MKASA: Nilimuua rafiki yangu mwaka 1990, ananitokea akinitaka nikatubu

MKASA: Nilimuua rafiki yangu mwaka 1990, ananitokea akinitaka nikatubu

jafarikyaka

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2014
Posts
378
Reaction score
269
Habari zenu

Mimi ni kijana wa miaka 36. Mnamo mwaka 1990 mimi na rafiki yangu Jose tuliingia katika kazi yetu ya uvuvi, ilikuwa ni tarehe 23 mwezi wa nne siku hyo kulikuwa na hali mbaya kidogo
Ziwa Nyasa.

H
atukuchukua muda ziwani tulipigwa na wimbi la maji kila mtu akarushwa kivyake ila baadae kidogo nilijikuta nipo pembezoni na rafiki yngu akiwa pembeni akiugulia maumivu ya mbao ilomchoma ubavu wa kushoto na miguu yake ilikuwa nyanganyanga.

Kwa kuwa alikuwa akilalamika mno na hali yake si ya kupona nilishikwa na roho ya ajabu nikammalizia kwa kumkaba koo mpaka akafa.

Baada ya miaka kupita,mnamo mwaka 2007 Jose kaanza kunitokea na kunirudisha sehemu ile ile niliyomuulia na ananitaka nikatubu,

Nashindwa hata nifanyeje ndugu zangu, nakosa kabisa amani na familia yangu.

Nisaidieni wakuu.

NB: KUTUBU BADO SIJATUBU KWAKUWA NAONA KAMA NDOTO.
 
Pole mkuu,
Ila usiogope saana hizo ni imani tuu...
mtegemee mwenyezi mungu, kuwa karib na yeye kwa kusoma vitabu vitakatifu

Ukipata muda watembelee ndugu zake kama wapo karibu..

Usipende kujiwekea mawazo
 
Kaka unatoka sehemu gani ya ziwa Nyasa? Hii itanisaidia kukushauri kwa kuzingatia mila na desturi za mahali husika. kwa ujumla utapaswa ukatubu kaka. Lasivyo, huyo ghost hatakuacha. Lakn tusaidie maelezo zaidi tuboreshe ushauri, yaani wewe kilichokufanya ummalizie ni kumuonea huruma? sijakupata vema?
 
Nenda tu ukatubu, bila hivyo utaendelea kukosa amani. Lakini ulipata wapi ujasiri wa kumuua? Kama ulishindwa kuangalia anavyoumia ni bora hata ungejifanya unaondoka kwenda kutafuta msaada kwa watu
 
Ndani na bahari, ziwa na.mito kuna mambo mengi ya ajabu. Huwenda alikumbwa na upepo wa ajabu. Lazima utubu ili upate amani. Pole sana
 
Ushauri wangu kwako in huu zingatia
1- kama unakunywa pombe acha na kama haunywi kabisa basi anza kutundika mitungi mwanzo mwisho ndio salama yako hiyo
2- kama unavuta bangi acha na kama hauvuti bangi kabisa anza kulipuliza tena kama dozi asubuhi, mchana, na jioni stiki moja moja yaani stiki tatu kwa siku.
Narudia tena zingatia vinginevyo utachizi muda sio mrefu.
Usicheze na damu ya mtu.
 
Ushauri wangu kwako in huu zingatia
1- kama unakunywa pombe acha na kama haunywi kabisa basi anza kutundika mitungi mwanzo mwisho ndio salama yako hiyo
2- kama unavuta bangi acha na kama hauvuti bangi kabisa anza kulipuliza tena kama dozi asubuhi, mchana, na jioni stiki moja moja yaani stiki tatu kwa siku.
Narudia tena zingatia vinginevyo utachizi muda sio mrefu.
Usicheze na damu ya mtu.

Haha ngumu kumesa aisee
 
jafarikyaka

Tukisema Wafu wanaishi ktk Ulimwengu wa Roho watu wanapinga na kuona km ni Ushetani,haya sasa ngoja yakukute!!,Upo Ushahidi wa Kibiblia Unaoonyesha kuwa Wanadamu tukifa Roho zetu zinaendelea kuishi ktk Ulimwengu wa Roho na Wanakuwa na Uelewa ndiyo maana hata Yesu anapozungumzia mfano wa tajiri na Lazaro,Yule Tajiri anaonyesha hali ya utambuzi kwa kumwomba Ibrahim atume mtu Huku Duniani ili kuwaokoa ndugu zake,Ushauri wangu nenda ukatubu.
 
Last edited by a moderator:
Pole mkuu,
Ila usiogope saana hizo ni imani tuu...
mtegemee mwenyezi mungu, kuwa karib na yeye kwa kusoma vitabu vitakatifu

Ukipata muda watembelee ndugu zake kama wapo karibu..

Usipende kujiwekea mawazo

ndugu zake nilionana nao ila hawaonyeshi msaada wowote
 
Back
Top Bottom