Lowassa alishiriki Richmond 100%
Kama ndivyo,basi anatudanganyia nini anavyosema Aliundiwa kashfa? Anapaswa kuadhibiwa kwa ulaghai huu?
Huyu bwana alikuwa na project nyingine ya ulaji pia:mvua ya kutengeneza. Je alifanikiwa kutengeneza mvua ya kuweza kujaza mtera?mpaka anaondoka pale ilikua haijalipwa hata senti tano shahidi zakia meghji shemeji yake kikwete alikua waziri wa fedha kipindi hicho
Kuna mtandao unatoa MIMINA I guess ww ni member wa huo mtandao wa kumimi.....wa
Alitakiwa aseme kipi kilianza tume ya sita na Mwakyembe au richmond? Na aseme je ni chini ya uwaziri wake mkuu ndio tulikuwa giza ?
Na aseme je ndiye yeye aliyeshikiri mzabuni wa Richmond kupewa tender na kunyimwa kampuni mahiri kama GE?
Na aseme je ulikuwa mpango wake na swahiba wake Rasta aziza kuingiza Richmond nchini na Generoator za GE alizotumia Gire wakuijua ni nzima na kutumia wafanyakazi wa tanesco ku zi sabbotage ili zisiwake, kwa deal la kumkimbiza gire ilimwisho ama wazitaifishe ama wazinunue ili wao ndio wazalishe umeme kama ilivyotokea kwenda Dowans??
Aseme je deal zima lilinzia wapi?
Na aje aseme kwanini alikaa kimya muda wote huo. Na kama ni kulinda serikali za uhujumu je mangapi bado anayalinda wakati nchi inahujumiwa na kuporwa?
Kama kaweza kulinda uozo akiwa waziri atafanyaje akiwa raisi si atauza nchi kisha kulinda wahujumu??
Wameungama?!!
Anyway,ukweli kuhusu Richmond utakuja julikana siku CCM wakitoka madarakani na si vinginevyo.
ilikua fake,ila kina mwak,walicheza na lugha.
ishu ya umeme ilikua ni ya dharura,na hivyo taratibu zikaenda kidharura ili watu wapate umeme,,Nadhani baadhi ya taratibu za zabuni zikarukwa ili ipatikane kampuni itakayoleta mashine.
huwa nashindwa kuelewa wanaodai pesa za richmond ziliibiwa ni zipi hizo
Sawa mkuu.
Ebu niweke sawia hapa,
1.Mkataba ambao Lowassa alitaka kuuvunja ila akauiwa na mwenyekiti ulikuwa baina ya TANESCO na RIchmond ipi kama hii ilikuwa feki?
2.Kitu alichokificha Lowassa kwa heshima ya serikali yake na chama chake(kumb.tamko la kung'atuka bungeni) kilikuwa kipi ambacho kingeiangusha serikali yote kama sio ufisadi wa Richmondi?
3.Kama hamna wizi uliotokea kwa nini alikubali kufanya MAAMUZI MEPESI ya kujiuzulu kwa ajili ya kashfa ya kutunga? Karibu mkuu.
Unajua waziri mkuu ana-reort kwa nani? huyo anaye m-report- ndo alimshinikiza, ingawa bado si uadilifuLowassa alishiriki Richmond 100%
Wanajukwaa,salam,
Baada ya kumsikia waziri Mkuu wa zamani,ndugu Edward Lowassa na baada ya kusoma michango mbalimbali humu ukumbini kutoka kwa wanaomuunga mkono na wanaompinga kuhusu ''safari ya matumaini'' nahisi mkanganyiko,
1.Inasemwa kashfa ya Richmondi ilitungwa tu na akina Sitta na Dr Mwakyembe ili ku muangusha Kwenye uwaziri mkuu.Hivyo hapakuwa na kitu halisia kama Richmond scandel,ilibuniwa tu,
2.Lowassa kasema hakufanya kitu chochote kuhusu Richmond bila kumshirikisha mh.Rais.Hata alifikia hatua ya kutaka kuvunja mkataba ila hakukubaliwa.Hapa,je,huo mkataba aliotaka kuuvunja ni upi kama Richmondi ilikuwa ni kitu ya kubuni? Ina maana angevunja mkataba dhahania?
3. Ndg Lowassa anasema alikaa kimya kwa muda mrefu wa takribani miaka saba ili kuilinda Serikali (rais) na chama! Kwa hiyo hapa rais mtarajiwa anakiri kuwa mradi wa Richmond ulikuwa ni ufisadi mkubwa hata wa kuiangusha serikali! Na hivyo,je,tujue lipi,kwamba ni rais pekee ndio alikuwa mhusika wa Richmondi au Rais na Waziri mkuu wake(Lowassa) walihusika pamoja ila yeye alikaa kimya ili bosi mwingine apone(Hapa kama ndio hivyo maana yake uzalendo wake ni kwa mtu na siyo nchi?)
4.Ripoti ya kamati ya Dr.Mwakyembe ilionesha vimemo kutoka kwa PM kwenda kwa mawaziri na mpaka wabunge wa ccm wakashawishika kumhusisha Lowassa na Richmond.Ina maana hawa walikuwa hawaelewi mtego wa Sitta na Dr Mwakyembe,walikuwa wamehongwa au kipi kilitokea?
(Akina ole Sendeka,Kilango Malecela et a' nasikia wameshaungama)
Yote kwa yote,Richmondi ilikuwa kitu REAL au FAKE?
Kama ilikuwa real,Lowassa hakushiriki kabisa au alishiriki pamoja na mh.Rais ila baadae akatolewa sadaka kwa niaba ya mkuu?
Na kama alishiriki pamoja na mkuu wake kwa nafasi yake kunamfanya asiwe fisadi?
Karibuni Wajuaji,mtufumbue wengine macho.
Unajua waziri mkuu ana-reort kwa nani? huyo anaye m-report- ndo alimshinikiza, ingawa bado si uadilifu
Hayo yote sawa lkn ile mitambo ya richmond/dowans ilinunuliwa na symbion tena obama na hillary wakaja ifungua je naanza kupata waswas wake je bwana mkubwa alikuwa hajui mpk kukana kwmba hajui wamiliki wa dowans