Mkapa aitahadharisha serikali

Jul 24, 2012
81
6
Mkapa atahadharisha Serikali kuwa makini Send to a friend
Wednesday, 01 August 2012 21:14


Ibrahim Yamola
RAIS Mstaafu Benjamin Mkapa, ameitaka Serikali kushirikina na wadau wa sekta binafsi katika mchakato wa kusaini Mkataba wa Ushirikiano na Makubaliano ya Uchumi (Epa) kati ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Umoja wa Ulaya (EU).

Rais Mkapa aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati wa sheherehe ya siku ya Sekta Binafsi iliyoandaliwa na Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), huku akitaka kabla ya kusaini makubaliano hayo lazima kuweka maslahi ya taifa mbele.

“Mnatakiwa kuwa makini kuhakikisha maslahi ya taifa letu yanakuwapo, hilo ndilo linalotakiwa kuwekwa mbele kwani bila kufanya hivyo tutajiweka matatani,” alisema Mkapa na kuongeza:
“Kutokufanya hivyo mtawapa nafasi hawa EU kufanya wanalolitaka katika nchi zetu, hivyo mkijipanga kama EAC na kuwa na sauti moja hakika mtawatendea haki wananchi.” :israel:

Rais Mkapa alisema madhara ya kusaini mkataba huo ni kuwapa nafasi kuingiza bidhaa zao nchini bila kuwapo kodi yeyote, kitendo ambacho kitasababisha kukosa mapato kwa taifa.

“Kwanza mtanakiwa kutambaua hawa EU wanataka nini kutoka kwetu na sisi tunataka nini, mkijua hilo mtahakikisha mnatetea wananchi wenu,” alisema Rais Mkapa na kuongeza:

“Kwanza mnatakiwa kuhakikisha wawekezaji wa ndani wanakuwa tofauti na wageni, ili kuleta tofauti na maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumala, kwani kuna baadhi ya wawekezaji wa kigeni wanafanya kazi ambazo zinaweza kufanywa na wetu.”

Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk Abdallah Kigoda alisema wamesikiliza maoni ya wadau na watahakikisha wanayafanyia kazi kwa mstakabali wa maendeleo ya taifa.
Dk Kigoda alisema hakuna nchi yeyote duniani iliyopiga hatua ya maendeleo bila ya kushirikisha sekta binafsi, hivyo wanatambua mchango wao na wataitumia kikamilifu.

“Tutaangalia matatizo yanayowakumba pale wanaposafirisha bidhaa zao kwenda nchi za nje hususan za EAC, ili kuhakikisha tunaondoa na kudumisha ushirikiano wetu,” alisema Dk Kigoda.
souce ni website ya gazeti la mwananchi:israel:
 
Mkapa alikuwa wapi kufanya haya wakati nae katoka humohumo hakuna jipya hapo
 
Alichosema kina mantiki lakini na yeye alikuwa wapi wakati wa Barrick au anamaanisha nikwa weusi wenzetu tu?
 
Nirahisi sana ukiwa nje ya system kuona mapungufu ya wenzako walio ndani ya system. Lakini ukipewa nafasi hayo yote uliyokuwa unawalaumu wenzako nawe unaanza kuyaendeleza kwa kasi ya ajabu mpaka kila mtu anakushangaa. Hivyo BWM amesema ukweli lakini kwa sasa ansumbuliwa na hako kaugonjwa ka Ndani/Nje system.
 
Haya anayoyasema,kama angeyafanya kwenye utawala wake tusingekuwa hapa tulipo.
 
Nirahisi sana ukiwa nje ya system kuona mapungufu ya wenzako walio ndani ya system. Lakini ukipewa nafasi hayo yote uliyokuwa unawalaumu wenzako nawe unaanza kuyaendeleza kwa kasi ya ajabu mpaka kila mtu anakushangaa. Hivyo BWM amesema ukweli lakini kwa sasa ansumbuliwa na hako kaugonjwa ka Ndani/Nje system.

umeongea vizuri sana mkuu...hii uwakumba na wapinzani wengi sana wa kisiasa hapa Afrika na kwingineko..wakiwa nje aah wanaona kila kitu na wana majibu ya kila tatizo wakiwa ndani tu ya wanashindwa wanaanza na wenyewe kulipua na kuziba ziba viraka hapa na pale ili mradi siku zifike wastaafu
 
Mnafiki mkubwa alipobinafsisha mashirika ya umma na kuwapa wawekezaji akukumbuka na wala kufukiria maisha ya watanzania baadae,maelfu ta watz walikosa ajira na wanaendelea kuteseka mpaka leo.Ni bora apige kimyaaaaa!
 
bora anyamaze kimya, yeye alituny.e.a mwenzake anataka kujamb.a anaanza kupunga upepo kwenye pua. Sera ya chama chao lazima wazifuate-Uza nchi peleka vijisenti Ulaya!
 
he have go to hell.....he have very poor of character of judgement and himself labeled very smart!
 
mkapa lalishindwa kuyafanya hayo na kushauri tangu akiwa waziri wakati wa mwalimu,wakati wa mwinyi,mpaka akaja kuwa Rais,aache uzushi,atulie tu kando hana lolote zaidi ya unafiki!
 
he have go to hell.....he have very poor of character of judgement and himself labeled very smart!
Wakati wa utawala wake watu walikuwa wakisema haya anayosema yeye anawaita WAVIVU,UWEZO WAO WAKUFIKIRIA NI MDOGO AU WAMESUKUMWA NA WIVU.Kwenye context sijui yeye inamweka kundi gani?
 
Chezea wanasiasa weweeeeee.. Wote babayao ni mmoja.. Ngoja na JK amalize mda wake eti naye utasikia anatoa ushauri.... Halafu hata aibu huwa hawana.
 
Mkuu, ninajua una uchungu mwingi!
Lakini tukubali kwamba hata Musa alilelewa na Farao!

Pamoja na kulelewa kwa Farao lakini MWISHO MUSA ALIKATAA KUITWA MWANA WA BINTI FARAO na akasema ni Bora kwenda Kufa kwa njaa na wana wa Israeli kuliko Kufaidi vinono utumwani...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom