Mkapa umejifunza nini Arumeru? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa umejifunza nini Arumeru?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mlitika, Apr 2, 2012.

 1. Mlitika

  Mlitika JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 458
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Fursa aliyoipewa na watanzania ya kuwa rais wa taifa Ndugu Ben imempa heshima kubwa na kwa mila za kiafrika yeye ni kama “baba” kwa watanzania wote. Anayo haki ya kuheshimiwa na watanzania wana wajibu wa kumheshimu na halipashwi kuwepo jambo la kumfanya asigane na watanzania.

  Nionavyo mimi kitendo cha raisi mstaafu kujihusisha na siasa za majukwaani tena katika kada za chini kama majimbo hasa katika mazingira ya siasa za kibongo kunamweka katika mazingira ya kusigana na watanzania maana wako huru kutofautiana kifikra na mtazamo. Mbaya zaidi Mr. Ben mwenyewe hana diplomasia ya kikampeni; yaani ana ubabe fulani hivyi akiwa jukwaani.

  Matokeo yake ndo kama tulichoshuhudia Arumeru. Mzee wa heshima kubwa kama yeye kuanza kukashifiwa na hata kutukanwa na watoto wadogo majukwaani na katika mitandao. Anasababisha laana ya bure kwa watoto wanaoshindwa kuzuia kishawishi cha kumkashifu na kumtukana baba yao! Kwa CCM kubwagwa Ben amevuna aibu kubwa kuliko Sumari! Jambo hili halina faida kwa nchi na linabomoa heshima yake Mr. Clean. He should only be called to intervene on serious issues of national or international interest.

  Samahani Mr. Ben, ni mtazamo tu. Ila siyo siri, unajiaibisha bure!
   
 2. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,724
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  "La kuvunda halina ubani". Sasa kama chama kimeoza unafikiri uheshimiwa utatibu hali. Watanzania hawaangalii anyepiga kampeni ana cheo gani. Ikumbukwe, migogoro ya ardhi huko Arumeru ilisababishwa na Mh Mkapa ya kuuza ardhi kwa wageni akitumia mwavuli wa uwekezaji
   
 3. Mlitika

  Mlitika JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 458
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwenda kwake Arumeru alikwenda kuwazidishia hasira Wameru na amesaidia kuangushwa kwa CCM na yeye kuvuna aibu na matusi!

  CCM IS DESPERATE!​
   
 4. Shenkalwa

  Shenkalwa JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Safi sana. Natamani angeisoma hii
   
 5. Spetsnaz

  Spetsnaz Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mlitika,

  You are absolutely right. Kama majimboni wanamtumia hadi ex-president kukampenia watoto wadogo, sasa ikifika 2015 kwenye kampeni za urais si CCM watamleta OBAMA na viongozi wote wa G7??
   
 6. SIMBA WA TARANGA

  SIMBA WA TARANGA JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 992
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kajivunjia heshima na kujifunza mitusi- cdm wajinga, vifaranga
   
 7. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nafikiri atakua amejifunza kwamba:
  1. Siasa haibakwi
  2. Mfiwa hafutwi machozi kwa kupewa ubunge
  3. Kustaafu uraisi na kuendelea kuishi kwa gharamba za walipa kodi hatakiwi tena kurudi kwenye siasa za majukwaani
   
 8. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Ukweli ni kwamba hawajifunzi kutokana na matukio kama hayo, hususani BWM. Imagine energy iliyotumika na CCM (Ikishirikiana na Serikali yake) kutafuta jimbo kama ingetumika kutatua tatizo moja tu hapo (Say Ardhi) Arumeru Mashariki tungekuwa mbali sana kimaendeleo.
   
 9. n

  nketi JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nasikia ccm wamempa hiyo km adhabu kwa kutumbukiza nchi kwenye lindi la mikashfa ya ufisadi. Aliambiwa asipopanda majukwaani watamshitaki kwa ufisadi wake wa kujiuzia kiwira.
   
 10. Sema Chilo

  Sema Chilo JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 324
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkapa alilazimishwa tu kwenda Arumeru ndio maana hata siku ya uzinduzi ilibadilishwa. Hatahivyo viongozi wa CCM huwa hawana desturi ya kujifunza kutokana na matukio wapowapo tu
   
 11. M

  Mchokozi JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mzee Mkapa anatakiwa kusoma alama za nyakati, alitakiwa apumzike maana heshima aliyonayo na madhambi aliyofanya wakati akiwa madarakani RADAR, EPA, UBINAFISISHAJI nk vitaibuliwa upyaaaaaa, pumzika mzee BEN kama walivyowapumzisheni kwenye NEC
   
 12. Mlitika

  Mlitika JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 458
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ecxactly! Anapashwa atambue kuwa kuitwa akatoe msaada majukwaani ni kejeli kwake hasa baada ya kuambiwa kwenye NEC hawataki kumwona. Kwama kweli wanautahamini msaada wa busara zake basi sehemu ya maana ilikuwa kwenye NEC.
   
 13. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Well said Mlitika. Napigia mstari ushauri wako kwa bwna Ben. Nyongeza kidogo ni hii:

  1. BWM anatakiwa kujua kuwa "wenye CCM" wa wakati huu ni maadui zake nambari one na wala siyo kisiri siri bali wazi wazi. Wameanzisha na kuratibu kwa makusudi propaganda nyingi dhidi yake za kumchafua na kufunika yote aliyoifanyia nchi hii wakati wake (pamoja na mapungufu ambayo hayawezi kukosekana). Anapofumba macho na kuvimba kichwa wanapokuja kumwomba akasaidie wapate ulaji anawapa nafasi wajione wajanja sana na wazidi kumkebehi. Mbona alikataa wazi wazi kuzunguka kumnadi JK 2005? Ujasiri huo anaukosaje sasa?
  2. Kwa upande wa pili fundisho linawageukia wataka madaraka wanaotapatapa (CCM). Ingawa walimchafua kwa makusudi bado waliamini watu wengi nje na ndani ya nchi wanamheshimu sana BWM na ndiyo maana wanarudi kumwangukia awape tafu wakimhakikishia kuwa "Watanzania wanakuheshimu sana na wanakuskiliza mzee". Sasa wajue kuwa huo si mtaji tena; watanzania washafunguka akili na machi na HAWADANGANYIKI hata umlete Obama au nani.
   
Loading...