Mkataba wa shirika la reli RVR kufutwa?

Mkataba wa shirika la reli RVR kufutwa?

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,144
Reaction score
166,082
Mkataba wa shirika la reli RVR kufutwa?

Wajumbe wa serikali za Uganda na Kenya wanatarajiwa kukutana leo nchini Uganda ili kujadili hatma ya kampuni ya Reli ya Rift Valley Railways.
Nchi hizi mbili zilikabidhi usimamizi wa reli kwa kampuni ya Afrika kusini ya RVR Novemba 2006 chini ya makubaliano ya kuikuza kwa kipindi cha miaka 25.
Lakini miaka takriban mitano hakuna maendeleo yoyote na ndio nchi hizi zinataka kufuta mkataba huo na kuupa kampuni yenye uwezo.
Shirika hili limeshutumiwa kwa kushindwa kuboresha usafiri wa reli. Pia kwamba kabla ya Rift valley kukabidhiwa kandarasi hiyo reli hiyo lilikuwa ikibeba asili mia 25 ya mizigo yote kupitia bandari ya Mombasa, kiwango ambacho sasa kimeshuka hadi asili mia tano.
Serikali hizi mbili sasa zinakusudia kuhamisha hisa zake kwa kampuni mpya inayojulikana kama Kenya Uganda Railways (KURH) Ltd ambapo pande zote husika zitakuwa na hisa sawa.
Lakini hilo halijakubaliwa na wenye hisa.
 
Back
Top Bottom