- Karibu sana mkuu, nimekwambia anytime unapohitaji taarabu karibu sana, ninazo kibao on you! ha! ah! ha! ha! ha! vipi kwenye ule mkutano utakuja tena kwa mgongo wa Professor? ha! ha! ha! ha!
Es!
Huhitaji akili nyingi kujua nani ni mkurupukaji kati yetu. Kama ulifuatilia kesi ile vizuri utajua kwamba kinachofanyika sasa hivi ni kuinyonga haki na dhana ya kwamba wakubwa hawastahili kwenda jela! Kama ungekuwepo pale IFM (mimi nilikuwepo) wakati wa video evidence ambayo Marando aliipinga sana (bila mafanikio) ungejua kwamba nchi hii ilipaswa kugeuka kuwa China kwa muda na kumtia adabu Mahalu. Yule muuzaji wa jengo lile alionyesha kushangazwa na Tanzania kuwa na maofisa ambao wanalazimisha kutengeneza mikataba miwili tean mmoja ambao una-inflate bei ya mauzo na huku Mahalu akikiri wazi kwamba alitaka kujipatia kitu. Na kwa nini ilielekezwa fedha hizo za malipo ziingie kwenye akaunti binafsi ya Mahalu. Fungua macho! Usiingie kwenye mkumbo wa watu ambao wana chuki binafsi na rais na kubeza hata yale ambayo yanafanyika kuwasaidia watanzania. Kwa mwenendo huu hakika kuna haja ya kutangaza wazi kwamba kila aliye na dhamana ya mali au rasilimali za umma sasa ajichukulie tu! Hivi mnadhani Mahalu ni malaika? Ulizeni mtaambiwa. Jiulize kwa nini imechukua miaka hataki kujitetea kama hana hatia na ana utetezi wa nguvu? Hivi tutabadilika lini na kuweka maslahi ya taifa mbele? Kama Kikwete ni mtu wa bifu basi angemwadhibu Prof. Mwandosya. Mbona wanapiga kazi pamoja tena bila matatizo? Acheni kulishwa sumu na huku mnachekelea!
Mbopo:
1(red): - Kama ulifuatilia kesi ile vizuri utajua kwamba kinachofanyika sasa hivi ni kuinyonga haki na dhana ya kwamba wakubwa hawastahili kwenda jela! Hii inajulikana kama PREJUDICE. Nani kakwambia wewe una uwezo wa ku-judge? Washitakiwa hata hwajaanza kujitetea wewe tayari unapitisha hukumu? Au kama walivyosema Wakwere wenzako, lazima profesa aende na maji?
2 (blue): - Kama ungekuwepo pale IFM (mimi nilikuwepo) wakati wa video evidence ambayo Marando aliipinga sana (bila mafanikio) ungejua kwamba nchi hii ilipaswa kugeuka kuwa China kwa muda na kumtia adabu Mahalu
Sheria ya kutumia video conference kwenye uendeshwaji wa kesi, na yatokanayo ndio kwanza imepita. Wakati ule ilikuwa bado! kilichojiri pale ni kituko ukiacha ukiukwaji wa taratibu na haki . Unathubutu kukiri kwamba ulikuwapo pale! Kama umesomea sheria na ukafuzu(?) basi wewe ni walewale wa za chupi. Shame on you
3 (darkred): - Kama ungekuwepo pale IFM (mimi nilikuwepo) wakati wa video evidence ambayo Marando aliipinga sana (bila mafanikio) ungejua kwamba nchi hii ilipaswa kugeuka kuwa China kwa muda na kumtia adabu Mahalu Wewe mzushi. Muuzaji wa jengo lile hajawahi kutoa ushahidi wowote. Upande wa mashitaka ulipaswa kuwasilisha ushahidi wa muuza jengo. Hawakufanya hivyo. Badala yake wakatumia mihela kibao kumleta yule Notary Public na kuhakikisha anasema waliyotaka kusikia. Ilipofika zamu ya Utetezi kumhoji, HAKIMU MWANGESI akachomoa. Ati mda umekwenda sana, ipangiwe siku ingine. Siku hiyo ni ile ya video kwani Papi alikataa kata kata kurudi Bongo. Shahidi wa piili toka Italia, Avvocato Georgio alifariki siku moja kabla ya kujitokeza kwenye video conference hiyo hiyo. Wewe Mbopo, URONGO ni URONGO tu hata upindishe vipi!
... By the way kwani Mwandosya angeadabishwa kwa kitu gani vile? Anahusika vipi?
.... By the way, DPP alipoenda kwa Mzee Mkapa akimsihi ajiengue kwenye ushahidi alitolewa nje, sawasawa na Mzee Warioba na wengine wote. kwa taarifa yako na wenzako, Mzee wa watu yuko tayari kwenda pale Kisutu hata kuwa in-person badala ya Kamera. Siku hiyo wewe na wazushi wenzako mchimbe.
- Mahalu hawezi kushinda hii kesi, na akishinda ni uoga wa wasimamizi wa sheria na sio CCM wala Rais, maana ukweli upo wazi kwamba hapa kuna wizi umefanyika, ndio haya tunasema kila wakati kwamba waoga ni sisi wenyewe watendaji wa level za chini, halafu baadaye tunalilia Rais na CCM!
- Sasa Marando naye si tulisema kwamba alikuwa kila siku kushinda kwenye ndege ya Rais Mkapa sasa ndio wakati wa kulipia zile fadhila, huku alikilia mafisadi kwenye Chadema! ha! ha! hili taifa bwana!
Es!
Mawakala wa ufisadi utawajua tu! Hata kwa Liyumba na Babu Seya mlisema hivyo hivyo. Nadhani nchi hii imelaaniwa!
Wewe acha kulaani nchi yetu!
Hii kesi imeisha siku nyingi...Sirikali inatafuta pa kutokea tu!!
Please tupe source za hii information.....napita!!! nikirudi nitachangia kama utakuwa umetekeleza ombi langu.
Mawakala wa ufisadi utawajua tu! Hata kwa Liyumba na Babu Seya mlisema hivyo hivyo. Nadhani nchi hii imelaaniwa!
Naweza kusema kuwa siasa za ujanjanja na hovyohovyo zimefanikiwa kuifikisha nchi kwenye state of paralysis, from state capacity to political thinking even among the self anointed critical citizens....
Nimejaribu kuisoma hii sijui ni ripoti ama makala kuona ni wapi ama ni vipi Mkapa amemkaanga Kikwete zaidi ya kujikaanga mwenyewe sioni.
Nikiangalaia kwa karibu nakubaliana na Mbopo kuwa huu ni muendelezo wa siasa za ujanjaujanja ambazo sasa zinaelekea kujikita katika mahakama zetu na kugeuza kuwa kama yale majukwaa rasmi na yasiyo rasmi kisiasa ambayo inaelekea kwa baadhi ya wanasiasa kama Mabere Marando, hayajatosheleza kufisadisha siasa za nchi yetu kwa manufaa ya muda mfupi na yale binafsi.
Watanzania wote tumegeuzwa kuwa mashabiki wa ama upande wa Kikwete ama upande wa "Wengine" bila ya kujali jukumu letu la kuweka mbele umakini zaidi ya ushabiki katika kufuatilia, kuchambua na kuzungumzia maswala muhimu ya kuikomboa nchi yetu kama ambavyo tunapenda kujinadi.
Siamini kama ushahidi huu wa kuwa serikali ilikuwa na taarifa na kwamba eti taratibu zote zilifuatwa zingeliweza kuwa ushahidi wa maonevu dhidi ya mshitakiwa katika macho ya washabiki wa upande mwengine ambao unadai kuwa huu ni uonevu na ulipaji kisasi.
Wote hapa tunajua kuwa utawala wa Mheshimiwa Mkapa ulikuwaje, inashangaza kuona kuwa kuna watu wanadhani kuwa Waziri wa wakati ule alikuwa na uwezo wa kukataa kile ambacho bosi wake Rais anataka ama amekubali kifanyike.
Lakini pia inashangaza kuona kuwa usemi wa kuwa ununuzi huo ulifuata taratibu na ulikuwa na baraka zote za serikali unaweza kusafisha uwezekano wa wizi ama rushwa wakati wote tunajua kuwa hata EPA ilikuwa na baraka na utaratibu uliofuatwa.
Halafu huu mchezo wa kukimbilia kuwa kesi kama hizi ni uthibitisho dhana, madai ama shutuma kuwa Rais ana hulka ya kisasi ni ujinga na upumbavu. Haiwezekani watu tupige kelele Rais achukuwe hatua dhidi ya ufisadi na mafisadi halafu anapochukuwa hatua dhidi ya wale ambao hawamo katika listi zetu za kuwachukia ama kuwahukumu kuwa ndio mafisadi basi Rais ndio ageuzwe mkosaji.
Kwa mtazamo wangu, fikira kama hizi ndio zinazowavunja nguvu na kuwafanya baadhi ya viongozi wetu kuamua ama kujiunga na ufisadi ama kuunyamazia huku wakilinda na kuboresha maslahi yao kwani wanakuja amini kuwa hao wanaopaswa kuwapigania ni mabingwa wa kutoa shukurani za punda kwa kuwapiga mateke pale wanapojitahidi kuwatetea na kuwalinda.
Zaidi naamini umefika wakati na ni muhimu kwa Uongozi wa Mahakama zetu kuchukua hatua kuzuia madhubutu kuhakikisha kuwa mahakama zake hazirasimishwi kuwa majukwaa ya siasa za ujanjaujanja na hovyohovyo kama ambavyo imekuwa ikijionyesha katika miaka ya hivi karibuni. Kama kweli hii habari imetolewa na upande wa utetezi unaongozwa na Wakili Marando ambaye hivi karibuni amekuwa wazi akitumia habari ama sehemu yake katika shughuli za mahakama kufanyia siasa, ni lazima hatua kali zichukuliwe kabla hali hii haijaota mizizi. Inatosha kuona jinsi mahakama zetu zimegeuzwa kuwa kisima cha rushwa na uonevu mwengine, kuruhusu siasa za majukwaani kuota mizizi katika mahakama zetu ni kucheza na hatima ya nchi yetu.
- Maneno mazito sana haya mkuu, yanahitaji kuyatafakari sana!
William @ NYC, USA.
ndio.....uko sawa kabisa...alichukizwa sana na lile neno alilosema mahalu kipindi kile jk ni waziri wa mambo ya nje....akasubiri alipoingia ikulu ndo akaanza kumkaanga pasipo kujua madhara yake sasa mzee mkapa kamwaga yote
You are better than this! Yaani badala ya nyie kushangazwa na kitendo cha Mkapa kujishushia hadhi yake kwa sababu tu ya urafiki, sasa mnamshutumu Kikwete kwa kufanya kitu ambacho asingefanya mngemlaumu. Sisi wengine tunajua kabisa juhudi ambazo Mkapa alizifanya kuhakikisha kwamba Mahalu hashitakiwi kwa sababu tu ya urafiki wao. Lakini ukweli ni kwamba ushahidi uliotolewa mahakamani umemuumbua Mahalu na ndiyo Maana Marando na wenzake walihaha sana kukimbia kila mahakama ili Mahalu asijitetee wakati tayayri kuna uamuzi wa kwamba ana kesi ya kujibu.Hii affidavit ya Mkapa ilikuwa itumike kuombe Nolle Prosequi lakini Mkurugenzi wa Mashitaka alipokataa ndo sasa wakaamua kuitoa hadharani ili kutafuta public sympathy, na huyu Marando akawa anatamba kwamba sasa wanaandika barua ya kuomba Kikwete akatoe ushahidi halafu wai-leak kwenye press na kweli wakafanya hivyo. Hivi mpaka hapo hamuoni kwamba kuna tatizo hapa. Tena wanaofanya hivyo ndiyo wale wanaojifanya kupambana na ufisadi (Marando akiwa Chadema) na huku akifanya mambo ambayo mengine ni kinyume na maadili ya taaluma yake. Nchi hii ni ya ajabu sana. Mtu akiwa mwizi wa mali ya umma watu wanamuona kama shujaa na kumpongeza. Hivi kuna nini cha kupongeza hapa wakati profesa mzima wa sheria anafanya forgery ya wazi na ya kitoto ili kukomba hazina ya nchi? Halafu nyie hao hao mnapigia kelele ufisadi mwingine wakati huu wa Mahalu mnauchekea!