Mkapa, Mwinyi ‘waguswa’ na mabilioni ya Uswisi

Mkapa, Mwinyi ‘waguswa’ na mabilioni ya Uswisi

Bwana Mapesa

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
2,551
Reaction score
1,777
VITHLANI.jpg

UTARATIBU wa Watanzania kwenda kuhifadhi fedha katika mabenki ya Uswisi ulikithiri wakati wa utawala wa marais Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, imefahamika. Picha za grafu na zilizotolewa na mtandao wa Umoja wa Waandishi wa Habari za Uchunguzi Duniani (CIJ) na ambazo Raia Mwema imefanikiwa kuziona zinaonyesha kwamba wateja wengi kutoka Tanzania walipeleka fedha zao Uswisi katika kipindi cha kati ya mwaka 1988 na 2007. Mwinyi alianza kuwa Rais wa Tanzania mwaka 1985 na kumaliza muda wake mwaka 1995 na Mkapa alianza mwaka huo na kumaliza awamu yake mwaka 2005. Mtandao huo, kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya duniani, vimeibua taarifa hizo kutoka katika benki maarufu ya HSBC iliyoko Uswisi na habari hizi ni sehemu ya kampeni kali ya kupambana na ufisadi. Mtandao huo tayari umeibuka na taarifa kwamba Watanzania 99 wamehifadhi kiasi cha dola za Marekani milioni 114 katika benki hiyo, huku wakiwa na jumla ya akaunti 286. Hadi kufikia juzi usiku, ni Mtanzania mmoja tu, Sailesh Vithlani, ndiye ambaye anajulikana kuwemo katika orodha hiyo ya watu 99. Lakini Raia Mwema limeahidiwa na vyanzo vyake kwamba litapatiwa majina ya Watanzania wengine 98 waliobaki. Taarifa hizo za uchunguzi ambazo zimepachikwa jina la "SwissLeaks" zinaonyesha kwamba katika kipindi cha kati ya mwaka 1982 ambapo ndipo taarifa hizi zimeanza kuvujishwa hadi mwaka 2006, wateja 91 kati ya 99 waliokuwa na akaunti Uswisi ndiyo walifungua kiasi hicho. Kwa maana hiyo, wateja wengine wanane walifungua akaunti zao katika kipindi cha kati ya mwaka 2006 na 2007. Mwezi Juni mwaka 2012, Benki Kuu ya Uswisi ilitoa taarifa iliyoeleza kwamba Watanzania wanahifadhi kiasi cha dola milioni 197 (zaidi ya Sh bilioni 313) katika akaunti mbalimbali nchini humo. Kwa taarifa za sasa za SwissLeaks, ina maana kwamba ukiondoa dola hizi zilizopo HSBC, kuna takribani dola nyingine milioni 83 katika benki nyingine tofauti nchini Uswisi. Hii ni kama walioziweka hawajaziongeza au kuziondoa kwenye akaunti zao tangu Junui 2012. Hata hivyo, mwaka juzi, gazeti hili lilibaini kwamba pamoja na ukweli kwamba Uswisi ndiko kunakosifiwa, Watanzania wamehifadhi fedha nyingi zaidi katika Visiwa vya Jersey vilivyo chini ya Himaya ya Waingereza kuliko za Uswisi. Gazeti liliwahi kuripoti kwamba fedha za Watanzania pekee zilizoko katika visiwa hivyo zinakadiriwa kufikia kiasi cha pauni za Uingereza milioni 413 (sawa na shilingi za Tanzania trilioni 1.06). Fedha hizo zinatosha kuhudumia bajeti za wizara za Afya, Mifugo na Uvuvi, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Wizara ya Afrika Mashariki kwa mwaka mzima bila ya kuomba fedha kutoka kwa wafadhili na bado ‘chenji' ikabaki. Gazeti hili haliwezi kutaja chanzo cha habari hizi kwa vile taarifa hii ilipatikana katika mkutano uliofanyika Uingereza wiki iliyopita chini ya kanuni za Chatham (Chatham Rules) ambazo zinakataza kutaja vyanzo vya habari zilizopatikana kutoka katika mikutano inayotawaliwa na kanuni hizo. Kwa mujibu wa taarifa za uhakika zilizopatikana, Raia Mwema limeelezwa kwamba zaidi ya Jersey, kuna fedha nyingine nyingi katika visiwa vingine kama Cayman na Isle of Man ingawa pia kuna fedha zilizohifadhiwa jijini London, mji mkuu wa Uingereza. "Kuna watu binafsi ambao wamehifadhi fedha zao. Kuna fedha za kampuni kadhaa na kuna fedha za inayoitwa mifuko ya hisani. Naweza nikashindwa kuwapa majina haswa ya wenye fedha hizo lakini nadhani inawezekana kuwapa majina ya kampuni na mifuko hiyo ya hisani (trusts), kilieleza chanzo hicho. Kisiwa hicho ni miongoni mwa nchi zinazopendwa na watu, kampuni au taasisi zinazokwepa kulipa kodi au zinazopata mapato yake kwa njia ya kifisadi kwa vile zinatoza kodi kidogo na zina sheria zinazolinda usiri wa walioweka mali zao. Mkutano huo ulielezwa kwamba visiwa hivyo vilivyo chini ya Uingereza lakini vinavyojitawala vyenyewe vimehifadhi kiasi cha pauni bilioni 40 kutoka Afrika na katika hizo, pauni milioni 413 zinatoka Tanzania. Visiwa vya Jersey vilijipatia umaarufu mkubwa nchini Tanzania miaka michache iliyopita baada ya kubainika kwamba aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Andrew Chenge, alikuwa na akaunti katika visiwa hivyo ambayo ndiyo iliyotumika kumwekea fedha (dola milioni moja) zinazodaiwa kutokana na mauzo ya rada ya kampuni ya BAE Systems kwa serikali ya Tanzania.






Tufuatilie mtandaoni:


- See more at: Raia Mwema - Mkapa, Mwinyi ‘waguswa’ na mabilioni ya Uswisi
 
Mwinyi anashanga nini na hussein mwinyi mwanae naye ni mmoja wao.
 
Mi najiuliza kila siku hivi kweli viongozi wetu wana dhamira ya kweli ya kututoa hapa tulipo?
Je hawa viongozi wetu wana uzalendo wa kweli kwa nchi yetu?
Mbaya zaidi kwenye katiba pendekezwa licha ya mzee Warioba kuweka mambo mazuri kabisa juu ya makatazo ya watu kutokuwa na account nje ya nchi bado timu ile ile ya wapigaji ikayatupilia mbali mapendekezo hayo na kukubaliana kwa eti kwa masharti fulani fulani bado mtu binafsi anaweza kuruhusiwa kuwa na account nje ya nchi!!! shame on you guys!!!!
Katika hali uchanga wa mataifa yetu haya ambapo uzalendo wa kweli bado ni issue watu hawaoni haya hata kidogo kukwapua mapesa ya walala hoi na kuyapeleka nje yaani kweli lazima tujitafakari upya HAIWEKZEKANI HATA KIDOGO !

Ewe Mwenyezi Mungu Mfalme wa Mbingu na nchi twakuomba baba tuondolee dhulma hii miongoni mwa watu hawa wachache wenye roho za ubinafsi mioyoni mwao
Na nyie viongozi wetu hebu kuweni na hofu ya Mungu mioyoni mwenu ili mukaitende haki kama Baba yenu wa Mbinguni alivyowaamuru
 
Ndiyo .maana wameipiga nchini Rasimu ya Katiba ya wananchi maana ilitamka waziwazi ni marufuku kwa kiongozi kuwa na akaunti nje ya nchi.

Vv
 
Nini kifanyike ili kuzipata fedha zetu? Tuache blah blah za kina Werema hapa.
Bunge liitake serikali kuleta mswada wa sheria ya kuwazuia watu kuhamisha fedha nje ya nchi.
Mwanasheria mkuu wa serikali alitolee maelezo na hatua atakazochukua kutaifisha na kuwashtaki wenye fedha nje ya nchi. Vinginevyo ccm must go to hell this year ili tutengeneze mazingira ya kuwakamata wezi wote.
 
HSBC ni benki ya wajanja ambayo hata UK imesaidia sana matajiri kukwepa kodi, sidhani kama hizo hela zitarudi, binadamu na tamaa akiona kuwa anawalimbikizia watoto wake kama akifa lakini pesa chafu huwa zinaisha kwa uchafu tu na familia kugombana kwa tamaa.
Wakati Mwingi pia benki hufaidi pindi wanapokufa bila mrithi na kuzichukua, hizo hela ni chafu na zinatumika kukopesha tena wauza silaha ambao wanaleta kutumaliza tena.
 
BAE Systems and Tanzania: Investigating 1999s suspect radar deal
Consultancy Africa Intelligence - Your African partner in superior research and analysis, 17 Jan 2011

Sailesh Vithlani, head of the Tanzanian firm Merlin International, served as BAE's "covert" agent to secure the Tanzanian Government's approval for the Commander radar system.(4) BAE put the money in a Swiss account for Vithlani and concealed the transaction, giving BAE plausible deniability as they turned a blind eye to the likelihood that this money would be used to bribe Tanzanian Government officials.

The corruption was evident in this deal, not only due to the money provided to Vithlani in the Swiss bank account, but also because this is one of the poorest states in Africa (poor enough that they had to lend the entire amount for the purchase of the radar from a UK bank, Barclays) and they were purchasing a radar defence system for a country with no air force.

It remains to be seen what justice can be found in Tanzania regarding the prosecution of Sailesh Vithlani and investigating the possibility of Government officials being involved.

While BAE has admitted to ...
Trinidad and Tobago's Newsday : newsday.co.tt : Daily News from Trinidad and Tobago, 23 Dec 2010 [cached]

While BAE has admitted to paying the money to its agent Sailesh Vithlani, for his part in securing the 28 million pound contract, the company denied any corruption in the transaction.

BAE also admitted that most of the money paid to Vithlani was funneled through a secretive company it set up in the British Virgin Islands.

BAE has admitted paying the...

BBC - Homepage, 20 Dec 2010 [cached]
BAE has admitted paying the money to its agent, Sailesh Vithlani, for his part in securing the £28m contract.
However, BAE denies any corruption.
BAE also conceded that most of the money paid to Mr. Vithlani was funneled through a secretive company it set up in the British Virgin Islands.
...
It has already agreed a deal with the Serious Fraud Office, under which it offered to make an ex-gratia payment of up to £30m to Tanzania, and admitted failing to keep accurate records of the payments to Mr. Vithlani.

BAE's secret $12m payout in African deal | Special reports | Guardian Unlimited
Latest US news, world news, sports and opinion from the Guardian | theguardian.com | The Guardian [cached]

Yesterday's admissions by the Tanzanian middleman, Sailesh Vithlani, led Ms Short to call for BAE's prosecution if the allegations were proved.
...
In Dar es Salaam, Mr. Vithlani's business partner, Tanil Somaiya, told the Guardian that British police had already flown out to trace and interview both men as potential witnesses.
...
That money was under the personal control of Mr Vithlani, Mr Somaiya said, and this had been admitted to UK police.
...
When asked about the BAE money, Mr Vithlani told theGuardian he had made no disbursements from the Swiss cash to public officials "in Tanzania".Asked if he had disbursed any of the $12m to third parties outside of Tanzania, he declined to comment."When the UK police travelled to Tanzania, we met them at their request and answered all their questions," he said.

Mr Vithlani acted as agent not only on the radar deal but also in the 2002 purchase from the US of a top-of-the-range Gulfstream official jet for the then Tanzanian president, Benjamin Mkapa, at a cost of more than $40m.
...
Police sources in Tanzania said the agreement to use Mr Vithlani as an agent had been signed off by the then chairman of BAE, Sir Dick Evans.
...
BAE Systems were yesterday asked why they had made a 30% payment to Mr Vithlani's Swiss account.

BAe Innocent of Bribe Allegations - The Money Bag
Roulette – Informationen und Bewertungen | TheMoneyBag, 27 Jan 2007 [cached]

[The] admissions by the Tanzanian middleman, Sailesh Vithlani, led Ms Short to call for BAE's prosecution if the allegations were proved.
...
Police sources in Tanzania said the agreement to use Mr Vithlani as an agent had been signed off by the then chairman of BAE, Sir Dick Evans.
...
BAE Systems were yesterday asked why they had made a 30% payment to Mr Vithlani's Swiss account.
 
Tuleteeni orodha ya hao wanamiliki hayo mapesa nje ya nje
 
Back
Top Bottom