Mkasa ulionikuta COCO beach usiku

Talking nonsense solves no problems, as everyone knows,so why is it unjust to deprive you of the right to speak?

Mkuu unadhani ukiandika kithungu ndo utapata pointi ? Usitetee uovu ...penye ukweli paachwe pawe ivo...cocobeach askari wamepaharibu sio sehemu tena ya kwenda na kuwa na amani..vitisho vingi..
 
Nilipokuwa nasoma nilikuwa natetemeka sana sijui hasira!!! daah aisee pole sana, nadhani hukulala siku hiyo mkuu kwa hasira.Ila ulimvimbia kinoma,alikoenda alijua amekutana na kidume.Wajinga sana hawa jamaa.

Tuna hasira wengi sana
 
Pole kwanza kwa mkasa ila pili sishangai sana kwa kilichokupata hua inatokea mda mwengine anakua na wenzake wanaangalia kwa mbali.

Nakusifu hukuchukua uamuzi wa kuondoa gari lako kwani ungempa mwanya wa kufyatua kama alivyodhamiria. Ushauri wangu ukikutana na askari mwenye silaha usioneshe kua juu au jeuri zaidi yake utajikuta matatizoni kwa kujeruhiwa bila sababu ya msingi.

Nakumbuka niliwahi kimbizwa na wale antirobery kama jambazi usiku wa manane wakaniblock kwa makeke yote wametoa mitutu na amri juu ya kuzima taa na gari nikatii ila waliponikaribia wakaniomba masamaha na kusema wamekosea sio mimi, hapo mwili wote wa baridi najua napigwa risasi leo.
 
Je ulimuuliza kama anakitambulisho cha upolisi?
 
Pole Mkuu!

Ila kama nimekupata vizuri ,inawezekana huyo askari feki,alikuwa na bastola feki,au kama ilikuwa bastola halisi haikuwa na risasi.

Mtu anapojaribu mara mbili kukupiga risasi bila mafanikio-kwa upande wangu ama zake ama zangu;kwanza kosa lenyewe si la kutishiana kifo namna hiyo,ungeamua kumkuja kisawasawa,ungekuwa na utetezi mzuri wa self defence.

Pili,mtu kama huyo hukupaswa kumwacha,ungeenda polisi ukaripoti ili kama ni askari kweli anapata wapi kiburi cha kutishia watu maisha.Lakini pia,si kawaida askari akukute kwenye parking aanze kukuomba leseni-huyo ni muhuni.
 
Kama unaona hakuna haja ya kubeba bastola poa, ukichezewa makalio uwe mtulivu.

aah kumbe wewe unabeba bastola ili usichezewe makalio??!! wenzio wanazo hizo wanaziweka pembeni na watu wanawachezea makali.....wakuchezewa ni wakuchezewa tu hata uwe na AK47.
 
Pole mkuu...kama wewe ulikuwa unatokwa jasho nahisi huyo wa pembeni yako alikuwa amezimia kabisa


kwikwiwkwiwkwiiiiiii wewe tabia yako mbaya sasa kwa nini mwenzake azimie ila atakuwa alilowa chapachapa.
 
duh pole mkuu.
ila tumefika huko kwa askari kuuliza leseni na ukigoma unatolewa bastola ama kutishiwa maisha?
bado naendelea kuitafakari kama alikuwa jambazi angemalizia dhamira yake,

kama ni tapeli tu wa kawaida tapeli hutumia maneno mengi sana na si silaha

kama alikuwa tapeli anayetumia silaha feki basi kazi ipo ila alikuwa anataka utoe pesa au akuibie nini kingine zaidi ya pesa mbona hakufanya hivyo sasa na mwisho umesema wewe mwenyewe ulitoa leseni zote hivyo ulitii na kwa vile ulishaonesha kushindwa chochote kingine angeweza kufanya
alikuwa nani huyo kwa nini alifanya hivyo.
poleni sana.

lakini siku nyingine na wewe mkuu usiende sehemu hatarishi kama hizo ufukweni usiku wa saa mbili? unaweza hata kukumbwa na jini jamani , zipo sehemu nyingi ambazo unaweza kwenda na baby wako kwa raha zenu na faragha bila mahoteli makubwa, malls, etc
haya ni mawazo yangu
 
umeona ehee maeneo hayo labda angemuomba kitambulisho cha kazi au cha taifa nk
yani sijaisoma hali kabisa
 
Mod post kama hivi za zakutunga na kuchafua jeshi letu.It's the usual complaint system does good, system is abused.

i thought it is an alert to the rest, yet you noticed fabrications!!!!!!!!! how will the real incident be?

Aisee mie nachukua hiyo tahadhali na kumshukuru mtoa mada kwa hilo ambalo hata maaskari wetu watalifanyia kazi kubaini wanaojihusisha matukio kama haya.
 
Hii kitu umetunga na kama sio ya kutunga basi wewe ni kilazaaa mpenda sifa za kijinga...mtu kakuwekea cha moto halafu bado unakomaa???

Sintorudia tena mkuu.
 

Until they can be proved,allegations remain merely assertions
 
Mkuu unadhani ukiandika kithungu ndo utapata pointi ? Usitetee uovu ...penye ukweli paachwe pawe ivo...cocobeach askari wamepaharibu sio sehemu tena ya kwenda na kuwa na amani..vitisho vingi..

What should you do once an allegation has been made?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…