Mkanda wa mauaji wa chumba namba 1046( Kivuli cha 'Don' na jasho la wapelelezi)

SteveMollel

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
8,430
23,751
MKASA WA MAUAJI YA CHUMBA NAMBA 1046. (KIVULI CHA 'DON' NA JASHO LA WAPELELEZI)
.
.
.
.
Katika jiji la Kansas, Missouri, mchana wa mwezi wa kwanza, tarehe 2 mwaka 1935, mwanaume mmoja aliingia ndani ya HOTEL PRESIDENT akihitaji chumba kwenye ghorofa kadhaa za juu.
.
.
.
Hakuwa amebeba mzigo. Alijisajili kwa jina la “Roland T Owen” wa Los Angeles, na akalipia makazi ya siku moja.
Mwanaume huyu alielezewa kuwa kijana mrefu mwenye sauti ndogo ya kukwaruza, nywele nyeusi na kovu kubwa upande wake wa kushoto wa kichwa. Alipewa chumba namba 1046.
.
.
.
Akiwa anaelekea kwenye chumba alichopewa, Owen akamwambia mhudumu, kwa jina Randolph Propst, kwamba mwanzoni alikuwa anafikiria kuchukua chumba kwenye hoteli ya Muehlebach, lakini akashindwa kwasababu ya ughali wa chumba ndani ya hoteli hiyo, $5 kwa usiku mmoja tu.
.
.
.
Walipofika chumba namba 1046, Owen akachukua kitana, mswaki na dawa ya meno kutoka kwenye koti lake na kuviweka bafuni. Alafu, Owen pamoja na mhudumu, Randolph, wakaongozana mpaka ukumbi wa mapokezi baada ya mhudumu kufunga chumba hicho.
.
.
.
Mhudumu alimkabidhi Owen funguo, Owen akaondoka mhudumu akiendelea na kazi zake za kawaida.
.
.
.
Baadae ndani ya siku hiyo hiyo, mhudumu mwanamke aliyevalia sare nadhifu, alienda kutimiza majukumu yake ya kusafisha chumba namba 1046. .
.
.
Owen alikuwa ndani ya chumba. Alimruhusu mhudumu aingie ndani akimwambia aache mlango pasipo kuufunga kwa komeo kwasababu alikuwa anategemea ujio wa rafiki muda si mrefu.
.
.
.
Ndani ya chumba hicho, pazia za madirisha zilikuwa zimeshushwa na kufungwa vema. Kulikuwa kuna taa ndogo tu ikiwaka kujitahidi kung’arisha chumba japo kwa udhaifu. Kiufupi, mwanga haukuwa wa kutosha.
Mhudumu huyu baadae alikuja kuwaambia polisi kuwa Owen alionekana ni mwenye hofu na asiye na amani. Macho yake hayakuwa na furaha, na uso wake ulikuwa umezubazwa kwa woga.
.
.
.
Wakati mhudumu akisafisha chumba, Owen akavaa koti lake na kuondoka akimsisitizia mhudumu kutofunga mlango.
.
.
.
Kwenye majira ya saa nne usiku, mhudumu huyu akarudi kwenye chumba hichi akiwa amebebelea mataulo masafi. Mlango ulikuwa bado haujafungwa, na chumba bado kikiwa gizani.
.
.
.
Owen alikuwa amejilaza kitandani akiwa amevalia kamili. Mhudumu aliona kikaratasi kidogo juu ya meza kikiwa kimeandikwa na kusomeka:
“Don, nitarejea ndani ya dakika kumi na tano. Ngoja.”
.
.
.
NINI MAANA YA UJUMBE HUU?
.
.
.
Huu ujumbe si tu kwamba ulionyesha Owen alikuwa anatarajia ugeni, lakini pia ugeni wa aina gani.
Jina la ‘Don’ ambalo ndiyo ujumbe umelengewa, ni jina litumikalo Hispania, Ureno, Italy na mpaka huko Ufilipino kama kianzio cha jina la mtu mwenye mamlaka na cheo.
.
.
.
Huko Amerika ya kaskazini, jina la ‘Don’ lilifanywa maarufu sana kwa njia ya filamu za kimafia, kama vile ‘The Godfather’ ambamo ndaniye kiongozi wa uhalifu hudai ishara za heshima ambazo kiuhalisia zilikuwa zinatolewa kwa viongozi wa hadhi huko Italia.
.
.
.
Hivyo Owen alikuwa anamngojea ‘Don’. Ujio mkubwa kabisa huu kwake. Don hakutani na kijakazi wake kwa jambo dogo, bali nyeti na muhimu. Huwa hawana masikhara kazini, hawaperembi na hawana muda wa kupoteza. Kuua kwao ni kama kuria uji.
Si bure Owen alikuwa anahofia. Hakuwa na furaha wala amani. Kwani alishindwa kukimbia kuokoa nafsi yake? Si rahisi kama unavyowaza.
.
.
.
Bila shaka rejelea za Dons kama wakina Richard ‘The Iceman’ Kuklinski, Giovanni ‘The Pig’ Brusca, Roy DeMeo na Joseph ‘The Animal’ Barboza zinaweza zikakuonyesha hawa wanyama ni watu wa aina gani unapokatiza kwenye mstari wao mwekundu.
.
.
.
TURUDI CHUMBANI…
.
.
.
Baada ya hapo, Owen alikuja kuonekana asubuhi ya kesho yake saa nne na nusu mhudumu alipokuja kusafisha chumba chake.
.
.
.
Alifungua mlango kwa kutumia ‘passkey’ (kitu mhudumu anachoweza kufanya kama tu mlango ukiwa umelokiwa kwa ndani). Alipoingia, akashangaa kumkuta Owen ameketi kimya kwenye kiti, akitazama giza. Hakuonekana kama mtu anayejali.
Hali hii ya tahamaki ilivunjwa na mlio wa simu ya Owen, mwanaume huyo akapokea na baada ya muda, akasema:
“Hapana, Don. Sihitaji kula. Sina njaa. Nimepata tu kifungua kinywa.”
Kisha akakata simu. Kwa sababu fulani zisizofahamika, akaanza kumpeleleza mhudumu kuhusu ile hoteli na majukumu yake ndani ya hoteli. Akarudia tena malalamiko yake juu ya ughali wa hoteli ya Muehlebach uliomfanya aachane nayo na kuja hapo, President Hotel.
.
.
.
Mhudumu alipomaliza kufanya usafi, akachukua mataulo yaliyotumika, akaondoka, pasipo mashaka akiwa na furaha kwa kumuacha mgeni huyu wa ajabu.
.
.
.
MKASA CHUMBANI WAANZA KUJITENGENEZA.
.
.
.
Mchana wa siku hiyo, kwa mara nyingine mhudumu akaenda tena kwenye chumba cha Owen na mataulo masafi. Nje ya mlango, akasikia wanaume wawili wanaongea kwa ndani.
Alibisha hodi akajitambulisha pamoja pia na dhamira yake. Ila sauti nzito ngeni ikamjibu hawahitaji mataulo yoyote, akapandisha mabega na kuondoka zake.
.
.
Ina maana huyo ndiyo alikuwa Don? – mgeni ambaye Owen alikuwa anamngojea?
.
.
Mhudumu alijiuliza kuhusu sauti hiyo aliyoisikia, ya nani? ila asijisumbue, akapuuzia na kuendelea na yanayomhusu.
.
.
.
MIRIRI YA MIKASA HOTELINI:
.
.
.
CHUMBA NAMBA1048:
.
.
.
Baadae ndani ya siku hiyo, kuna mteja mwingine alikuja ndani ya hoteli PRESIDENT, akihitaji chumba kwa ajili ya mapumziko. Alikuwa ni mwanamke akijisajili kwa jina la Jean Owen (hana mahusiano yoyote na Owen wa chumba namba 1046).
.
.
.
Akapewa chumba nambari 1048. Karibu kabisa na kile cha Roland T Owen, 1046.
Mwanamke huyu hakupata usiku wa amani kabisa. Alisumbuliwa pasipo kikomo na sauti ya juu ya kama vile mwanaume na mwanamke wakizozana vikali. Baadae akasikia sauti ya mtu akiwa kama anahaha kutafuta hewa. Ila akadhani pengine itakuwa ni kukoroma.
.
.
Alijiuliza kama ana haja ya kutoa taarifa, ila akaamua kupuuza.
.
.
.
'KAPO' YA AJABU HOTELINI.
.
.
.
Chrarles Blocher, muendesha lifti ya hotel, pia naye aligundua jambo halipo sawa usiku huo. Kulikuwa kuna mambo ambayo alidhania ni tafrija ya makelele ndani ya chumba namba 1055.
.
.
.
Muda fulani baada ya usiku wa manane, alimpeleka mteja fulani mwanamke kwenye sakafu ya kumi ya hoteli. Mwanamke huyu alikuwa anaulizia chumba namba 1026.
.
.
.
Blocher alishawahi kumuona mwanamke huyu maeneo ya hotelini mara kadhaa akiwa na wanaume kadhaa kwenda vyumba kadhaa.
Baada ya dakika chache, alipewa taarifa ya kurejea sakafu ya kumi. Mwanamke huyo alikuwa ameguswa maana mwanaume aliyekuwa na miadi naye hakuonekana. Blocher hakuwa na cha kumsaidia hivyo akajishukia zake chini.
.
.
.
Lakini nusu saa mbele, mwanamke akamuita tena Blocher amshushe chini kwenye korido kubwa ya kuchagulia vyumba. Punde mwanamke huyo akarudi kwenye lifti akiwa ameongozana na mwanaume, Blocher akawapeleka kwenye sakafu ya tisa.
Kwenye majira ya saa kumi usiku, mwanamke huyo akaondoka, akifuatiwa na mwanaume nyuma.
.
.
.
Hii kapo haikuwahi kuja kutambulika, na haikuthibitika kama ilihusika kwa namna yoyote na Owen, na chumba namba 1046. Ila mazingira yao, kwa namna moja ama nyingine, yalitengeneza haja ya kutiliwa ‘tushaka’. Hawakuwa wa kupuuza kwenye upelelezi.
.
.
.
KISA CHA MFANYAKAZI WA JIJI.
.
.
.
Ndani ya usiku huo huo, tukirudi nyuma, kwenye majira ya saa tano usiku, mfanyakazi wa jiji aitwaye Robert Lane alikuwa anaendesha kuelekea katikati ya jiji alipomuona mwanaume mmoja akiwa anakimbia, alikuwa amevalia nguo ya ndani tu.
.
.
.
Alistaajabu kuona hilo jambo kwenye majira ya baridi. Mwanaume huyo alisimamisha gari la Robert na kumuomba ampeleke mahali anapoweza kupata taksi. Robert akakubali kumsaidia. Alikuja kugundua mtu huyo alikuwa ana jeraha kubwa mkononi.
“Unaonekana umetokea kwenye magumu?” Robert aliuliza. Mtu huyo akatikisa kichwa na kisha akanguruma:
“Nitamuua yule **** kesho!”
Walifika mahala panapopatikana taksi, yule mtu akashuka, akachukua taksi na kutokomea.
.
.
.
Robert hakujua kama atakuwa amehusika kwa namna moja ama nyingine kwenye jambo kubwa na la kutisha kama hili.
.
.
.
SASA TURUDI KULE CHUMBANI KUMHUSU OWEN.
.
.
(KINOTI CHA 'DON'T DISTURB MLANGONI)
.
.
.
Kwenye mishale ya saa moja asubuhi, yani kesho yake baada ya mhudumu kuambiwa mataulo hayahitajiki, mfanyakazi wa hoteli anayehusika na mambo ya mawasiliano ya simu aligundua simu ndani ya chumba namba 1046 ilikuwa ipo hewani.
Yaani ilitumika alafu ikaachwa pasipo kukobekwa kwenye kitako chake.
Baada ya masaa matatu kupita bila ya simu kukobekwa kitakoni, akamtuma mhudumu Randolph Propst kwenda kumwambia yeyote aliyekuwepo chumbani akate simu.
.
.
.
Mhudumu akakuta mlango umefungwa, na mlangoni kukiwa kuna note ‘Don’t disturb’ imepachikwa. Akagonga mlango, akasikia sauti inamruhusu aingie ndani, ila alipofungua mlango bado ulikuwa umefungwa.
.
.
.
Akagonga tena, mara hii akasikia sauti ikimuagiza taa ziwashwe. Baada ya kugonga mara kadhaa pasipo matunda, akaamua kufoka:
“Weka simu kwenye kitako chake!” na kisha akaondoka akitikisa kichwa chake.
.
.
.
Lisaa limoja na nusu baadae, mhudumu wa simu akagundua bado simu haijakobekwa kitakoni. Basi akamtuma mhudumu mwingine, Harold Pike, kwenda kuhusika na tatizo hilo.
.
.
.
Harold akakuta mlango bado umefungwa na una kinote cha ‘Don’t disturb’. Basi akatumia passkey kufungulia mlango. Ndani ya kiza, aliweza kugundua kwamba Owen alikuwa amelala juu ya kitanda akiwa uchi. Simu ilikuwa mbali na kikobeko chake, akainyanyua na kuirudisha.
.
.
Kama vile Randolph, Harold akadhani Owen alikuwa amelewa chakari. Akaondoka pasipo kutazama hali ya Owen kwa ukaribu zaidi.
.
.
.
MCHEZO UKAENDELEA...
.
.
.
Muda mfupi mbeleni, kwenye majira ya saa tano asubuhi, mhudumu wa simu wa hoteli akagundua simu ndani ya chumba 1046 ilikuwa nje ya kikobeko chake kwa mara nyingine!
.
.
.
Akamtuma tena Randolph aende akamalize hilo tatizo. Randolph akakuta kinoti cha ‘Don’t disturb’ mlangoni. Akabisha hodi pasipo majibu, akatumia passkey kuzama ndani.
.
.
Mhudumu huyu akagundua jambo kubwa lililomshangaza. Owen, bado akiwa uchi, alikuwa amepiga magoti akishikilia kichwa chake kilichokuwa kimepatakaa damu. Randolph alipowasha taa, akaona damu zaidi ukutani na bafuni.
.
.
Mhudumu huyu, akiwa amejazwa hofu mno, akatoka nje ya chumba haraka na kwenda kutoa taarifa.
.
.
.
OWEN ALIFANYWA NINI?
.
.
.
Maafisa wa polisi walikuja kugundua kwamba masaa sgta ama saba nyuma, kuna mtu alimfanyia kitu kibaya mno Roland Owen. Alikuwa amefungwa na kuchomwa visu mara kadhaa. Fuvu lake la kichwa lilikuwa na ufa kwa kupigwa mno. Shingo yake ilikuwa na mikwaruzo iliyothibitisha kunyongwa.
.
.
.
Damu ilikuwa imetapakaa. Hiki chumba kilikuwa kimegeuzwa chumba cha mateso.
.
.
.
Owen alipoulizwa nini kimetokea, akiwa mdhaifu wa fahamu, akajibu:
“Nilidondokea kwenye sinki la kuogea.”
Ulipofanyika msako ndani ya chumba ikagundulikana hakukuwa na nguo yoyote ile ndani ya chumba 1046. Pia sabuni, shampoo na mataulo hayakuwapo. Kilichopatikana ilikuwa ni tai, sigara ambayo haikuwa imevutwa, alama za damu za vidole kwenye taa, na kibanio cha kike cha nywele.
.
.
.
Mfanyakazi mmoja wa hoteli alisema, masaa kadhaa nyuma kabla ya kuhangaika na Owen, alimuona mwanamke na mwanaume fulani wakiwa wanatoka hotelini haraka. Sasa hakukuwa na shaka kwa wapelelezi kwamba, kulikuwa kuna watu wengine waliojichanganya na hili.
.
.
Wakati Owen akikimbizwa hospitali, akapoteza fahamu kabisa. Alikufa baadae usiku.
.
.
.
SHIDA INAKUJA SASA...
.
.
.
Wapelelezi walikuja kugundua kwamba haya mauaji ya Owen hayakuwa ya kawaida. Polisi wa Los Angeles hawakupata rekodi yoyote ya mtu anayeitwa Roland T Owen, jambo ambalo lilipelekea wakaamini mtu huyu alighushi jina.
.
.
.
Mwili wa Owen ulichukuliwa kutangazwa kwa matumaini kwamba kuna mtu anayeweza kuutambua. Miongoni mwa waliotembelea na kutoa taarifa akawa bwana Robert Lane ambaye alimfananisha kabisa Owen na mtu aliyeonana naye usiku wa mwezi wa kwanza, tarehe 3.
.
.
.
Wahudumu kadhaa wa bar nao pia wakakiri kumuona mwanaume aliyefanana na Owen akiwa ameongozana na wanawake wawili. Polisi pia waligundua kwamba usiku kabla ya Owen kwenda PRESIDENT Hotel, mwanaume anayefanana naye alikaa katika hoteli ya Muehlebach, akijiandikisha kwa jina la Eugene K Scott wa Los Angeles.
.
.
.
Walitafuta pia taarifa kumhusu Eugene K Scott, hawakupata kitu.
Pia hawakupata bahati yoyote ya kumpata ‘Don’, anayetuhumiwa kuwasiliana na Owen kipindi yupo ndani ya hoteli ya PRESIDENT.
.
.
Je, alikuwa ndiye yule mwanaume aliyekuwa na yule mwanamke malaya?
.
.
Je, alikuwa ndiye yule sauti ya kigeni iliyomkataza mhudumu asiingize mataulo?
.
.
Je, alikuwa ndiye yule mwanaume ambaye Owen alimwambia Robert lane kwamba anataka kumuua?
.
.
Maswali yote haya hayajawahi kujibiwa kamwe.
.
.
.
SIKU TISA BAADAE.
.
.
.
.
Siku tisa baada ya “Owen” kufa, promota wa michezo ya mieleka aitwaye Tony Bernardi alimtambua Owen kama mtu aliyemtembelea wiki kadhaa nyuma kujiandikisha kwa ajili ya mechi za mieleka. Bernardi alisema mwanaume huyo alijitambulisha kwa jina la Cecil Werner.
.
.
.
Wakati yote haya kumhusu ‘Roland Owen’ yakiwa bado hayajasaidia kujua haswa uhalisia wake, achilia mbali muuaji. Kile kibanio cha kike cha kubania nywele kinaamsha hoja je mauaji haya yalikuwa ni mchezo wa mapenzi?
.
.
.
Unakumbuka yale maneno ya mwanamke Jean Owen wa chumba namba: 1048 kuhusu kusikia sauti ya mwanaume na mwanamke wakizozana na kufokeana? Mwanamke huyo alikuwa ni nani? Na je alikuwa anazozana na nani? – Owen?
Nadharia hiyo bado imebakia hewani pasipo majibu ya uhakika!
.
.
.
MAZISHI YA ROLAND T OWEN NA KIVULI CHA MUUAJI.
.
.
.
Siku zikiwa zimeenda, na sasa mwezi wa tatu ukiwa mwanzoni, polisi wakaiona hii kesi imeshindikana kuing’amua, hivyo maandalizi ya kumzika Owen yakaanza kufanyika.
.
.
.
Lakini kabla Owen hajapelekwa kwenye makaburi ya jiji, kiongozi wa mazishi akapokea simu kutoka kwa mtu asiyemtambua na ambaye hakujitambulisha.
.
.
.
Mwanaume huyo akaomba mazishi yakawie kidogo mpaka atume pesa ya kuendeshea shughuli hiyo. mpiga simu hiyo akasema jina la Roland T Owen ndilo jina halisi la mtu huyo, na kwamba alikuwa na mahusiano na dada yake.
.
.
.
Zaidi akasema polisi ‘wamepotezwa maboya’. “They are on the wrong track!” kumaanisha muelekeo waliopo si sahihi.
.
.
.
Kweli, muda mfupi pesa ikatumwa kupitia barua pepe maalum ya usafirishaji ‘special delivery mail’ pasipo kujulikana aliyeituma, na Owen akazikwa kwenye makaburi ya Memorial Park. Hakuna yeyote aliyehudhuria, isipokuwa wapelelezi.
.
.
.
Pesa zaidi ikatumwa kwa muuza maua kwa ajili ya maua mengi ya kuweka juu ya kaburi la Owen. Maua hayo yalikuwa na kadi iliyosomeka: “Love forever – Louisie.” (Mapenzi milele – Louisie)
.
.
.
ROLAND T OWEN ANAFAHAMIKA.
.
.
.
Kesi ya Owen ilitupiliwa mbali mpaka mnamo mwaka 1936, ambapo mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Eleanor Ogletree alipoona taarifa za mauaji ya watu kwenye gazeti la ‘American Weekly’.
.
.
.
Eleanor aligundua taarifa za Owen zinarandana kabisa na za kaka yake aliyepotea aitwaye Artemus. Familia yao haijapata kumuona tangu mwezi wa nne mwaka 1934 alipoondoka nyumbani Birmigham, Alabama kwenda matembezi.
.
.
.
Mara ya mwisho mama yake, Ruby, alipata kusikia jambo kutoka kwake kupitia barua tatu fupi, ambazo kwa mujibu wa tarehe, barua ya kwanza aliipokea mwaka 1935 wakati Owen akiwa tayari ameshakufa.
.
.
.
Mama alisema alishangazwa sana na hizo barua kwani alikuwa anafahamu fika kuwa mwanaye hawezi kutype! Miezi kadhaa mbele akapokea simu toka kwa mwanaume aliyejitambulisha kwa jina la Jordan, alimwambia mama kwamba mwanaye amemuokoa maisha yake huko Misri, na kwamba mwanaye ameoana na mwanamke tajiri sana huko Kairo, Misri.
.
.
.
Je, huyu ‘Jordan’ ndiye yule aliyetuma yale maua na pesa za mazishi akidai Owen alikuwa na mahusiano na dada yake?
.
.
.
Sawa, kuhusu kukawia kwa barua twaweza sema ni sababu za kimawasiliano na teknolojia, lakini alikuwa anaziandika nani ilhali Owen alikuwa hajui kutype?
.
.
.
OWEN AMEJULIKANA, NA HAYA JE?
.
.
.
Kwa sasa tumeshamjua Owen kumbe anaitwa Artemus Ogletree, mama yake anathibitisha hilo kwa kuitambua picha ya marehemu, lakini haki kwa kifo chake cha kinyama imeyeyuka. Mpaka sasa kesi hii inaelea elea na imekosa nyama.
.
.
.
- Kwanini Artemus Ogletree alikuwa anatumia majina mbalimbali ya kughushi? Nini alikuwa anaficha na kukikimbia?
.
.
.
- Nani amemuua na kwanini?
Nani huyu anaitwa “Louisie?” – ambaye jinale lipo kwenye kadi ya maua?
.
.
.
- “Jordan” ni nani?
Nani alituma pesa kwa ajili ya mazishi ya Artemus?
.
.
.
- Nani aliyeandika barua kwenda kwa Ruby Ogletree, mamaye Artemus?
.
.
.
- Nini kilitokea ndani ya chumba 1046?
.
.
.
Wataalamu na wapelelezi wamenoa hapa. Vichwa vinawauma kila wanapofungua faili la kesi hii.
.
.
.
Muuaji ni 'Don' hapa wote wanaokena kukubaliana. Ila Don huyu hafahamiki mpaka leo tuongeavyo. Amekuwa ni kivuli kinachoonekana uwepo wake ila hakikamatiki. Nyayo alizoziacha kwenye mawasiliano yake ya kimauaji zimeshindwa kufuatiliwa na kumgundua.
.
.
Kaenda zake!
.
.
.
1491642851350.jpg
Artemus Ogletree (Roland T Owen)
.
.
1491642888914.jpg
Chumba namna 1046 ndani ya hoteli ya PRESIDENT. Artemus alipouawa na saga lake kubaki kizani.
.
.
1491642938309.jpg
Hoteli ya PRESIDENT. Mauaji yalipofanyika.
.
.
1491642972987.jpg

.
.
.
Na SteveMollel
 
MKASA WA MAUAJI YA CHUMBA NAMBA 1046. (KIVULI CHA 'DON' KILICHOWAACHA HOI WAPELELEZI)

1491672435506.jpg
Artemus Ogletree (Roland T Owen)

1491672467067.jpg
chumba namba 1046 alichokaa Artemus Ogletree.

1491672512417.jpg
Hotel PRESIDENT. Mahali ambapo mauaji yalitukia.

1491672546779.jpg
Hoteli ya PRESIDENT.
.
.
.
.
.
.
Na SteveMollel.
 
View attachment 492747 Artemus Ogletree (Roland T Owen)
.
.
View attachment 492748 Chumba namna 1046 ndani ya hoteli ya PRESIDENT. Artemus alipouawa na saga lake kubaki kizani.
.
.
View attachment 492749 Hoteli ya PRESIDENT. Mauaji yalipofanyika.
.
.
View attachment 492750
.
.
.
Na SteveMollel
Hii ntasoma jion nikitulia
 
Back
Top Bottom