafuta tu rafiki wa kike maana jambo hilo linanishughulisha sana kichwani mwangu na anasema hawezi kuja mpaka nimfuate kwao, nami siwezi kwenda kwao kwa 7bu sikumfukuza, akipenda atakuja na asipopenda..basi
 
Pole sana ndugu. Alipoondoka na mali zako na mtoto alifikiri kuwa mtoto kazaaje? Huyo mtoto ni wako tu hata aende naye wapi. Ukimkaribisha ndani tena unajiletea majanga. Shauri yako
 
pole sana kwa hlo.we kabla hamjafanya makubaliano kuwa arud nymbn inabdi umshawish mkapme kwanza huwezjua alpoondoka alfanya mambo gan huko nyuma alafu ukijua nimzma msamehe ulee mtoto wako
 
chukua mwanao mlee au kama vip mpelekee mama yako amlee ila kumrudia huyo mwanamke sikushauri
 
huyo amekuja kumalizia alivyokuwa amebakiza...mkaribishe uone atakavyo inuka itakuwaje...itakuwa zaidi ya escrow
 
chukua mwanao mlee au kama vip mpelekee mama yako amlee ila kumrudia huyo mwanamke sikushauri

duuuhh! mama zetu kazi wanazo!!! watalea wangapi jamani!?? watulee sisi na mizigo yetu tuwape tena?? watapumzika lini sasa!!!
 
Safari hii shoga ake atamwambia akuwekee sumu ufe...manake anaonekana hana maamuzi binafsi...
 
Back
Top Bottom