Mkapa amuangukia Kikwete

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Akutana na vigogo kuomba msaada

Tuhuma mpya zazidi kumuandama


Na Saed Kubenea

MwanaHALISI~Maslahi ya Taifa Mbele

RAIS mstaafu Benjamin Mkapa amelalamika kuwa anasakamwa na wanasiasa na anachafuliwa, MwanaHALISI limeambiwa.

Kwa miaka miwili mfululizo sasa, Mkapa amekuwa akitajwa na kuhusishwa na baadhi ya tuhuma za ufisadi na utovu wa “utawala bora” wakati wa kipindi chote cha utawala wake – 1995 hadi 2005.

Kufuatia malalamiko hayo, wachunguzi wa siasa za Tanzania wanasema inawezekana ukaidi wa Mkapa umeyeyuka na sasa yeye ameona kuwa “ni maji shingoni.”

Taarifa zinasema Mkapa alitoa malalamiko yake kwa mwanasiasa mmoja nchini (jina tunalo) nyumbani kwake, Sea View, Dar es Salaam hivi karibuni.

Alimkomalia mwanasiasa huyo kuwa na yeye anashiriki kumchafua huku akionyesha kuwa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya “kuwaacha viongozi wastaafu kupumzika” kuwa imeshindikana kutekelezwa.

Rais Kikwete aliwaambia waandishi wa habari mwaka 2007, alipoulizwa iwapo atachukua hatua dhidi ya Mkapa kufuatia tuhuma alizokuwa akibebeshwa, kuwa viongozi waliostaafu waachwe wapumzike.

Kilio cha Mkapa kimekuja kufuatia mlolongo wa tuhuma za kale na sasa kurudiwa mara kwa mara na kumnyima, yeye na familia yake, kuishi kwa raha hata katika jiji la Dar es Salaam ambako aliwahi kukutana na vijana mitaani wakiimba “Fisadi! Fisadi! Fisadi!”

Chanzo cha taarifa kinasema, hata hivyo, mwanasiasa huyo hakumsaidia Mkapa, kwani alikana kumkashifu na kusema angekuwa anataka kumkashifu, angefanya hivyo kwa vile alikuwa na ushahidi wa mambo yake mengi.

Huyo ni mwanasiasa wa pili katika kipindi cha miezi miwili kukutana na Mkapa. Mwingine ambaye ni waziri mwandamizi anadaiwa kumwambia Mkapa kuwa hakuna anayemwandama bali “mambo ni mazito.”

Taarifa zinasema waziri huyo alimweleza kuwa ahadi ya rais Kikwete ipo palepale lakini kwa hapo alipofika, ingekuwa vema naye (Mkapa) akajitahidi kujenga upya sura yake kwa “kurejesha baadhi ya mali unazodaiwa kumiliki kutoka serikalini.”

“Ni kweli nimekutana na Mkapa. Tumezungumza mengi. Nimemwambia tutakulinda, lakini na wewe jaribu kujisafisha kwa kurudisha mali serikalini, hasa ule mgodi wa Kiwira,” chanzo cha habari kimemnukuu waziri wa Kikwete akisema.

Mkapa anahusishwa na umiliki wa mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira mkoani Mbeya kupitia kampuni yake ya ANBEN anayomiliki na mkewe, Anna ikiwa miongoni mwa makampuni matano yaliyoingia ubia na kampuni ya TanPower Resources Company Limited.

Kupatikana kwa taarifa kuhusu waziri kubadilishana mawazo na Mkapa kunathibitisha kuwepo ufuatiliaji wa karibu wa Rais Kikwete kuhusu tuhuma zinazomkabili Mkapa.

Wakati Mkapa anatajwa kukutana na waziri na mwanasiasa machachari akitaka hatua zichukuliwe kumlinda, tuhuma mpya zimeibuka dhidi yake.

Mkapa, kupitia TanPower Resources Limited, anahusishwa na dhamana ya serikali ya kupata mkopo wa Sh. 17.7 bilioni kutoka CRDB Bank kwa ajili ya kuendeleza mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira.

Kwanza, inadaiwa kuwa Mkapa alimiliki kampuni akiwa bado rais (ANBEN 1998) wa nchi na hivyo atakuwa alitumia nafasi yake kujinufaisha binafsi na kampuni yake.

Pili, kwa kuwa alikuwa bado madarakani na kwa kuwa uamuzi wa kuuza Kiwira ulifanyika ndani ya Baraza la Mawaziri aliloliongoza, basi uamuzi huo ulikuwa wa upendeleo kwa kampuni yake.

Tatu, hata waziri aliyejenga hoja mbele ya baraza la mawaziri, Daniel Yona ametokea kuwa mshirika katika umilikaji wa mgodi huo, jambo ambalo haliendani na utawala bora.

Nne, mkataba wa kampuni ya Mkapa kuuza umeme kwa Tanesco ulifungwa Mkapa akiwa madarakani (Septemba 2005), jambo linaloonyesha upendeleo kwa kampuni yake na utovu wa utawala bora.

Kwa mujibu wa mkataba huo, kampuni ya Mkapa ingelipwa (dola 3.65 milioni – sawa na zaidi ya Sh. 4 bilioni kila mwezi.

Tano, Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini imegundua mwanzoni mwa mwaka huu, kuwa fedha za mkopo zilizodhaminiwa na serikali (Sh. 17.7 bilioni) hazikutumika kama ilivyokusudiwa.

Kutokana na kutotumia fedha palipohitajika, jenereta moja ya kuzalisha umeme imechakaa kiasi cha kutoweza kufanya kazi; na nyingine ina uwezo wa kuzalisha megawati moja tu ya umeme kutoka megawati sita wakati mgodi unabinafsishwa.

Nyaraka zinaonyesha kuwa TanPower Resources Limited kimkataba ilitakiwa kuzalisha megawati 200 za umeme kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ni kuzalisha megawati 50 kufikia Julai 2007 na megawati 150 ifikapo Machi, mwaka huu. Yote hii sasa ni ndoto.

Uchakavu wa miundombinu umeathiri pia uzalishaji wa mkaa wa mawe na mwekezaji “ameuza baadhi ya vifaa vya mitambo kama vyuma chakavu,” wameeleza wafanyakazi mgodini.

Sita, TanPower Resources Limited imeshindwa kulipa wafanyakazi wake 1,632 kwa karibu mwaka sasa licha ya kuonyesha kwenye mchanganuo wake kwamba ilitenga Sh. 3.0 bilioni kwa ajili hiyo.

Katika mazingira haya, serikali ambayo bado ina hisa katika mgodi huo (asilimia 15) italazimika kuwalipa wafanyakazi kwa mtindo wa Tanzania Railways Limited (TRL) ambako serikali imekuwa ikikingia kifua wawekezaji.

Mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira ulioanzishwa kwa msaada wa serikali ya China, Novemba 1988, ulitarajiwa kuzalisha tani 150,000 za mkaa ghafi kwa mwaka na kwamba uzalishaji ungekua hadi kufikia tani milioni moja kwa mwaka.

Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, tayari imependekeza mgodi wa Kiwira urejeshwe serikalini, jambo ambalo waziri aliyekutana na Mkapa anapendekeza.

Tathmini ya mgodi mwaka 1988 wakati ukibinafsishwa, na Mkapa akiwa madarakani, ilionyesha ulikuwa na thamani ya Sh. 4.2 bilioni. Lakini tathmini iliyofanywa na Taasisi ya Ardhi mwaka 1991 ilionyesha thamani ya Sh. 7 bilioni.

Kamati ya Bunge inasema imeshindwa kuelewa vigezo vilivyotumika kutupilia mbali tathmini iliyofanywa miaka mitano baadaye na serikali kuamua kuuza hisa zake kwenye mgodi huo kwa gharama ya Sh. 700 milioni tu.

Hata hivyo, kampuni ya Mkapa ililipa Sh. 70 milioni tu.

TanPower Resources Limited ina wanahisa watano – kila mmoja akiwa anamiliki hisa 200,000 ikiwamo ANBEM Limited inayomilikiwa na Mkapa na mkewe.

Makampuni mengine ni Devconsult International Limited ya S.L.P. 65440 Dar es Salaam inayomilikiwa na Daniel Yona na Dan Yona.

Mengine ni Universal Technologies Limited inayomilikiwa na Wilfred Malekia na Evans Mapundi; Choice Industries Limited inayomilikiwa na Joe Mbuna na Goodyear Francis; na Fosnik Enterprises Limited inayomilikiwa na Nick Mkapa, Foster Mkapa na B. Mahembe.

Makampuni matatu ya mwisho yanatumia anwani moja ya posta ambayo ni S.L.P 8764 Dar es Salaam.

Mkapa anakabiliwa pia na tuhuma za kuuza benki ya NBC kwa “bei poa,” na kupokea Sh. 500 milioni kutoka benki ya Afrika Kusini (ABSA) iliyonunua NBC ambazo hazikutolewa maelezo.

Vilevile Mkapa anatuhumiwa kuuza makampuni ya umma kwa kasi kana kwamba ameshikiwa bakora; kuuza nyumba za serikali kwa njia ya upendeleo na kwa bei ya bure na kuingilia zabuni ya Hotel 77 ya Arusha ambako serikali imelazimika kulipa fidia ya Sh. 3.3 bilioni na gharama nyingine.

Hivi karibuni, wakili wa mahakama kuu amekaririwa akidai kuwa Rostam Aziz, mbunge wa Igunga, alimwambia asaini hati za mikataba ya kampuni ya Kagoda Agriculture Limited ili wachote zaidi ya Sh. 40 bilioni kutoka Benki Kuu (BoT).

Alisema, na bado haijakanushwa, kwamba aliyetoa amri ya kuchukua fedha hizo kutoka BoT, mbele ya Katibu wa CCM wakati huo Philip Mangula na marehemu Daudi Ballali, ni Benjamin Mkapa.

Asasi mbalimbali za kiraia na wananchi wa kawaida wamekuwa wakitaka serikali kumchukulia hatua Mkapa.
 
Bubu,
Jinsi unavyomumuna kweli yaniacha hoi! Manake uzito wa Mh.Mkapa kumdondokea Mh. Kikwete....tehe heheheheh:rolleyes:

Mie nilifikiri ajali kazini:eek:

Wata-ji-sort kama kweli watafikia sehemu ya kuangukiana!!!!!
 
Diversion kama kawaida kila tukiwa in the middle of something hot, wajanja wanatupeleka kwingine, ili tusahau issue za DECI, Richmond, EPA na nyingine ila kwa sasa kumtumia Mkapa kama mbuzi wa kafara mlie tuu tuko makini sana.2010- around the corner mpaka mwalimu mtamfufua ili muungwana apete kiulaini
 
Ifike mahali huyu mzee kama ni Mwungwana akubali kwamba aliiba na akubali sheria ichukue mkondo wake. Ni vigumu kwa yeye kujitofautisha na tuhuma zote zinazoelekezwa kwenye uongozi wake, naona kila mtu alikuwa anabuni tu namna ya kuiba na kwenda kumwambia Rais mgawo wake katika hilo na jamaa anatoa go ahead. Hizo zilizoelekezwa hapo ni chache tu kati ya tuhuma, zipo nyingi zaidi, ikiwemo kiwanda cha Kilombero. Mpaka leo nashangaa alikuwa anataka fedha hizo zote kwa ajili ya nini, wakati ataishi kwa pensheni ya uraisi mpaka kufa? Nadhani huu ufisi peke yake wafaa kumpeleka kortini. Tumemlisha miaka kumi kwa kodi zetu, tunamlipa pensheni miaka yote, bado tena ametuibia?? Shame!!
 
Mkapa Mkapa hadi namuonea huruma sana sana.....kweli ameharibu nchi kabisa hata ukiwa na raisi anapokea 10%??ni aibu sana....
 
Mbona Mengi hakuwataja hawa au ni wenziwe wanahitaji kulindwa na kuachwa kupumzika ni bora wakapumzikie jela.
 
Diversion kama kawaida kila tukiwa in the middle of something hot, wajanja wanatupeleka kwingine, ili tusahau issue za DECI, Richmond, EPA na nyingine ila kwa sasa kumtumia Mkapa kama mbuzi wa kafara mlie tuu tuko makini sana.2010- around the corner mpaka mwalimu mtamfufua ili muungwana apete kiulaini
hapa ni kupotezana tuuuuu...

mkapa si lolote kwa sasa wanataka kutuzuga ili tusijue ukwelii...

tatizo ni CCM CCM CCM CCM CCM.....jamani hatuhitaji akili kutambua hiloooo..
 
baba yangu siku moja aliniambia hivi '' kuiongoza nchi hii kama rais ni rahisi sana maana wananchi wake wanarubuniwa kirahisi kupita kias na wepesi wa kusahau''
hata huyu akiondoka madarakani iwe 2010 au 2015 itagundulika kuwa ameiba sana wakati yuko ikulu.
HUKO NDIKO KUPOKEZANA VIJITI
 
Kwa kweli TAMAA ndani ya mwanadamu haina macho - hivi Bwana Benjamin William Mkapa mali/mapesa yote hayo atayapeleka wapi?? jumba kubwaaaaaaaa la gorofa Upanga, Jumba kubwaaaaaaaaaa la kifahari Lushoto (nyingine sijui) mali hadi mgodi wa mawe - watoto wenyewe nasikia wawili - anajitia dhambi bure na hapo kesho ahukumiwe na Mungu kisa mali/pesa ambazo hata kutumia hawezi - HIVI UNAWEZA KULA GUNIA LA MCHELE KISA UNA MCHELE MWINGI?? Utaishia kula sahani moja tu - HIVI UNAWEZA KULALA NYUMBA MBILI AU TATU USIKU MMOJA KISA UNAZO NYINGI - utalala moja tu na kitanda kimoja tu na chumba kimoja tu - INAFIKA KIPINDI KABLA MWANADAMU HUJAIBA NA KUJILIMBIKIZIA MALI KIBAO - ATAFAKARI NA KUFIKIRI - HATA UKIWAJENGEA WATOTO NYUMBA - WAKIWA WAKUBWA WATAONA NI OLD FASHIONED - watataka aina nyingine - LABDA ndogo KULIKO KUBWA etc. INGEPENDEZA HUYU MR. MKAPA AZITOE HIZO NYUMBA ZITUMIKE KAMA VITUO VYA WATOTO YATIMA - NA HAYO MAPESA PIA - KWANI ATAVIACHA VYOTE HAPA DUNIANI NA KESHO HUKUMU KWA MUNGU ARUDISHE MGODI WA MAKAA YA MAWE KWA WATANZANIA - aliye karibu naye ajaribu kumkumbusha haya - HUENDA AMEJISAHAU AKADHANI AMESHAFIKA - KUMBE "THIS WORLD IS NOT OUR HOME WE ARE JUST PASSING" BY (a song by late Jim Reeves)
 
Naanza kupata shida tena na kubenea, story hii ktk mwanahalisi hai tally na hata chembe na mkapa na hao waliomjibu na kumshauri, jk yeye ni rais wa nchi hii, tumemuona obama akitengua alot of maamuzi ya george walker bush na hakuna makelele, sasa kama mtangulizi kakosea ni aliyepo kuchukua maamuzi anayoona yanastahili hii ni ikiwa na kuirejesha kiwira, kunyang'anya mali ambazo si halali kwa mkapa na kutengua au kurekebisha mikataba ambayo inaiumiza nchi.

Kinyume cha hapa nasisitiza kujiangalia na mode ya media yetu(mwanahalisi na wengineo) kama kulitumia jina la mkapa kwa kila jambo ambalo ufumbuzi wake ni rahisi tu na kulikuza as if mkapa ni mtume mohamad aliyekabidhiwa koran na kuagiza kuwa no chance for editorial.

Kubenea nilipingana sana na kile ulichokuwa unatufanyia kwenye kila tolea lako, heading was lowasa ,lowasa, lowasa, mkapa, mkapa, mkapa---- sidhani kama unatutendea haki wananchi wenzako, ni kama unatumwa na watu walioshindwa kazi kuanzisha ulalamishi wa kitoto.

Natoa hoja
 
Toka enzi za zama zatanu nba ujamaa wake usofanikiwa kwa kutunyima elimu na kusafiri nje ya nchi kwa manufaa ya taifa na famili zetu leo bado ccm ,chama cha miujiza bado kinataka kuleta siasa za kulindana hebu nendeni8 gongo la mboto mama ana mkapa ana haki gani ya kuchukua ardhi kubwa kiasi kile na kuwaacha wananchi wa pale wakikodolea macho ardhi yao??????????????
Mkapa ashitakiwe kwa au ufisadi au ufisadi ndani ya serikali yake.uhuni mlofanya watosha ati upumzike???????????????kwa lipi? Ulikuwa waogopewa kama mungu mtu?asilimia kumi kwenye jicho na sio pua wewe na wazulumati wa jasho la wananchi.watanzania tubadili utawala ndipo ufisadi utaondoka
 
hukumu yao inakuja, tena iko karibu sana. yenu macho. tukishindwa sisis wanadamu, Mungu mwenyewe ataingilia kati.
 
Back
Top Bottom