darcity
JF-Expert Member
- Jul 20, 2009
- 9,208
- 18,226
Tanesco imeingia maktaba wa dola milioni 309.26(zaidi ya tsh bilioni 673 na milioni mia sita ishirini) kujenga line ya USAFIRISHAJI ya kilometa 414 toka Isinya nchini Kenya.
Dondoo muhimu*
1.Kilometa 318 kujengwa TZ zitagharimu US dollar mil.258.82
2.kilometa 96 kujengwa kenya zitagharimu us dollar mil. 50.45
3.Kampuni zitakazojenga ni Kalpatan Power Transmission Limited ya India, Ms Bouygues Energy and Services ya Ufaransa na Energoinvest and EMS ya Yugoslavia
4.Wafadhili (wakopeshaji) Serikali ya TZ, African Development Bank (AfDB)(mkopo utakaorudishwa na riba) na Japan International Cooperation Agency (JICA)(mkopo pia kwa jina la mfadhili)
5.Muda wa mradi ni miezi 24
6.Ni mradi wa pamoja kati ya TANESCO na Kenya Transmission Company (Ketraco)
7.Unalenga kuunganisha mtandao wa umeme wa Kusini mwa Afrika (Southern African Power Pool -SAPP) na ule wa mashariki ya Afrika East African Power Pool (EAPP) kupitia njia ya kaskazini ya Zambia
Dodoso*
1.Je wakati tunahangaika na miradi ya usafirishaji umeme inayohusisha mataifa mengine uzalishaji wetu unatosheleza?
2.Nani atakayefaidika na uuzaji umeme kwani hatuna kiwango cha kutosha cha kuuza umeme kwenda nchi za nje? Kenya, Zambia au CONGO?
3.Tumetumia zaidi ya bilioni 673 kwa ajili ya kusafirsha umeme, je fedha hizo zingetumika kuzalisha umeme sisi wenyewe badala ya kununua toka Kenya tungezalisha megawati ngapi?
4.Kilometa 96 zinazojengwa Kenya nani analipia? na kama mkataba wa mauziano ya umeme yakiisha zitabaki chini ya umiliki wa nani?
5.Ina maana uongozi wa Tanesco hauna alternatives nyingine ya kuzalisha umeme kwa kutumia vyanz vya ndani kuzalisha umeme (bahati nzuri amekaririwa Mramba kwamba kuna vyanzo lukuki)?
6.Kwa nini TANESCO haisomi hsitoria na kuwa kila siku inaingia miradi tegemezi ya uzalishaji wa umeme (Symbion,IPTL nk) ambayo huingiwa kwa mbwembwe mwishowe huwa majanga?
7.Kwa nini uongozi wa Tanesco umejaa mainjinia badala ya watu/wataalam wa biashara?(finacials,marketing,admistrative nk) hawa mainjinia wangefaa wawekwe kwenye vitengo/idara za chini kulingana na ujuzi wao.
8.Gharama zilizotumika tungejenga power production plant nagpi tz?
Naombeni tujadili
source:http://www.dailynews.co.tz/index.php/home-news/54270-tanesco-project-to-benefit-kenya