Mkapa, Vincent na Madaraka: What Else?

Joined
Apr 27, 2006
Posts
26,584
Reaction score
10,464
- Ninajiuliza swali moja hawa wote ni Familia moja, sasa wanapochafuana huko Arumeru as they have done, linakuja swali moja kubwa je hawa wanafamilia moja wana siri ngapi zingine hawajatuambia wa-Tanzania? Au tusubiri kampeni nyingine ya siasa tuwapange tena tusikie zaidi? Just curious!

- Lakini hawa wana siri nyingi tunahitaji kuzijua Wananchi wa Tanzania!, sasa wapangwe tena another kampeni!, I mean kinachoendelea huko Arumeru ni serious business:

- HOWEVER: hivi kweli CCM haikuwa na mwingine wa kumpeleka Arumeru zaidi ya Mkapa? I mean kweli Viajna wote walioko CCM Why him?


FMEs!
 

Mkapa ni Familia ya Nyerere?

Mkapa Nyerere?
 

Kuweka kumbukumbu sawa sawa Mkapa sio mwanafamilia na Nyerere
 
Mkapa nae ni familia ya Nyerere? Ni lini Watanzania tutakuwa 'serious' na vitu tunavyosema na kufanya? Au mizaha ndio destiny yetu??
 
Mkapa nae ni familia ya Nyerere? Ni lini Watanzania tutakuwa 'serious' na vitu tunavyosema na kufanya? Au mizaha ndio destiny yetu??

- Wakuu ndio tatizo letu wa-Tanzania, mara ngapi wakati wa kumbu kumbu za Mwalimu tumesikia Familia ya Mwalimu wakisema Mkapa ni mwana-familia yao? Magazeti mengi sana yamewahi kusema haya kwamba Mkapa ni familia ya Mwalimu sasa why leo mnashangaa?

- Hebu atokee mwanafamilia ya Mwalimu aseme bila uoga kwamba hawajawahi kusema Mkapa ni member wa familia yao! Tuwakumbushe siku na tarehe na aliyeyasema na wapi, WA-Tanzania sio mabwege tena siku hizi, hawa ni familia moja bana! sasa watumabie what else they know au wanaficha kuhusu Taifa!


Es!
 
mmmmmmmmmmmmhh!..

mkuu mimi naunga mkono hoja kwenye swala la kwanin mkapa????WHY??...

halaf mkuu hebu uliza vyanzo vyako vya taarifa ..kwamba kwanin siku ya uzinduzi wa kampeni kwa hichi chama chetu tawala..ni the same day mh rais aliongea na sis wazee pale dar...?kwamba hili la arumeru halimuhusu sana hata akazicapture media zote yeye?
 

Fungua macho mkuu wangu....

Lile la Arumeru limekaa ki-Lowassa zaidi.... Lina maslahi ya Lowassa lile.

Sasa yaani...dah!
 
Mkuu FMES,

Habari za Nyerere kumalizwa na Mkapa tulishasikia miaka mingi iliyopita Vicent karudia tena vyombo vya habari vimeamua kuipatia umuhimu kwasababu aliyesema ni mwanaukoo wa Nyerere.Mkuu FMES hakuna siri nyingine zaidi ya hii kwamba Nyerere alitangulizwa kabla ya siku zake ili wauze benk yetu ya NBC kwa bei poa,waingie mikataba mibovu ya uchimbaji wa madini,wanunue ndege ya rais ikibidi tule majani,wanunue rada kwa bei kubwa kupita kiasi na wauze viwanda vyetu kwa marafiki zao kwa bei poa.

Yote haya yasingefanyika kama Nyerere asingetangulizwa mapema,bahati mbaya Nyerere hakumjua Mkapa hadi aliposhiriki kumuingiza magogoni kwa gharama kubwa sana ikiwemo kuwapakazia na kuwachafua washindani wake ndani ya CCM na nje ya CCM.
 

- Kwenye hili CCM hawakuwa makini ingawa sijui the prons, lakini kumpeleka kampeni kama hii Mkapa, siamini kwamba politically ilikuwa a sound idea, ninaamini huku walitakiwa Vijana zaidi infact hata wagombea wenyewe wako in their 20s, labda kuna something sijui lakini kwa maoni yangu it was overreaching on CCM's part!

Es!
 
Fungua macho mkuu wangu....

Lile la Arumeru limekaa ki-Lowassa zaidi.... Lina maslahi ya Lowassa lile.

Sasa yaani...dah!

sasa kwa hali kama hiyo tunaweza kusema kweli tuna mwenyekiti wa ''chama chetu tulichokizoea'' mwenye busara kweli?
 
Mkapa ni Familia ya Nyerere?

Mkapa Nyerere?
Alipewa heshima hiyo na wanafamilia. Soma kipande hiki cha gazeti la ThisDay la jumapili, tarehe 27 April 2008(online version):


Ofcourse, kwa heshima hiyo tu huwezi kumwita Mkapa Nyerere! FMEs nadhani ameandika ki fasihi zaidi kunogesha kile anachotaka kusema.
 
Unaongelea Uanafamilia wa Hiari au wa Damu ? Mbona ukoo wa Burito ukikaa huwa Mhe. Mkapa haalikwi ?
 

Kamanda nakufurahia sana tangu nilipojiunga jukwaa hili toka enzi zile za bcstimes baadaye jamboforums, siku hizi niko na jina halisi kama unavyoona hapo juu. Nilipoona vijimambo vya Mkapa dhidi ya familia ya Nyerere nikakumbuka sana kamanda wangu, nikawa najiuliza wapi Mzee wa sauti ya Umeme? Nimemiss sana dataz zako kusema kweli
 
Vicent Nyerere kutokuwa mwanafamilia wa mwalimu nyerere ina uhusiano gani na uchaguzi wa ARUMERU!!!!!!!!!??? Ni kiherehere tu hicho ndo kimemponza Benja.
 
Mzee Mkapa akiendelea kuhubiri siasa kama naye ni Ditopile Ukiwaona ajue ndo mwisho wa heshima kwake...Kila mtu ana fani yake na siamini kabisa yeye anavaa vema viatu vya Marehemu Kaka Dito!
 

Kuweka mambo sawa hapo Mkapa alienda kuzima propaganda za vyombo vya habari kwamba ametoa masharti ya kwenda Arumeru mpaka makundi yavunjwe ndo aende ndo maana alienda kujibu na kusema waliosema hivyo ni wajinga.
Twendelee....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…