Mkataba wa "Lights" lazima uvunjwe-Trwawu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkataba wa "Lights" lazima uvunjwe-Trwawu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, Jan 30, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Saturday, 29 January 2011 09:35 0diggsdigg

  Lilian Lucas,Morogoro
  KAMATI Kuu ya Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (Trawu), imeiomba serikali kutekeleza ahadi yake kuhusu kuvunja mkataba wa Kampuni ya Lights.

  Wakizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa Trawu,Sylivester Rwegasira, alisema serikali kupitia kikao cha Bunge la mwisho, ilitangaza azma ya kuvunja mkataba wa Kampuni ya Lights, lakini hadi sasa haijatekeleza ahadi hiyo.

  Alisema Trawu imesikitishwa mno na itendo hicho ambacho alikiita kuwa ni cha kuwadanganya Watanzania na wafanyakazi wa Shirika la Reli.

  Rwegasira alisema ahadi hiyo ya serikali haikuwa ya kweli hasa ikizingatiwa kuwa menejimenti ya Lights, bado inaendelea kufanya kazi ikiwa ni pamopja na kukusanya mapato ya Kampuni ya TRL.

  Alielezea kushangazwa kwake juu ya serikali kutochukua hatua dhidi ya kampuni hiyo, ambayo imekuwa ikiitia hasara Tanzania.

  Hata hivyo kamati kuu hiyo imetoa muda wa wiki moja kwa serikali kuhakikisha kuwa menejimenti ya Kampuni ya Lights, inaondolewa katika kusimamia shughuli za uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania na kutoa nafasi kwa kamati ya wazawa kusimamia shughuli hizo katika kipindi cha mpito.


  Katibu huyo alisema kama serikali haitafanya hivyo, suala hilo litafikishwa katika ngazi ya wanachama ili ikibidi wagome kufanyakazi.

  "Tunadhamiria kuchukua sheria kama serikali haitasikiliza madai yetu," alisema Rwegasira
  Source:Mkataba wa Lights lazima uvunjwe-Trwawu

  Kulikoni gazeti la Mwananchi? Hivi RITES imebadilishwa jina na kuwa Lights?
   
Loading...