BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,283
Mkapa azimwa
na Josephat Isango
Tanzania Daima
RAIS mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, amezimwa kuzungumza na waandishi wa habari waliofurika nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam.
Waandishi hao walifika nyumbani kwa rais huyo kuitikia mwaliko wa Idara ya Habari (Maelezo) wa juzi, uliowataka kufika nyumbani kwake kuanzia saa sita mchana kwa ajili ya mkutano huo uliopangwa kufanyika jana saa saba mchana.
Ilielezwa kuwa Mkapa aliitisha mkutano huo kwa ajili ya kuzungumzia maadhimisho ya jubilee yake ya miaka 75, inayotarajiwa kufanyika Novemba 12, lakini bila shaka angezungumzia mambo mbalimbali yanayolizunguka taifa kwa sasa.
Hata hivyo wakati maandalizi yakiwa yameshakamilika kwa maana ya wanahabari kufunga vifaa vyao vya kazi, Mkapa aliahirisha mkutano huo kwa madai kuwa alikuwa na dharura.
Taarifa ya Mkapa kuahirisha mkutano huo ilitolewa na Idara ya Habari (Maelezo) hapo hapo nyumbani kwa Mkapa, hivyo wanahabari waliokuwa na shauku ya kutaka kumsikiliza, hawakupata hata fursa ya kumwona kwa macho.
Rais Mkapa amefurahishwa na ujio wenu kwa wingi, alikuwa anataka kuongea nanyi kuhusu kuadhimisha jubilei yake ya miaka 75 ya kuzaliwa inayotarajiwa kufanyika Novemba 12, mwaka huu katika Kanisa la Mtakatifu Petro, Upanga jijini Dar es Salaam. Anawaomba sana radhi kwa usumbufu, kwani hataweza kuongea na waandishi wa habari kutokana na dharura aliyoipata, alisema mtoa taarifa huyo bila kufafanua ni dharura ipi.
Tangazo la kuahirisha mkutano huo, liliwaacha waandishi wa habari wakipigwa na butwaa, kwani wakiwa hapo nyumbani kwa Mkapa waliona meza imeandaliwa na kiti ambacho kingetumiwa na rais huyo mstaafu kuongea na waandishi, ambacho muda wote kilikuwa kinalindwa.
Ingawa taarifa iliyotolewa ilisema kwamba mkutano huo umeahirishwa kutokana na dharura, uchunguzi wetu umebaini kuwa rais huyo mstaafu alizuiliwa kufanya mkutano huo kutokana na mambo mazito aliyotaka kuyasema.
Wadadisi wa mambo ya siasa wanadai kuwa huenda kiongozi huyo wa zamani wa nchi amezuiliwa kufanya mkutano huo na baadhi ya viongozi wa juu wa chama chake cha CCM, hasa kuhusiana na mnyukano wa kiti cha urais mwaka 2015 ndani ya chama hicho.
Baadhi ya mambo ambayo rais huyo angeulizwa na kuyatolea majibu ni pamoja na mnyukano wa urais, rasimu ya Katiba mpya, masuala ya ujangili na utoroshwaji wa rasilimali za nchi, dawa za kulevya, rushwa, nk.
Jingine ambalo Mkapa angelizungumzia ni suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwani ni mmoja wa waasisi wa Jumuiya hiyo ambayo katika siku za hivi karibuni uhusiano wa nchi wanachama umekuwa ukizorota.
Hii ni mara ya kwanza kwa Mkapa kuita waandishi wa habari nyumbani kwake kuzungumzia sherehe zake za kuzaliwa au jambo jingine lolote lile tangu atoke madarakani.
Rais mstaafu Mkapa alizaliwa Novemba 12, mwaka 1938, Ndanda, Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara.