Mkataba wa EPA umeasisiwa na nani?

Kiasi fulani muono wako juu ya mpangilio uko vizuri, lakini unadhani pia kwamba, serikali hii hii inayoshughulika na mikopo hewa, huku kukiwa na cv fake, wafanyakazi hewa huku kukiwa na kukosekana kwa ajira, ukosefu wa dawa, huku kukiwa na ongezeko kubwa la watu, nk. inaweza kujiongezea jukumu lingine kubwa la ki sera kama hilo?
Hii nchi kuna kila kitu kilichokosekana ni utayari na utashi tu! Wala leo hii hatuhitaji kuwa na sera mpya ya kilimo ili tuweze kufanya kilimo bora bali kutengeneza mazingira mazuri kwa watu ambao tayari wapo in business! Sio kwamba una-encourage watu waingie kwenye kilimo na kwamba watapata mikopo kwani ukifanya hivyo utapata makumi kwa makumi ya watu wasio na passion ya kilimo bali wataingia kwa sababu tu wamesikia kuna mikopo na matokeo yake, wakipata mikopo watai-divert kwenye shughuli zingine. Unaandaa mazingira na hata ikibidi kuwawezesha wale ambao tayari wapo kwenye biashara ya kilimo na wana rekodi mzuri ya uzalishaji kulingana na level yao! By kuwawezesha wala haimaanishi kuwapa pesa bali wawe na easy access na mahitaji yatayoendeleza shughuli zao na bila shaka, moja ya hayo mambo ni mikopo... wawe na easy access to loans. Unajua moja ya changamoto kubwa kabisa ya kilimo na ugumu wa kuhifadhi mazao ya kilimo hususani mazao ya bustani. Lakini hizi storage facilities zipo lakini watu wanashindwa kwavile hawana uwezo wa kuzinunua na matokeo yake; mtu hawezi kulima nyanya kwa lengo la kuuza Ulaya kwavile anajua zitaozea airport hata kabla hazijapanda ndege!! By the way, si tumeanzisha Benki ya Kilimo? Ingekuwa kweli basi ni benki ya kilimo na kuwe na easy access to mikopo ya kuendeleza (sio kuanzisha) investments za kilimo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom