MKATABA WA MAFUTA ZANZIBAR Shivji amvaa Dk. Shein

MKATABA WA MAFUTA ZANZIBAR Shivji amvaa Dk. Shein

Kashishi

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2010
Posts
1,147
Reaction score
641
MKATABA WA MAFUTA ZANZIBAR

Shivji amvaa Dk. Shein

Mwandishi Wetu Toleo la 319 9 Oct 2013

319_shivji.jpg


MAKUBALIANO ya mkataba wa awali (MoU), uliosainiwa hivi karibuni baina ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk Ali Mohamed Shein, na kampuni ya kimataifa ya mafuta ya Shell unaohusu utafutaji na hatimaye uchimbaji wa mafuta, umeelezwa kuwa ni mkataba ‘feki’ na usiokuwa na uhalali wowote kisheria.

Magwiji wa sheria na mikataba nchini, Profesa Issa Shivji na Dk Rugemeleza Nshala, kwa nyakati tofauti, wameliambia gazeti hili kuwa hicho kinachodaiwa kusainiwa na Dk Shein na kampuni hiyo ya Shell, hakipo kisheria kwa maelezo kwamba mafuta na gesi asilia ni mambo yaliyo chini ya Muungano, na kwa hiyo mwenye mamlaka ya kusaini mkataba wa aina hiyo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, ni waziri mwenye dhamana kuhusu masuala ya nishati.

Katika toleo la wiki iliyopita, gazeti hili lilibeba habari kuu iliyokuwa ikielezea namna Dk Shein alivyoingia makubaliano ya awali (MoU) na kampuni kubwa ya kimataifa inayojishughulisha na biashara ya nishati ya mafuta na gesi asilia, Shell, wakati akiwa katika ziara yake ya kiserikali nchini Uholanzi, Agosti mwaka huu.

Katika mkataba huo wa makubaliano ya awali, SMZ imeipatia kampuni hiyo ya Shell idhini ya kutafiti na hatimaye kuchimba mafuta katika vitalu vinne, vilivyopo Zanzibar, vilivyopewa majina ya Block 9,10,11 na 12.

Akizungumzia hatua hiyo wiki iliyopita akiwa mjini Kilwa Masoko kwa ajili ya kutoa mafunzo yanayohusiana na masuala ya mafuta na gesi kwa wanahabari nchini, yaliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), Profesa Shivji, alisema Dk Shein hana mamlaka yoyote hadi sasa ya kisheria kusaini mkataba wowote unaohusiana na masuala ya mafuta na gesi ndani ya eneo la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Alisema mafuta na gesi ni mambo ya Muungano, na kwa hiyo mamlaka pekee yenye uhalali wa kisheria kusaini mkataba wowote unaohusiana na jambo hilo, ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Aidha, Profesa Shivji aliwataka Watanzania kuwapuuza wote wanaodai kwamba masuala ya mafuta na gesi asilia viliingizwa kinyemela katika mambo yote ya Muungano, akisisitiza kwamba maliasili hiyo iliongezwa kwenye mambo ya Muungano mwaka 1968 wakati wa utawala wa Mzee Abeid Amani Karume.

“Masuala ya mafuta na gesi yaliongezwa kwenye mambo ya Muungano na Mzee Karume mwenyewe mwaka 1968. Zitafuteni Hansard (taarifa mazungumzo yaliyofanyika ndani ya Bunge), zipo. Hao wanaopiga propaganda kwamba mambo hayo yaliingizwa kinyemela kwenye mambo ya Muungano ni watu wa kupuuzwa,” alisema Profesa Shivji.
319_nshala.jpg
Kwa upande wake, Dk Nshala alisema kwa kusaini makubaliano hayo, si tu kwamba Dk Shein amevunja Katiba, bali hata kampuni yenyewe ya Shell iliyosaini mkataba huo, imesaini mkataba kanyaboya (feki) kutokana na kile alichosema kampuni hiyo imeingia makubaliano na mtu asiyehusika kwa mujibu wa sheria ya sasa ya madini, mafuta na gesi.

“Mwenye mamlaka ya kisheria kusaini mkataba wowote unaohusu nishati na madini, kwa mujibu wa Katiba yetu, kwa niaba ya Serikali yetu, ni Waziri wa Nishati na Madini. Suala la mafuta na gesi asilia viko chini ya Muungano, Dk Shein hana uhalali wowote wa kusaini mkataba wa mafuta, gesi wala madini…unajua kuna watu wanataka kutumia kipindi hiki ambacho tuko kwenye mchakato wa kuandika Katiba Mpya kuvuruga Muungano,” anasema Dk Nshala ambaye amebobea katika masuala ya mikataba ya madini, mafuta na gesi.

Raia Mwema linafahamu kwamba ingawa MoU inaonyesha kwamba walioingia makubaliano ni Shein na Mtendaji Mkuu wa Shell, Peter Voser, aliyesaini mkataba huo kwa niaba ya Shein ni Waziri wa Nishati wa SMZ, Ramadhan Abdallah Shaaban.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Katiba na maelezo ya Prof. Shivji na Dk. Nshalla, aliyepaswa kusaini makubaliano kama hayo kwa sasa ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.

- See more at: Raia Mwema - Shivji amvaa Dk. Shein

Chanzo: Gazeti la RaiaMwema.
 
Naomba kufahamishwa: kilichosainiwa ni MKATABA au MoU? Mimi sio mwanasheria lakini kadiri nijuavyo hivyo ni vitu viwili tofauti. Ni kama zile MoU kati ya Kanisa na Serikali ambazo hata waislamu waliambiwa nao wapeleke zao badala ya kulalamika kitu ambacho kimewashinda kutekeleza hadi leo hii?
 
mou inaelekea kua mkataba mbeleni kwa iyo si kitu cha kupuuzwa? nadhan wenzetu zanzibar washafanya vitu vingi kinyume na muungano kama wanavyosajili meli walipoanzisha zanzibar maritime institute hadi wakaanza kusajili meli za iran nchi iliyowekewa vikwazo vya kimataifa na baadae ile meli iliyoshikwa na bangi kule italy!!
 
Profesa Shivji hivi umeliona la mafuta tu, mbona mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ya 2010 yaliyovunja katiba ya muungano na kuuvunja muungano kisheria huyatolei mayowe ya kuwa si ya halali? Na tuanze kwanza katika lililo kubwa zaidi ya MOU hii katiba ilioifanya Tanzania kuwa ni muungano wa Zanzibar na Tanganyika kwa sasa ina uhalali gani? La maendeleo ya wananchi analiona na kulipigia kelele, la msingi linalobeba uzito wa kuwepo kwa huo muungano kwa woga wao wamekaa kimnya, kwanza na tulianze la katiba ya sasa baada ya marekebisho ya katiba ya Zanzibar ya 2010 jee wasomi wa sharia muungano kisheria haukuvunjwa?
 
mou inaelekea kua mkataba mbeleni kwa iyo si kitu cha kupuuzwa? nadhan wenzetu zanzibar washafanya vitu vingi kinyume na muungano kama wanavyosajili meli walipoanzisha zanzibar maritime institute hadi wakaanza kusajili meli za iran nchi iliyowekewa vikwazo vya kimataifa na baadae ile meli iliyoshikwa na bangi kule italy!!

kumbe zile meli za majanga zimesajiliwa Zenji? aaaah! sasa mbona zinatutia doa Tz nzima? kweli ukimkabidhi mtoto uongozi haya ndo matokeo yake.
 
Hatuna tatizo na hilo kwani hata mikataba ya gesi Mtwara hatujui inasemaje, hata wabunge wetu hawajui. Yote sawa tu. Ngoja Shein naye aingie mkataba ili kama kuna 10% naye apate!
 
wewe kwa mapungufu yako ya akili unadhani Waislamu wameshindwa kuandika hiyo MoU? tuna wasomi wengi tu wa kuandika mengi zaidi ya hiyo,dini yetu inatukataza unafiki,serikali imetuundia chombo sisi Waislamu ambacho hatukitaki,tukishapata chombo chetu huru,ndio tutaamua nini cha kufanya na tegemea zaidi ya hiyo MoU
Naomba kufahamishwa:
kilichosainiwa ni MKATABA au MoU? Mimi sio mwanasheria lakini kadiri
nijuavyo hivyo ni vitu viwili tofauti. Ni kama zile MoU kati ya Kanisa
na Serikali ambazo hata waislamu waliambiwa nao wapeleke zao badala ya
kulalamika kitu ambacho kimewashinda kutekeleza hadi leo hii?
 
Tunaomba Shivji akite kisomi kwenye uhalali wa mkataba wa muungano pia. Huu nao ukibainaka feki basi mikataba yote ya serikali ya muungano Tanzania batili.
 
Shivji uzee unamsumbua.

shivji anatafsiri tu vifungu vya katiba ya jamhuri..,sasa wewe unajiita kijana ata sheria za nchi huzijui!ni mara mia kuwa na mzee km huyu kuliko vjana mia km wenye fikra km zako
 
Dr. Shivji yeye ni mkongwe wa sheria nashangaa mpk leo hajajua tu kuwa muungano haupo tena, au anataka aone watu wanagombana ndo ajue, sasa mm ninamwambia muungano haupo tokea 2010
 
Shivji uzee unamsumbua.


Yaani Shivji pamoja na hishma kwenye mambo mengi...lakini ingelazim siku moja apewe deportation order ya kwenda kwao India akanyie kwenye sinia na Makumbaro wenzie...nafikiri ndo atatia akili uzuri! Kwi! Kwi! Kwi!

Niwie radhi Bobwe;lakini hyu Mzee wakti mwingine hunitibua mno! Yaani yeye katika uonevu,dhulma ,rushwa na mengineyo yoote hayaoni...kilichomkera ni hayo mafuta ya Zanzibar tu!?

Alikua wapi huyo Shivji wakti ule yule Nyerere wake...communist mwenzie,akinyanyasa Wazanzibar na kumfanyia madhila Alhaj Jumbe na wenzie!?

Kuna mangi yakunena,na huyo Mzee Shivji namjua uzuri mno na kumkumbuka vyema pale Mlimani!...one of those sell outs!

Ahsanta.
 
MAGAMBA WASHAMTEKA ALIKUWA ANASEREREKA VEMA TU SIKU ZA NYUMA :tape:
 
MKATABA WA MAFUTA ZANZIBAR

Shivji amvaa Dk. Shein

Mwandishi Wetu Toleo la 319 9 Oct 2013

319_shivji.jpg


MAKUBALIANO ya mkataba wa awali (MoU), uliosainiwa hivi karibuni baina ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk Ali Mohamed Shein, na kampuni ya kimataifa ya mafuta ya Shell unaohusu utafutaji na hatimaye uchimbaji wa mafuta, umeelezwa kuwa ni mkataba ‘feki’ na usiokuwa na uhalali wowote kisheria.



- See more at: Raia Mwema - Shivji amvaa Dk. Shein

Chanzo: Gazeti la RaiaMwema.

Shivji alikuwa arejea mpango huu unaotaka kupitishwa haraka haraka nini.

Je huo mkataba mpaka leo umefikia wapi?
Nini madhara yake pale Sheria hii itakapo pitishwa na wazee wa ndiyooooooooooooo
Na spika kumalizia na ndhani waliosema ndiyooooo wameshinda.

 
Back
Top Bottom