Mkapa aenda kusimamia kura za maoni Sudan | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa aenda kusimamia kura za maoni Sudan

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 4, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Mkapa aenda kusimamia kura za maoni Sudan


  Na Andrew Ignas

  RAISI Mstaafu wa awamu ya tatu, Bw. Benjamini Mkapa amewataka Watanzania kumuombea aweze kusimamia upigaji kura za maoni Januari 9 mwaka huu ambazo
  zitakuwa ndio zinatarajiwa kutoa mstakabali wa amani ya Sudani.

  Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili jana ofisi kwake jijini Dar es salaam, Msemaji wake, Bw. Azizi Mlima alisema kuwa, Watanzania wanapaswa kumuombea dua Bw. Mkapa ambaye anatarajiwa kuondoka leo kuelekea nchini humo kusimamia shughuli hiyo ifanyike kwa amani na utulivu.

  Alisema kuwa Mkapa ambaye aliteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon anatarajiwa kuondoka leo kwenda kusimamia shughuli ya upatanishi baina ya serikali mbili, Sudani Kusini na Sudani Kaskazini, ili kupata muafaka wa kuunda serikali moja.

  "Mkapa anatarajia kuondoka kesho (leo) ili kuandaa taratibu za awali kwa ajili ya siku ya kura za maoni ambayo inatarajia kufanyika tarehe 9 ya mwezi huu nchini humo, hivyo Watanzanai wanatakiwa kuiombea nchini hiyo kuwepo amani wakati wa zoezi hilo," alisema Bw. Mlima.

  Hata hivyo, alisema kuwa kiongozi huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Usimamizi wa Kura za maoni kwa nchi hiyo, anakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhakisha anasimamia kwa ukamilivu shughuli hiyo ili hali ya amani iweze kupatikana.

  [​IMG]
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Ya TZ yalimshinda sasa kiherehere huko ni cha nini?
   
 3. M

  MLEKWA Senior Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 18, 2007
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MKAPA NI CHAGUO LA VATICAN m wakatoliki Wenzake wali loby vya Kutosha kwa Obama kupata choice yao Mkapa huu ndio Ukweli usiofichika.
   
 4. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mmmh!...ok!
   
Loading...