Mkapa ameondoka katu hatorudi tena

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,934
3,805
Wengine tuliobaki ,tunjiani twasogea.
Mkapa ameondoka, katu hatorudi tena.

mengi ametufanyia kwa hisabu sikumbuki
Mkapa ameondoka katu hatorudi tena

Kama wanafunzi bora,tuyasome yake mema.
Mkapa ameondoka katu hatorudi tena

Sisemi hana mabaya,ya pemba si ya kuigwa
Mkapa ameondoka katu hatorudi tena

Majuto ni mjukuu,tuige yake mazuri
Mkapa ameondoka katu hatorudi tena

Tanzania yetu sote,wengine kwao ni gumu
Mkapa ameondoka katu hatorudi tena

Moja haliwezekani,sote tuwe ni Raisi
Mkapa ameondoka katu hatorudi tena

Nchi huwa na mmoja,na wote akiwalinda
Mkapa ameondoka katu hatorudi tena

Haki bora kuitenda,hata kwa wako swahiba
Mkapa ameondoka katu hatorudi tena

Magufuli hala hala,mbele yako uchaguzi
Mkapa ameondoka katu hatorudi tena

Hebu tangazia umma, za wizi uzikatae
Mkapa ameondoka katu hatorudi tena

Ushindi uliobora ,si wa kuzidisha moja
Mkapa ameondoka katu hatorudi tena

Mwisho wa siku majuto,Mkapa ameandika
Mkapa ameondoka katu hatorudi tena.


.....Endelezeni ka mna ubavu
 
Magu amemfuata alikokwenda mwenzake
Kwa waliyotutendea huenda wakakutana.

Alishinda kwa makeke,kwenye uchaguzi ule.
Kwa waliyotutendea huwenda wakakutana.

Bado hakujielewa ,safari aliyopata.
Kwa waliyotutendea ,huwenda wakakutana.

Magu alikuwa ladu enzi za uhai wake.
Kwa waliyotutendea ,huwenda wakakutana.

Kila aliesikia .aliona ladha yake.
Kwa waliyotutendea ,huwenda wakakutana.

Leo wewe huna kazi,niuongo ndugu zangu ?
Kwa waliyotutendea ,huwenda wakakutana.

Tuseme tumepoteza,kifaa adimu sana.
Kwa waliyotutendea ,huwenda wakakutana.

Hata ukiangalia,kwa mbali utayaona.
Kwa waliyotutendea ,huwenda wakakutana.

Wapo waliopotea ,nga pemba tukijua
Kwa waliyotutendea ,huwenda wakakutana.

Mliotimiza lengo,fanyeni yakuridhisha.
Kwa waliyotutendea ,huwenda wakakutana.

Msione mmefika ,wangine kuwashupaa
Kwa waliyotutendea ,huwenda wakakutana.

Magu ametenda mengi,yakupigiwa mfano.
Kwa waliyotutendea ,huwenda wakakutana.

Ila mengine kinehemachungu kuyatamka
Kwa waliyotutendea ,huwenda wakakutana.

Nilimpenda kwa yangu,wengine nao kwa yao.
Kwa waliyotutendea ,huwenda wakakutana.

Kasoro ni zetu mila,mengine ni ya ubabe.
Kwa waliyotutendea ,huwenda wakakutana.

.....Endelezeni ka mna ubavu
 
Back
Top Bottom