Mkakati wa kupinga kila kitu unavyoimaliza CHADEMA na UKAWA

stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
20,532
2,000
Baada ya kukabwa kila mahali na utendaji mzuri wa Awamu ya Tano, Chadema na Ukawa kwa ujumla wakaamua kuadopt strategy ya kupinga kila kitu.

Mkakati huo wa kupinga kila kitu ulikuja kama namna ya kudhoofisha jitihada za wazi za kurudisha nchi katika mstari na kufisha morali ya Kiongozi mkuu wa Nchi.

Ingawa Chadema na ukawa kwa ujumla wake wanaenjoy mkakati huo, lakini madhara yake ni makubwa kwao na yameshaanza kuonekana taratibu.

Moja ya kiashiria cha kumalizika kwa chadema kutokana na strategy yao hiyo ni matokeo ya hivi karibuni ya Tafiti Ya Taasisi ya Twaweza iliyokuja na majibu kwamba Ushawishi wa Chadema kwa wananchi umepungua na kwa sasa ni chini ya asilimia 17.

Chadema wanaweza kuona kama wanafanikiwa lakini kiuhalisia wanapoteza kundi kubwa sana la watu kwa kasi , kutokana na kujenga taswira hasi mbele ya Jamii, kwani kati ya mambo ambayo yanapokea pingamizi toka Chadema na ukawa ni mambo yasitotaka ubishani kutokana na ukweli kwamba kila binadamu mwenye macho na akili anaweza kuyaona na kuyapima bila kupatiwa ufafanuzi wa yeyote.

Siyo ajabu kabisa, kuendelea kushuhudia kudidimia zaidi kwa chadema na ukawa kwa ujumla kadri utendaji wa serikali unavyokuwa bora na kadri upingaji wa chadema na ukawa unapokuwa mkubwa zaidi.
 
Mdudu halisi

JF-Expert Member
May 7, 2014
2,730
2,000
Dereva wenu wa Lori atakaporuhusu mikutano ya hadhara ndipo mtakapojua kwamba watanzania wanaupenda muungano wa UKAWA ama la.
 
Malata Junior

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
2,990
2,000
Mkakati wa CCM kuunga mkono kila kitu ndiyo umeifikisha nchi kwenye ufisadi wa kutisha.Serikali inaleta mikataba mibovu bungeni kazi yao ni kugonga meza tu na kupayuka ndiyoooooo! Matokeo yake wanakuja kushtuka nchi imeshaibiwa vya kutosha.
 
chamilo nicolous

JF-Expert Member
Mar 10, 2016
1,463
2,000
mwanasheria wao, anapinga utafiti bila kufanya utafiti, huyu ni msomi wa ajabu sanaaa, lissssuuu sijui kulopoka kumemzidi
 
nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
8,073
2,000
Baada ya kukabwa kila mahali na utendaji mzuri wa Awamu ya Tano, Chadema na Ukawa kwa ujumla wakaamua kuadopt strategy ya kupinga kila kitu.

Mkakati huo wa kupinga kila kitu ulikuja kama namna ya kudhoofisha jitihada za wazi za kurudisha nchi katika mstari na kufisha morali ya Kiongozi mkuu wa Nchi.

Ingawa Chadema na ukawa kwa ujumla wake wanaenjoy mkakati huo, lakini madhara yake ni makubwa kwao na yameshaanza kuonekana taratibu.

Moja ya kiashiria cha kumalizika kwa chadema kutokana na strategy yao hiyo ni matokeo ya hivi karibuni ya Tafiti Ya Taasisi ya Twaweza iliyokuja na majibu kwamba Ushawishi wa Chadema kwa wananchi umepungua na kwa sasa ni chini ya asilimia 17.

Chadema wanaweza kuona kama wanafanikiwa lakini kiuhalisia wanapoteza kundi kubwa sana la watu kwa kasi , kutokana na kujenga taswira hasi mbele ya Jamii, kwani kati ya mambo ambayo yanapokea pingamizi toka Chadema na ukawa ni mambo yasitotaka ubishani kutokana na ukweli kwamba kila binadamu mwenye macho na akili anaweza kuyaona na kuyapima bila kupatiwa ufafanuzi wa yeyote.

Siyo ajabu kabisa, kuendelea kushuhudia kudidimia zaidi kwa chadema na ukawa kwa ujumla kadri utendaji wa serikali unavyokuwa bora na kadri upingaji wa chadema na ukawa unapokuwa mkubwa zaidi.
Ulale panapostahili Deo Filikunjombe
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
30,899
2,000
Mkuu sasa hivi wananchi wamebaki wanalishwa chakula cha aina moja. Bunge live hapana watu wakafanye kazi. Lakini wakati huohuo wa kazi wanajeshi wanapata nyota moja live ikulu, uzinduzi ndege 2 live, sijui ikiwa ndege kumi itakuwa mapumziko ya kitaifa.

Njoo sasa kwenye maisha ya wananchi kuhusu hilo tango pori la uzalendo, sukari bei juu, huduma muhimu bei juu, anayehoji au kupigia kelele hali hiyo anaitwa mchochezi!! Wananchi wanalazimishwa uzalendo fake lakini hawana ruhusa ya kuhoji mapungufu wala kusikia mawazo tofauti. Inatakiwa habari za kusifia tu, habari hasi hata kama ni kweli media inafungiwa!!

Yaani unaingiza timu uwanjani lakini unataka ufunge magoli tu bila mabeki wa timu pinzani kukukaba. Halafu unatoka unajisifu unajua kucheza sana na timu pinzani haina chochote!!!
 
Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,097
2,000
Uzuri mnajitahidi kuficha ficha ila maisha ya wananchi vijijini ndio yanazidi kuwa magumu!
Na sasa hivi mnamalizia kwa mama ntilie kulipa kodi ili nao akili ziwakae sawa!
Tukutane 2020
 
Siyabonga101

JF-Expert Member
Mar 8, 2016
2,430
2,000
Mkuu sasa hivi wananchi wamebaki wanalishwa chakula cha aina moja. Bunge live hapana watu wakafanye kazi. Lakini wakati huohuo wa kazi wanajeshi wanapata nyota moja live ikulu, uzinduzi ndege 2 live, sijui ikiwa ndege kumi itakuwa mapumziko ya kitaifa.

Njoo sasa kwenye maisha ya wananchi kuhusu hilo tango pori la uzalendo, sukari bei juu, huduma muhimu bei juu, anayehoji au kupigia kelele hali hiyo anaitwa mchochezi!! Wananchi wanalazimishwa uzalendo fake lakini hawana ruhusa ya kuhoji mapungufu wala kusikia mawazo tofauti. Inatakiwa habari za kusifia tu, habari hasi hata kama ni kweli media inafungiwa!!

Yaani unaingiza timu uwanjani lakini unataka ufunge magoli tu bila mabeki wa timu pinzani kukukaba. Halafu unatoka unajisifu unajua kucheza sana na timu pinzani haina chochote!!!
Swali la kujiuliza; Ni Mwenyekiti wa Chama gani yuko IKULU. Ilani ya Chama gani inayoongoza Halmashauri hapa nchini? Ukipata majibu hayo itakusaidia kupunguza mihemko na kulialia mkuu. Karibu tambi na tende.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
30,899
2,000
Swali la kujiuliza; Ni Mwenyekiti wa Chama gani yuko IKULU. Ilani ya Chama gani inayoongoza Halmashauri hapa nchini? Ukipata majibu hayo itakusaidia kupunguza mihemko na kulialia mkuu. Karibu tambi na tende.
Mkuu nashukuru kwa kuniquote lakini huna hoja.
 
rasilimali watu

JF-Expert Member
Apr 20, 2017
261
250
sasa chadema limekuwa danguro la watetea bangi na wauza unga, mafisadi na wafanyakazi hewa na bado wanasubiri 2020 ....labda watapindua nchi ila si kwa kusubiri kula za wananchi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom