#COVID19 Mkasa wa kipekee kuhusu pilikapilika za kujikinga na COVID-19

UPDATE-3: THURSDAY 04 FEBRUARY 2021

KWA WAUMINI WOTE WA KANISA A:

……………………..Inaendelea

KIONGOZI MKUU (KM)

Wakati wa matangazo baada ya Ibada kuisha, ndiyo sasa likatolewa tangazo la aina yake kwa ajili ya ratiba ya wiki iliyokuwa mbele, na ambalo mhusika hajawahi kulisikia tangu aanze kuhudhuria Ibada Kanisani; kwamba:

  • kuanzia J5 mpaka Ijumaa, waumini wanaotakiwa kuonekana Kanisani ni wale tu watakaokuwa wametumiwa ujumbe wa SMS kwenye simu zao.
  • Hapa pia inaonyesha kama waumini hawa ni wale tu ambao wako kwenye program moja na KM, kwamba watasikilizia kwanza siku za J3 na J4 kuona hali ya hewa inakwendaje kuhusiana na scud alilokuwa amerusha KM madhabahuni, na hatimaye kama kuna chocchote, basi wanaweza kuwasiliana kwa njia ya SMS na kukutana Kanisani kuanzia hiyo J5 for a way forward, katika kujaribu kuona nini kifanyike au kisifanyike, baada ya KM kuwa amefanikiwa kurusha makombora yake kwenye J2 ile ya wiki iliyokuwa imepita!
Possibly watu hawa walitakiwa wakutane kanisani kwa mawasilaino ya aina hii ili waweze kuwa under-cover, kwamba wasiweze kujulikana kirahisi iwapo kuna chochote kile kule mbele ya safari ambacho kinaweza kikawa nje ya matarjio, ili kuwakinga na dhahama ya aina yoyote ile
 
Kwa mtu ambaye amesoma na kuyaelewa kwa makini maelezo hayo hapo juu, hatasita kukubaliana na mhusika kuwa naonekana kama kuna haja ya swala la maji yaliyoonekana yakibubujika kwenye sakafu ya jengo jipya huko Moshi, kuangaliwa kwa jicho jingine jipya
Ni kweli maji hayo inatakiwa yadhibitiwe
 
UPDATE: FRIDAY 05 FEBRUARY 2021

KWA WAUMINI WOTE WA KANISA A:

……………………..Inaendelea

KIONGOZI MKUU (KM)

Kukwepa kutangaza mabadiliko ya siku ya harusi iliyohamishwa KM aliamua kutoa tangazo kwamba tarehe 14 kutakuwa na kuweka wakfu watoto

  • Tangazo hilo la watoto ndiyo likampa nafasi sasa ya kusema kuwa watoto hao inabidi waletwe kwenye Ibada ya kwanza tu kwa sababu Ibada ya pili kutakuwa na harusi.
  • Wakati huo tayari alikuwa ameshatangaza kufuta mojawapo ya harusi na ambayo ndiyo ilitakiwa kufanyika kwenye tarehe tajwa
  • Kwa hiyo mpaka hapa automatically, akawa amewaset watu kisaikolojia kujua kuwa kumbe ile iliyobaki itafanyika tarehe 14
Kawaida hii iliyokuwa imebaki, ilitakiwa kufanyika tareha 7

Mpaka hapa msomaji yeyote mweye akili ya kawaida anaweza kuona kuwa tangazo la watoto lilichomekwa pale kwa nia ya kuya-cover mabadiliko haya ila halikuwa na priority yoyote kwae kwa sababu

  • J2 zinazoruhusu kuwaweka wakfu watoto kwenye Ibada zote mbili zipo lukuki na hivyo hapakuwa na haja ya kuwa-confine wazazi na kuwapa restriction ya kuja na watoto kwenye Ibada moja tu ya asubuhi ya tarehe 14 na ambayo baadaye tena kuna pilika pilika za kitu kingine
  • Hapakuwa na uharaka wowote wa kuwaweka wakfu watoto hao kwa sababu huwa hakuna deadline, na J2 zenye Ibada mbili zipo lukuki mbele ya safari
Lakini pi kwa upande mwingine, hii pia inaonyesha kama kwa sababu siku hiyo ya harusi kutakuwa na pilika pilika za watu wengi mahali hapo, kunaweza kukawa na watu “special” ambao si waumini wa kanisa la mahali popote pale na ambao walikuwa wanatengenezewa mwanya wa kuja na watoto na kupita mbele ya madhabahu. Nia ya watu hawa ni kupita mbele ya madhabahu wakiwa wamebeba watoto, lakini lengo lao kiroho likiwa ni tofauti na swala la watoto wao kuwekwa wakfu, kwa sababu wanakuwa wala siyo waumini wa kutoka kanisa lolote lile

Assumingi hay kuwa ni kweli, kitendo hiki kinadhihirisha wazi kuwa swala la watoto kuwekwa wakfu Kanisa A siku hiyo, siyo priority, isipokuwa priority ni kitu kingine toafuti kabisa na swala hilo

KUHUSIANA NA SOMO LA MWILI NAFSI NA ROHO ALILOKUWA AKIFUNDISHA KWA VITENDO

  • Muda mwingi KM alikuwa anautumia akiwa yuko chini ya madhabahu, mbele ya waumini
  • Washiriki aliokuwa anawatumia kufanya demonstration yake kwa upande mwingine pia alikuwa anawatumia kama kisingizio cha yeye kutokusimama juu madhabahuni
  • Ni kwa sababu kwa wakati huo, alikuwa hashughuliki na madhabahu, alikuwa anashughulika na waumini waliokuwa wamekaa chini, mbele ya madhabahu
  • Inaonyesha kama somo lake hilo lisingeweza kuzaa matunda yaliyohitajika kama angelifundisha akiwa amesimama juu madhabahuni, madhabahu ingemkwamisha kwa sababu kwa wakati huo alikuwa bado hajaishughulika
Baada ya kuwa amefanikiwa kushughulika na waumini, halafu akafanya na test yake ikafanikiwa ndiyo sasa akawa amebakiza madhabahuni

Msomaji inabidi akumbuke kuwa baada ya kuwa amefundisha somo tajwa hapo juu linalohusiana na nafsi, mwili na roho

  • Alipotea tena madhabahuni yaani akawa hasimami tena madhabahuni kufundisha maandiko matakatifu
  • Hata hivyo siku hizi amebuni mbinu ambayo walio wengi hawawezi kumgundua kirahisi pindi anapokuwa amepotea madhabahuni kwa sababu anajitahidi sana angalau kila sikuya J2 awepo Kanisani na awe na angalau matangazo ya kuwatangazia waumini, hata kama matangazo hayo siyo ya muhimu
  • Mtu anaweza kui-magine Kiongozi Mkuu wa Kanisa anasimama madhababhui kutoa tangazo la salaamu kutoka kwa mtu Fulani kuja kwa waumini,….kwa mfano “so and so anawaslimia…… halafu baada ya hapo anasema, Ibada imeisha, tusimame….”
Matangazo haya yanaweza kutangazwa na kiongozi yeyote ambaye huwa ana zamu ya kusimama madhabahuni. Kwa hiyo pamoja na kupotea madhabahuni, bado huwa anaonekana kwa ajili ya kutoa matangazo na hivyo walio wengi inakuwa siyo rahisi sana kwao kuweza kufuatilia ratiba yake ya madhabahuni

Kwa hiyo alipomaliiza tu kufundisha somo hilo, akapotea madhabahuni na kupokelewa na watu wengine wawili ambao kati yao hakuwpo yule mhubiri wa uzinzi. Kwa bahati nzuri ratiba ya maombi ya wiki tatu nayo pia ikawa imewahi zaidi mwaka huu, na hivyo kupelekea conditions zote mbazo huwa anazihitaji, kuwa satisfied

Kwa hiyo baada ya maombi haya kuwa yamefanyika, na akiwa amepotea madhabahuni kwa wiki kadhaa, na scud yake akiwa tayari ameitest kwa kutumia waumini waliohudhuria kwenye hafla fulani na akawa amehakikisha kuwa imefanya kazi, ndiyo sasa ikawa amebakiza stage moja tu ya mwisho; kupanda juu madhabahuni ili sasa akamilishe kazi yake.

Hii inaonyesha kuwa wakti anafundisha somo la nafsi, mwili na roho, madhabahu ilikuwa inamlete shida, alikuwa hawezi kusimama madhabahuni na kufnay kitu na ndiyo maana aliwatumia hao vijana wawili kama kisingizio cha kutokusimama madhabahuni. Baada ya kufanikiwa kuwashambulia waumini, akwa ana uwezo sasa kwa kusimama madhabahuni tena, ila bado akawa hajakamilisha kazi yake, alikuwa bdo amebakiza madhabahu

Alichofanya ni kuvunga kwa wiki kadhaa, akiruhusu makada wenzake wasimame madhabahuni amboa wako naye kwenye shirika moja na wakiwa wanajua nini kinendelea, huku nao wakiwa wanalitumia neno “uzinzi” kwa sana. Baad ya hapo ndiyo wakawa wamemkabdihi wakiwa mametest na kuona kuwa kila kitu kiko sawa

Kwa hiyo J2 iliyopita ndiyo akapanda madhabahuni kuishambulia madhabahu, ili sasa baada ya hapo, (au baada ya wiki chcahe kadhaa mbele) aanze tena kusimama madhabahuni mffululizo.

HITIMISHO

Mambo kadhaa ya muhimu yanayojitokeza hapa ni kwamba:

  • Kabla hajawashambulia waumini, ilikuwa ni vigumu (au haiwezekani) kwake kuishambulia madhabahu kwa sababu ilikuwa haimruhusu kusimama juu yake
  • Kabla hajawashambulia waumini, ilikuwa ni vigumu (au haiwezekani) kwake kuwasshambulia kutokea juu madhabahuni, madhabahu ilikuwa haimruhusu
Kwa hiyo ndiyo maana alitengeneza utaraibu wa kufundishs somo kwa vitendo ili muda mwingi asiwe amesimama kwenye madhabahu.

Sehemu hiyo aliyokuwa anawaweka waumini na kuwasimamisha hapo kwa muda wote wa takriban saa nzima wakati wa Ibada, ndiyo shemeu ile ile ambayo watu huwa wanaasimama pindi wanapokuwa wameitwa kupita mbele ya madhabahu, na pia ndiyo sehemu popular ambayo muda wote huwa anaitumia kwa ajili ya mashambulizi yakiwemo yale ambayo mhusika ameshayaelezea hapo awali

Baada ya kuwa amewashambulia waumini, ndiyo sasa akapata nguvu ya kuishambulia madhabahu, kwa sababu akawa sasa tayari ametengeneza malngo kupitia kwa waumin, wa kuweza kuishambulia madhabahu na hivuo kuweza kusimama tena madhabahuni

Wachungaji wenzake wote huwa wanaweza wakasimama madhabahuni na kuwasalimia waumini

“wapendwa wa Ibada ya kwanza/ ya pili, nawaslimu kwa jina la Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo”, halafu wakishamaliza kusalimia hivyo wanongeza tena neno jingine “Bwana Yesu Asifiwe”

Yeye KM ni marufuku kwake kupanda madhabahuni halafu akatoa salaamu ya “Bwana Yesu Asifiwe” hakuna, HIYO SALAAM HAJAWAHI KUITUMIA MAISHA YAKE YOTE
Hawezi akapanda madhabahuni halafu akatoa salaam hiyo. Hata hivyo angalau siku hizi amenza kuichomeka chomeka kwenye mafundisho anapokuwa anafundisha kitu, ile ya kuchomeka kwa haraka haraka, SIYO KAMA SALAAM bali kama neno la kuwaweka waumini wawe wako attention muda wote katika kumsikiliza ancchosema

EBR. 6:4-6 SUV

Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
UPDATE-2: FRIDAY 05 FEBRUARY 2021

KWA WAUMINI WOTE WA KANISA A:

……………………..Inaendelea

KIONGOZI MKUU (KM)

Anaonekana kama ana mtandao ulioimarika ndani ya Kanisa. Kwa mtumishi anayeheshimu na kuogopa mamlaka iliyo juu yake, asingeweza kuwa anafanya yote haya hadi kufikia kiwango hiki.

Haya mambo hata kama ni tuhuma tu zisizokuwa na ushahidi wowote, hayastahiki kutuhumiwa mtu yeyote anayeitwa mtumishi wa Mungu. Hayana ukaribu wowote na mtu ambaye ni mtumishi wa Mungu, au mtu yeyote anayemjua Mungu. Ni mambo yana ukaribu na watu ambao ni wavuta bangi wa mitaani tu basi!

EBR. 6:4-6 SUV

Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
Nenda kule jukwaa la entertainment kuna thread zinazokufaa huko, hii haikufai itakupotezea muda wako wa kufanya assignment ulizopewa shuleni na walimu wako. Ukifeli masomo usije ukalaumu mtu humu jukwaani tafadhali
Acha hasira mzee wangu
 
UPDATE: SATURDAY 6th JANUARY 2021

KUHUSIANA NA MICHANGO IILIYOKUWA IMECHANGWA KWA AJILI YA HARUSI ILIYOFUTWA

Michango hii yaweza kuwa:

  • Ilikuwa ni sadaka iliyohitajika na KM kwa ajili ya kushambulia madhabahu
  • Ilikusanywa kwa ajili ya kufidia Sadaka za waumini ambazo pengine zimepungua kiasi na hivyo kupelekea kubuniwa utaratibu mwingine mpya wa kuongeza kipato cha hawa watumishi wa Mungu
  • Ilikuwa inahitajika kwa ajili ya mambo yote haya mawili, kwamba kilihitajika kipato cha ziada na pia sadaka kwa ajili ya madhabahu za kuzimu; sadaka ambyo ilibidi itokane na fedha za waumini ambazo hazijatokea madhabahuni, na hivyo hazijaombewa
Kama hali ndiyo hiyo, mhusika alitoa mchango wa TZS 51,000/= ambazo atajuta sana kuwa amezitoa, assuming nadharia ya matukio haya kutokuwa coincidences iko sahihi

Ikumbukwe pia kuwa J2 ya tarehe 18/10/2020 kuna dalili zinazoonyesha kuwa walifanya pia kitu kinachofanana na hiki. Waliitsha mchango wa ujenzi ghafla, tukio ambalo mhusika aliahidi kuliongelea baada ya Desemba 2020, muda ambao michango hiyo ilikuwa inaishia. Hakutaka kuliongelea ndani ya muda wa michango hiyo ili kukwepa lawama kuwa anahamasisha watu kutokutoa michango kanisani. Hili nalo ataliongelea panapo nafasi

KUHUSIANA NA “MHUBIRI WA UZINZI”

Assuming matukio haya siyo coincidences tu bali yalipangwa, huyu mtu anaelekea kubaya

  • Anawatoa kafara ya kuwadhalilisha watoto wake kanisani
  • Anakoelekea anaweza akaja akawatoa kafara ya damu, uhai, huko mbele ya safari
Hivyo mhubiri huyu wa uzinzi inabidi adhibitiwe ipasavyo ili asije akafikia kwenye level ya hatari zaidi ya hii

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
Hivi kwa mfano, kuna ugumu gani kwa Kanisa Jipya kuliita Kanisa jipya? Kipi ni rahisi zaidi kati ya kuliita

"Kanisa ambalo waumini wanasubiria madhabahu tu kuwekwa ili wahamie na kuanza kuabudu humo"

Kanisa jipya na jengo jipya? Kipi ni rahisi zaidi, na kwa mtu ambaye ni mtumishi wa Mungu?
Haya maneno yamenifurahisha sana

Hakuna ugumu wowote kuita kanisa jipya hata kama hakuna madhabahu bado
 
Naendelea kusoma, inaonyesha Mhusika ni mtu mkorofi sana, yaani mtu mmoja tu anataka apange kanisa liendeshwe vipi

Hata kama amegundua kuna ushirikina kanisani sasa kwahiyo yeye alijua makanisa yana utakatifu? Mbona ni kawaida tu makanisa na waendeshaji kuwa washirikina?

Mhusika ni mtu wa kupenda sana haki, asiyeweza kukaa kimya jambo ambalo sio baya lakini kwa bahati mbaya hapa duniani watu wa namna hii hupata tabu sana

Ndio sababu kuna watu hukaa kimya, sio lazima useme kila unachokiona, maamuzi sahihi ni kuachana na jambo hilo kama linakukera sana

Najua Mhusika hawezi kuachana na dini basi ataendelea kupata tabu maana kote atakoenda salama yake ni kukaa kimya, ama sivyo ni kibano kila kona na hivyo asitulilie
Sio mkorofi ni Mwendawazimu fresh
 
Haya maneno yamenifurahisha sana

Hakuna ugumu wowote kuita kanisa jipya hata kama hakuna madhabahu bado
Madhabahu tayari ipo, na kuna kipindi liliwahi kutumika kwa Ibada kadhaa lakini hatimaye ikaonekana eti kuna mwangwi, likawa abondoned. Mungu anisaidie sana mimi nisije nikapata mamlaka siku moja, maana nitakuja kufanya makosa ya kuingilia hadi sehemu zile ambazo hazinihusu
 
UPDATE: THURSDAY 14th JANUARY 2021

WASOMAJI WA UZI HUU ANAOMBA AWSHIRIKISHE JAMBO MOJA JINGINE LA NYONGEZA, NJE YA MADA ZINAZOENDELEA KWENYE UZI HUU:

Mhusika wa taarifa hizi anauliza swali akiwa anahitaji msaada kutoka kwa wasomaji kwamba: Je website hii aliyokuwa akiitumia kipindi kirefu nyuma kupata Salary Slips zake, ni kweli ilikuwa ya Serikali?

Website yenyewe ni hii hapa:

Ni website ambayo aliwahi kujisajili na hatimaye akawa ana-print salary slips zake kutoka kwenye site hiyo kuanzia March 2017

  • Ni baada ya taasisi anayofanyia kazi kuacha kutoa Salary Slips na kuwashauri watumishi wake wajisajili kwa ajili ya kupata salary slips hizo online, kutoka Serikalini moja kwa moja
  • Baada ya kuwa amejisajlili, Salary slip ya kwanza ailiyopata kutoka kwenye website hii ni ya March 2017
  • Aliendelea kupata Salary slip hizi hadi December 2018
  • Baada ya hapo, kuanzia February 2018 site ikawa inarudisha ujumbe kuwa iko kwenye matengenezo hadi leo
  • Salary slips alizowahi kupata anazo soft copies zke hadi leo, yaani za kuanzia march 2017 mpaka December 2018
  • Kuanzia pale hana tena Salary Slip yoyote hadi leo kwa sababu site hiyo inaonekana iko kwenye matengenezo muda wote
  • Ameshajaribu kujisajili kule kwingine Wizara ya Fedha, lakini anapata ujumbe kuwa Chek Namba, e-mail address pamoja na namba yake ya simu alivyotumia tayari vilishatumika na mtu au watu wengine
Attachment mbili zilizopo hapo chini zinaonyesha home page au login page ya website hiyo namna ilivyotokea alipojaribu kuitafuta jana tarehe 13/01/2021, lakini hakuweza ku-login, ilikuwa inaleta time-out error. Amejaribu tena leo tarehe 14/01/2021, imeanza tena kumletea ujumbe ule ule wa zamani ukisema

“MFUMO HUU KWA SASA UPO KWENYE MATENGENEZO SAMAHANI KWA USUMBUFU ULIOJITOKEZA. ASANTE”.

Huu ndiyo ujumbe ambao amekuwa aikiupokea tangu February 2018 na hana Salary Slips tena kuanzia pale hadi leo

Je, ni kweli kwamba hii site ilikuwa genuine na ni ya Serikali?
Siku hizi kuna salary slip portal sio watumishi portal, hiyo ilishazuiliwa sio kwako tu ni kwa wote
 
Madhabahu tayari ipo, na kuna kipindi liliwahi kutumika kwa Ibada kadhaa lakini hatimaye ikaonekana eti kuna mwangwi, likawa abondoned. Mungu anisaidie sana mimi nisije nikapata mamlaka siku moja, maana nitakuja kufanya makosa ya kuingilia hadi sehemu zile ambazo hazinihusu
Hahaha swala la mwangwi halikuwa na mantiki, ilibidi watafute namna ya kulifix

We kweli wasikupe mamlaka sababu unafatilia kila kitu tena kwa undani, hiyo inaweza isiwe nzuri sana sababu kikawaida kama kiongozi kuna mambo mengine inabidi uyapuuzie tu yapite.

Nimesoma uzi wote hatua kwa hatua na kwa utulivu mpaka nikauelewa, mwanzoni uzi ulinipa shida kidogo ila kadri nilivyozidi kuusoma niliuelewa vizuri,

Mkuu Hongera sana kwa muandiko mzuri na lugha inayoeleweka, umepangilia uzi vizuri sana japo kwa upande wangu nilikuwa natamani unapotu-update basi rejea ziwe kwa ufupi sanaa.

Kwavile umeruhusu maswali basi naomba nikuulize maswali machache kabla sijarudi kuwaongelea wahusika katika mikasa hii aliyokumbana nayo mhusika....
1. Yale mashambulio ya koo ambayo mhusika alikuwa anakutana nayo mpaka kuhofia kupoteza sauti ni mashambulio ya aina aina gani? Anakuwa anaumwa koo au anakohoa au anajiskiaje mpaka kuelewa kuwa amepatwa na shambulio hilo???

2. Lile shambulio la kiroho alilolipata baada ya kukanyaga maji machafu kwenye banda la watoto, aliendelea kuvaa vile viatu au alivitupa??

3. Lile shambulio ambalo lilifanyika kwenye gari la mhusika, nadhani ni ile siku KM wa kanisa A alipopaki gari yake mkabala na mhusika(ile siku aliyokuta kioo kiko wazi lilileta madhara yoyote? Kama ndio ni madhara gani hayo?)

4. Mhusika anafahamu fika kuwa amezungukwa na maadui kila sehemu awe ndani ya nchi au nje ya nchi, uzuri wahusika hao anatokea kuwajua, kwanini bado tu anawasalimu kwa kuwapa mikono na kuongea nao wakati anajua akifanya hivyo anapokea mashambulio ya kiroho?? Mfano ile siku ambayo mhusika anaona kama shambulio alilopata lilimfikia kwa kutumia watoto, lakini hapo hapo bado mhusika alidiriki kwenda kuwanunulia watoto wale zawadi na kuhakikisha zinawafikia, hivi mhusika haoni kama anatuchonganisha?? Yani watu wale wale ambao yeye wanamtendea mabaya kiasi cha sisi kuona ambavyo hatendewi haki, ye mwenzetu bado tu anawakumbatia

5. Kwanini bado mhusika anaendelea kuwa muumin wa kanisa A na hata lile B wakati ameshajua makanisa hayo yanafuga tu mapepo na ibada zao ni maigizo???
Ye anaetushuhudia hayo bado anashiriki kwa uaminifu na sadaka anatoa japo kwa sasa amepunguza kidogo

6. Je Mhusika amewahi kwenda hospital kupima na kuangalia afya yake kama alivyoshauriwa kazini na hata baadhi ya wadau waliochangia hoja humu??

Mwisho kabisa. NAOMBA ITAMBULIKE KUWA MIMI SIPO HAPA KWA AJILI YA KUKUPA SHAMBULIO LA KIROHO LA AINA YOYOTE ILE MI NI MWANANCHI WA KAWAIDA KABISA, IMENIBIDI NIWEKE SAWA HILI ILI USIJE UKAACHANA NA JAMII FORUM KWA KUDHANI SHAMBULIO LIMEHAMIA HUKU
 
Kabla sijachukua maelezo ya maswali yako kutoka kwa mhusika, naomba ujibu kwanza maswali haya mafupi yafuatayo
Je umesoma vizuri na kujua kiini kilichopeelekea uzi huu kuwemo humu jukwaani? Je, umesoma kuanzia mwanzo na ukasoma maelezo yote hadi kufikia sehemu iliyopelekea uulize maswali haya., au kuna sehemu ambazo umeruka?
Inaonyesha kama umeruka ruka, na kama hujaruka ruka basi kuna mambo umesoma lakini hukuelewa. Anayesoma bila kuruka hawezi kuuliza maswali haya uliyouliza wewe
 
UPDATE:MONDAY 8th JANUARY 2021

KUHUSIANA NA MICHANGO IILIYOKUWA IMECHANGWA KWA AJILI YA HARUSI ILIYOFUTWA

Michango hii yaweza kuwa:

  • Ilikuwa ni sadaka iliyohitajika na KM kwa ajili ya kushambulia madhabahu
  • Ilikusanywa kwa ajili ya kufidia Sadaka za waumini ambazo pengine zimepungua kiasi na hivyo kupelekea kubuniwa utaratibu mwingine mpya wa kuongeza kipato cha hawa watumishi wa Mungu
  • Ilikuwa inahitajika kwa ajili ya mambo yote haya mawili, kwamba kilihitajika kipato cha ziada na pia sadaka kwa ajili ya madhabahu za kuzimu; sadaka ambyo ilibidi itokane na fedha za waumini ambazo hazijatokea madhabahuni, na hivyo hazijaombewa
Kama hali ndiyo hiyo, mhusika alitoa mchango wa TZS 51,000/= ambazo atajuta sana kuwa amezitoa, assuming nadharia ya matukio haya kutokuwa coincidences iko sahihi

Ikumbukwe pia kuwa J2 ya tarehe 18/10/2020 kuna dalili zinazoonyesha kuwa walifanya pia kitu kinachofanana na hiki. Waliitsha mchango wa ujenzi ghafla, tukio ambalo mhusika aliahidi kuliongelea baada ya Desemba 2020, muda ambao michango hiyo ilikuwa inaishia. Hakutaka kuliongelea ndani ya muda wa michango hiyo ili kukwepa lawama kuwa anahamasisha watu kutokutoa michango kanisani. Hili nalo ataliongelea panapo nafasi

KUHUSIANA NA “MHUBIRI WA UZINZI”

Assuming matukio haya siyo coincidences tu bali yalipangwa, huyu mtu anaelekea kubaya

  • Anawatoa kafara ya kuwadhalilisha watoto wake kanisani
  • Anakoelekea anaweza akaja akawatoa kafara ya damu, uhai, huko mbele ya safari
Hivyo mhubiri huyu wa uzinzi inabidi adhibitiwe ipasavyo ili asije akafikia kwenye level ya hatari zaidi ya hii

EBR. 6:4-6 SUV

Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
3. Lile shambulio ambalo lilifanyika kwenye gari la mhusika, nadhani ni ile siku KM wa kanisa A alipopaki gari yake mkabala na mhusika(ile siku aliyokuta kioo kiko wazi lilileta madhara yoyote? Kama ndio ni madhara gani hayo?)
Halafu ebu ujaribu kunionyesha mahali ambapo umesoma kitu kama hiki, yaani mahali kilipoandikwa
 
Kabla sijachukua maelezo ya maswali yako kutoka kwa mhusika, naomba ujibu kwanza maswali haya mafupi yafuatayo
Je umesoma vizuri na kujua kiini kilichopeelekea uzi huu kuwemo humu jukwaani? Je, umesoma kuanzia mwanzo na ukasoma maelezo yote hadi kufikia sehemu iliyopelekea uulize maswali haya., au kuna sehemu ambazo umeruka?
Inaonyesha kama umeruka ruka, na kama hujaruka ruka basi kuna mambo umesoma lakini hukuelewa. Anayesoma bila kuruka hawezi kuuliza maswali haya uliyouliza wewe
Lete majibu tu

Nimesoma mwanzo mpaka mwisho na nimeelewa kwa namna yangu, kumbuka lugha iliyotumika sio rahisi hivyo ila nashukuru pia kwa hatua hiyo ya uelewa niliyofikia, ila nahitaji kupata majibu ya maswali hayo ili niweze kuendelea mbele zaidi na kuyachakata yale uliyoandika
 
Kafanye assignment ulizopewa shuleni, utafeli masomo yako. Nakushauri uachane na uzi huu, au soma ila usiulize maswali, unachuouliza ni utoto
 
Back
Top Bottom