Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 34,675
- 40,926
Baada ya kukabwa kila mahali na utendaji mzuri wa Awamu ya Tano, Chadema na Ukawa kwa ujumla wakaamua kuadopt strategy ya kupinga kila kitu.
Mkakati huo wa kupinga kila kitu ulikuja kama namna ya kudhoofisha jitihada za wazi za kurudisha nchi katika mstari na kufisha morali ya Kiongozi mkuu wa Nchi.
Ingawa Chadema na ukawa kwa ujumla wake wanaenjoy mkakati huo, lakini madhara yake ni makubwa kwao na yameshaanza kuonekana taratibu.
Moja ya kiashiria cha kumalizika kwa chadema kutokana na strategy yao hiyo ni matokeo ya hivi karibuni ya Tafiti Ya Taasisi ya Twaweza iliyokuja na majibu kwamba Ushawishi wa Chadema kwa wananchi umepungua na kwa sasa ni chini ya asilimia 17.
Chadema wanaweza kuona kama wanafanikiwa lakini kiuhalisia wanapoteza kundi kubwa sana la watu kwa kasi , kutokana na kujenga taswira hasi mbele ya Jamii, kwani kati ya mambo ambayo yanapokea pingamizi toka Chadema na ukawa ni mambo yasitotaka ubishani kutokana na ukweli kwamba kila binadamu mwenye macho na akili anaweza kuyaona na kuyapima bila kupatiwa ufafanuzi wa yeyote.
Siyo ajabu kabisa, kuendelea kushuhudia kudidimia zaidi kwa chadema na ukawa kwa ujumla kadri utendaji wa serikali unavyokuwa bora na kadri upingaji wa chadema na ukawa unapokuwa mkubwa zaidi.