Mkapa anashitakika - Dk. Slaa

duh hivi kuna watu wanaamini kwamba kelele za dr. slaa ndizo zilizowapeleka kina mramba kisutu??

Kwa nini usijiulize kama hayo majina yalikuwemo kwenye ile orodha ya mafisadi iliyoanikwa Mwembe Yanga na Dr. Slaa!! Ukishapata jibu ujiulize tena wenye mamlaka walisema nini kuhusu orodha hiyo tukianzia Serikalini hadi Chamani ( chama cha mafisadi wenyewe). Ukishapata jibu jiulize tena mafisadi wenyewe walisema nini baada ya majina yao kuanikwa hadharani.
 

Thanks Amani. Ni kweli kuwa statement hii ni pana na inaweza kuandikiwa kitabu. Ila nadhani inaeleweka pamoja na ufupi wake. Labda niiifungulie thread yake pekee ili kuielezea zaidi.

Shukrani Mkuu
 
In this post, I am going to be a little incoherent, naombeni mnisamehe!

Mkuu Plotinus, huna haja ya kutanguliza samahani. Mawazo yako ni ya haki kabisa. Ninavyoijua JF, hapa ndipo mahali pake kabisa.

Unajua kuna watu wanaboa sana, wanakaa kwenye computer zao halafu kazi ni kutoa ushauri na saa nyingine kubwatuka tu -

Kama ulivyoomba usamehewe, nawe usamehe wote wenye mawazo tofauti na wewe. Matumizi ya computer zao wenyewe nayo ni haki yao binafsi. Sioni kwa jinsi gani suala hilo linavyokukera. Unachoweza kufanya ni kuwaelewesha unachokiamini, wakikubaliana na wewe mtakuwa pamoja. Hoja kujengwa kwa hoja. Mkuu, ukumbi huu ni wa kuelimishana, na wengi hapa hawajali mtu anaeamua kuboreka kwa kauli zao.


Mkuu mimi sio Dr. Slaa. Yeye ameamua kuishi maisha ya kisiasa, mimi sijaamua kufanya hivyo. Yeye ni Mbunge, mimi sio Mbunge. Yeye ameweza kupata ushahidi kuhusu mafisadi, mimi sijaweza kuupata. Yeye anajua anachokitaka katika ulingo wa siasa, mimi ninajua ninachokitaka katika ulingo ninaoutumikia. Kupambana na ufisadi ni jukumu la kila mtu. Jinsi ya kupambana nao inatofautiana na matokeo tunayoyataka. Yeye amekerwa sana na mambo aliyofanya Mkapa (kwa sababu zake), mimi sijakerwa kiasi hicho. Yeye anaumia koo akilia majukwaani, mimi sipandi jukwaani na koo haliniumi. Ndio maana namshauri, badala ya kuendelea kuumiza koo lake bila matokeo yoyote, ni vyema akatumia nguvu hizo kufanya yanayoweza kumpa matokeo ya haraka na ambayo anayategemea. Mimi sitaki kumshitaki Mkapa, yeye anataka Mkapa ashitakiwe (sioni tija yake). Ni dhahiri kuwa matarajio yake katika maisha sio sawa na yangu.


Mkuu Plotinus, Tanzania haitakomboleka kwa kum-support au kutom-support mtu mmoja, au kundi fulani la watu tu. Tanzania itakomboleka kwa kutenda yanayotendeka kwa minajili ya kuiokomboa nchi yetu. Kila mtu anaowajibu wake katika ukombozi wa nchi yetu. Masuala ya ukombozi si ya kisiasa tu. Ukombozi ni wa-kiuchumi, kiulinzi na usalama, kijamii n.k.

Ndugu yangu, kubwatuka ni kazi ya mdomo. Kama inakukera pole sana. Maana hata wewe umebwatuka sana katika quote hiyo hapo juu. Ila hilo halikeri, kwakuwa kuna kubwatuka kunakokera zaidi (TUMIA HOJA, HAKUNA ANAELALAMIKA). Kuinufaisha familia yangu ni wajibu wangu binafsi. Maana nimeapa kufanya hivyo. Kimsingi nadhani unataka watu wote wamuunge mkono Dr. Slaa na CHADEMA yake. Hilo linajadilika. Ila halijadiliki kwa kulazimisha. Hakuna mtoto mdogo. Kila mtu ana matarajio yake na mapenzi yake katika itikadi anazoziamini. Ushindi wa kisiasa haufanywi hivyo. Ndio maana MAfisadi hao hao wanawashinda kila siku.

Mtikila amefungua ma-kesi mengi tu dhidi ya serikali, mlikuwa wapi, mbona hamkisaidia?!

Mtikila angeomba msaada angeweza kusaidiwa na wale wanaoona kesi za ni za msingi. Usipoomba hutapewa.

Hebu tuwe fair na tuwe tunafanya tathmini kama watu wenye hekima! Huo uwezo tu wakusoma katiba na kuzunguka nchi nzima-ku-counter statement za viongozi wa serikali mnadhani ni kitu kidogo...mnataka afanye zaidi!

Kuzunguka nchi nzima ni mapenzi yake na ni kazi yake. Mtu yeyote anaetaka kueneza itikadi yake kwa watu ni lazima afanye hivyo. Sasa unataka nilazimike kuunga jitihada za kila mtu kuzunguka nchi nzima kwasababu tu amefanya hivyo? C'mon do not be naive. Kama amechagua kuwa mwanasiasa ni lazima afanye siasa. sio lazima wote tuache kila kitu tuandamane nae. Yeye anajua faida ya kuwa mwanasiasa.


Nadhani hueleweki ama hujui unachokisema. Mtu akiingia madarakani kwa kuchaguliwa, anakuwa amefanya jitihada kubwa kuchagulika. Hutumia njia mbalimbali kushawishi watu wamchague. Asipotekeleza mahitaji ya waliomchagua, basi ni dhahiri kuwa watamchagua mwingine mwenye kufaa zaidi. Hakuna favour kwenye siasa. Hakuna kiongozi ambae yuko madarakani eti kwasababu asipokuwepo pale wananchi watateseka. Aache basi aone kama wengine hawatafanya.


Katika thread hii, hakuna aliekosoa content ya Dr. Slaa kutaka Mkapa ashitakiwe. Ila umetolewa ushauri wa Dr. Slaa kufanya hivyo haraka kama anaweza. Kama hawezi kushitaki, anategemea wengine wafungue mashitaka hata kama hawataki kufanya hivyo? Wewe wa wapi?

Watanzania - Do something-toka kwenye comfort zone yako---acha ku-expect wengine tu ndio wafanye!

Kila mtu atimize wajibu wake. Nchi inahitaji kwenda mbele. Tuache porojo.
 

NAUNGA MKONO HOJA HII; ingawa kidogo ulikuwa mkali nimeelewa ni hasira watu wanakera; tena mie nauita WATZ kama hawa ni wagonjwa wakubwa wa taifa; kusubiri Dr Slaa akufanyie wewe ukiwa hoi; do something; join him if u feel he is right or do yours the other way; hakuna chochote mineno mitupu; Dr Slaa ni shujaa wa miaka karibu mitatu sasa; hayupo kama yeye TZ hii mwenye ujasiri; hana simile; viongozi wanaanza kumuogopa sasa ( umeona hata Masha recently). Unataka afanye nini kweli; jamani naungana mkonona mtoa hoja hii hapo juu
 

Sasa Mwiba, ndiyo maana kuna haja ya kuwaunga mkono kina Slaa katika mapambano haya. Sisi Raia pia tunalo jukumu la kufanya katika kuonyesha kuwa serikali haitutimizii matakwa yetu. Nani ambaye ana wajibu wa kuibana serikali kama siyo mpiga kura? Maisha bora hakuahidiwa Slaa na wapiganaji wenzake, bali kwa kila Mtanzania kwa sababu rasilimali ambazo zimepangwa kutumika katika kuhakikisha maisha bora yanapatikana ni zo umma wa watanzania wote. Tujenge ujasiri wa kuwasimamisha viongozi wanapozurura mikoani na Mashangingi na kuwahoji hayo maisha bora yako wapi? wakitupa majibu ya rejareja, tujenge tabia ya kutumia kura zetu kuwawajibisha.
 
Hapa naona wachangiaji kuna jambo wanashindwa kulielewa kwa kina , ngoja nitoe ufafanuzi kidogo kwa jinsi ninavyoelewa ishu za Mkapa.

Itakumbukwa kuwa Mkapa alilazimisha kubinafsishwa kwa iliyokuwa benki ya taifa ya Biashara NBC LTD, Na mara baada ya Benki hiyo kuvunjwa na kuzaa NMB basi kipande kilichobakia kikauzwa kwa ABSA ya Afrika ya Kusini.

Baada ya dili hilo Mkapa aloilipwa na ABSA shilingi milioni mia tano (500,000,000) jiulize zilikuwa za kazi gani? Rais wa Nchi alipewa zawadi ama ilikuwa ni deni alikuwa anawadai hao jamaa?

Pili, kuhusu kuuzwa kwa Kiwira kwa asilimia 85, ambalo ni shirika aliloliunda mwalimu Nyerere kwa ajili ya watanzania ila yeye Mkapa , Mkewe Anna , mwanaye Nicolaus, Mkwewe Mbuna na aliyekuwa waziri wa Nishati na madini Daniel Yona walijiuzia Kiwira kwa bei ya kutupwa na hata hivyo hawajalipa mpaka leo deni lao .

Kibaya zaidi ni kuwa waliingia mkataba na TANESCO ambao ni mkataba usiokuwa na kikomo yaani hauna mwisho kuwa utaisha lini na kila siku itokayo kwa Mungu wanalipwa kiasi cha shilingi milioni mia tatu (300,000,000) kama Capacity charge hii ni kuwa wawe wamezalisha ama hawajazalisha umeme wanatakiwa kulipwa na TANESCO.

Na mkataba huo unaonyesha kuwa watakapoanza kuzalisha umeme wao utatakiwa kulipiwa service charge yaani gharama za huduma hiyo huu ni wizi .

Sasa nawashangaa wanaosema eti asishitakiwe wakati yeye mkataba wake ni mbaya kuliko ule wa RICHMOND ambao tulikuwa tunapoteza kiasi cha shilingi milioni 152 kwa siku huu ni mara mbili yake.

Anapaswa kushitakiwa kama wakina Mramba na wenzake ,ili kuwa fundisho kwa wengine laa sivyo nchi inateketea, watanzania tunakosa umeme kwa sababu TANESCO hawawezi kusambaza nyaya kutokana na kukosa fedha ambazo wanawalipa jamaa hawa kila kukicha.
 
Baada ya dili hilo Mkapa aloilipwa na ABSA shilingi milioni mia tano (500,000,000) jiulize zilikuwa za kazi gani? Rais wa Nchi alipewa zawadi ama ilikuwa ni deni alikuwa anawadai hao jamaa?

Kaka hapa ndo napapata kwa mara ya kwanza..... Mungu wangu nimjuae mimi
 
The kitu kibaya ni kuwa TANPOWER RESOURCES LTD inamilikiwa na watu wafuatao,

1.Daniel Yona - alikuwa waziri wa Nishati na madini 2004 wakati wanaichukua kiwira.
2. Advocate Mbuna - huyu ni mkwe wa Mkapa kwani mwanaye Mkapa kamuoa binti wa Mbuna.
3. Anna Mkapa - alikuwa nasema alikuwa kwani sina ushahidi kama bado ni mke wa Rais mstaafu Mkapa, alipitia ANBEM.
4. Nicholaus Mkapa - huyu ni mwanaye Mkapa sijui anajishughulisha na shughuli gani kwa sasa na hata wakati huo alikuwa nani.
5. Mapundi - huyu hajaulikani ni nani na anafanya nini ama alikuwa akifanya nini.
6.Benjamini Mkapa - alikuwa Rais 2004 wakati mkataba unaingiwa na alipitia kampuni la ANBEM.

Familia imeamua kuchukua rasilimali za Taifa bila huruma na kuna watu wanasema eti asishitakiwe kwa lipi?

Ajitokeze na aombe radhi na arudishe mali zetu hapo anaweza kusamehewa ila sio kumuacha aendelee kulinyonga Taifa hili.
 
Dr.tumekuelewa lakini si wote tuna mheshimu rais aliyeko madarakani.mbona DR. anampinga rais ambaye alisha sema mwacheni mzee wa watu apumzike.
 
Alafu leo anasisima jukwaani tunamuangalia tu! Alitakiwa aendelee kukaa kimya kama alivyosusa kuwaomba radhi Watanzania!
 
ashitakiwe huu ndio utawala wa sheria.kwani imeelekeza watu wa kushitakiwa walio tenda makosa?wengine mnasema aombe radhi mbana watu wengine au akina mramba hawakuambiwa waombe radhi?
 
Kwa madudu haya alafu huyu mtu anakuja kusimama jukwaani kufanya siasa alafu tunamkenulia meno! Ajibu tuhuma zake!
 
Kazi kwenu wana Arumeru,msikubali kutumika na watu kama hawa!
 
Dr slaa is just a leader...people need to take action when they are ready!
 

tuache majungu,Mkapa anastahili heshima yake kwa mchango wake...kuna MWINYI na NYERERE,je hawakufanya makosa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…