figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la Norbert Gidion (30) mkaazi wa Masanga katika Manispaa ya Kigoma Ujiji amekutwa amefariki dunia akiwa amejinyonga kwenye mti wa mwembe kwa kile kinachosadikika kuwa ni wivu wa mapenzi
Kamanda wa polisi mkoani kigoma Afande Ferdinand Mtui, amethibitisha tukio hilo na kusemw kwamba upelelezi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha kifo cha Marehemu Norbert Gidion ni kutokuwepo na maelewano dhidi ya marehemu na mke wake, Bi.Happyfania Caristus. "Natoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kuwa mazingira kama hayo husababisha kutokea vifo visivyotarajiwa kwa jamii:, alisema Kamanda Mtui.
Wakielezea tukio hilo wapangaji wenzie marehemu wamesema kuwa kwa kipindi kirefu marehemu alikuwa safari hadi umauti unamkuta na kwamba hata alivyorudi safari alikuwa halali nyumbani kwa mke wake. Mzazi wa marehemu Bw. Gidioni Hungu amesema kuwa mazingira ya kifo hicho imekuwa sintofahamu kwani alikuwa hana maelewano mazuri na mkewe.