Mkate wa kiwavi wenye kuku

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,377
2,000
dc8f847158c670ad8d499e820bb0350637919592.jpeg


Mahitaji
Kuandaa mkate huu tutakuwa na mahitaji ya aina mbili tofauti.

Mahitaji kwa Unga wa mkate
 • Unga wa ngano, kilo 1
 • Maziwa ya unga vijiko 2 vikubwa
 • Hamira kijiko 1 cha chai
 • Mayai 2 (Moja la kuchanganya kwenye mkate, lingine utapaka mwisho)
 • Vijiko 4 vikubwa vya mafuta ya kula
 • Sukari laini (Au unaweza kuisaga)
 • Chumvi kijiko 1 cha chai
 • Ladha ya Vanilla (Vanilla flavour)
 • Ufuta (kidogo tu wa kunyunyizia kwenye mkate)
 • Maji ya moto ¼ lita (kwa kukandia)
Mahitaji kwa kutengeneza sauce ya kuku
 • Minofu ya kuku ¼ kilo
 • Kitunguu 1 kilichokatwa vipande vidogo
 • Majani ya Korianda
 • Kijiko 1 cha chai
 • Pilipili ndogo za kijani, zikate vipande vidogo
 • Masala Kijiko 1 cha chai
 • Pilipili manga
 • Unga vijiko 2 vikubwa
 • Kikombe 1 cha maziwa

Katika kuandaa mkate wetu, tutaandaa katika hatua kuu 2.

1. Kuandaa nyama ya kujazia kwenye mkate

Unaweza kutumia kitu chochote kujazia ndani ya mkate. Mfano : sausage, mboga za majani, viazi nk.. Cha muhimu kabla hujaanza kuandaa, hakikisha kuku amechemshwa vizuri na amepondwa vizuri. Kwa ufupi, haya hapa maelezo yake.
 • Bandika kikaango, weka mafuta. Acha yapate moto.
 • Weka kitunguu. Koroga hadi kigeuke rangi na kiwe laini.
 • Weka unga, chumvi, pilipili manga, na masala. Koroga pamoja kama dakika 2 hadi 3.
 • Weka maziwa, koroga vizuri. Acha iive kiasi hadi iwe uji mzito.
 • Weka pilipili za kijani, ongeza majani ya korianda. Koroga vizuri.
 • Weka kuku. Koroga vizuri.
 • Bandua toka jikoni. Hifadhi pembeni acha ipoe.
2. Kuandaa mikate
 • Kabla ya kuendelea, hakikisha umeshakanda unga na kuuacha uumuke kwa muda.
 • Washa oven, weka nyuzijoto 180°C.
 • Tandaza unga mkavu kiasi kwenye meza au ubao unaotumia kukandia.
 • Weka unga uliokandwa kwenye meza ya kukandia, kisha kanda tena ngano yako kidogo. Hii inasaidia kuondoa hewa iliyobaki ndani ya unga.
20150118_162000.jpg


 • Gawa ngano kwenye mabonge machache kulingana na idadi ya mikate unayotaka.
 • Anza kutengeneza shepu unazotaka za mkate. Tafadhali angalia picha hapo chini.
 • Changanya nyama ya kuku uliyoandaa. Weka kwenye mkate kisha funga vizuri.
 • Ukimaliza kufunga, pasua yai, koroga na changanya maji kidogo. Paka mchanganyiko wa yai juu ya mkate kisha mwagia ufuta.
 • Panga mikate kwenye chombo cha kuokea
 • Weka mikate kwenye oven. Acha iive kwa muda wa dakika 30 hadi 40.
 • Angalia mikate kama imeiva.
catepillar2.jpg


Maelezo ya picha

1. Baada ya kukanda, tenga mabonge ya mkate kutokana na idadi ya mikate unayotaka kuandaa

2. Tandaza vizuri kwenye sehemu ya kukandia. Weka nyama ya kujazia, juu ya unga wako ulioutandaza vizuri.

3. Kata ngano yako kwa kisu vizuri mistari karibu karibu ili kuweza kutengeneza umbo unalotaka

4. Anza kukunja ngano yako. Kunja kuanzia kwenye nyama na kuizungusha hadi kufikia mwisho kule ulipochana

5. Ukishamaliza, paka majarini (siagi) na mwagia mchanganyiko wa yai na maji (egg wash) ili kuongeza ladha kwenye mkate wako. Hii ndio inanogesha zaidi. Kisha weka kwenye oven kwa muda wa dakika 30 hadi 40.

6. Mkate wako tayari kuliwa, jirambe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom