Mkakati wa kuing'oa C.W.T

Mkakati wa kuing'oa C.W.T

Licha ya CWT kuwa na madhaifu kibao, usitarajie hao viongozi wanaweza support Chama kikiwa stable. Wao wanapenda wawaburuze wafanyakazi bila kelele za chama. Hiyo ni nature, kwa uelewa wao wanatamani kusiwe na vyama bila kujua kuwa vina msaada kwao pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa
Kwanini iwe kampeni hapo kilichopo ni hizo tuhuma na kile wanachotakiwa kukifahamu hawa wagombea kwamba wanatakiwa kwenda kudeal na kero gani ambazo zina trend kwenye vichwa vya wanachama wao na cvinginevyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
mbona wanasema wanataka kuing'oa. Mimi nilidhani wanaing'oa halafu kuwe hakuna chama walimu walipwe walichoibiwa. Sasa kama hiyo siyo kampeni nini hicho??
 
Hakuna
Hakuna mwalimu anaeweza kutetea haki ya mwalimu mwenzake, hii imeshathibitika! Wote hao wanatafuta kutetea matumbo yao na jamaa zao
Asantee sanaaa hawa jamaa wapo Kwa matumbo yao tuu

Sent by IPhone
 
#NIMEITOA_KWENYE_GROUP_MOJA_HUKO.

MKAKATI WA KUIN'GOA CWT KISHERIA NA KUWARUDISHIA WALIMU PESA ZAO WALIZOIBIWA NA CWT PAMOJA NA FIDIA

Nimepitia mijadala mingi na malalamiko mengi ya WALIMU dhidi ya CWT, Hotuba ya Rais Magufuli na Mkuu wa Wilaya wa Hai dhidi ya madudu ya CWT.

Nashauri,CWT nigenge la ajabu na Haliwezi kukoma kuwepo bila ya KUTUMIA njia ya Mahakama.

Ni Mahakama pekee ndio inaweza kumkomboa Mwalimu hivyo nashauri tufungue kesi ya kudai yafuatayo (briefly)

1. Viongozi wa CWT watupatie majina ya WALIMU waanzilishi wa CWT pamoja na nakala ya CERTIFICATE OF REGISTRATION-sababu ni haki ya WALIMU kupatiwa

2. CWT watupatie nakala ya "Authorized Budjet"ya miaka mitano-kama sheria inavyoelekeza kuwa Mwalimu anatakiwa apate nakala hizo for five years consecutively if needed. Authorised Budget ndio document inayotakiwa kuonyesha mapato na matumizi,kiasi cha pesa kilichopo,assets, liabilities,idadi ya wanachama, wafanyakazi, budget ya mishahara, idadi ya walimu wanaokatwa agency fees, kodi zinazolipwa, n.k

3.C WT watupatie "company profile" ya Tanzania Teachers Development Co.Ltd (TDCL) Kampuni hii ndio inayomiliki shares katika BENKI YA WALIMU, na pia inamiliki vitega uchumi. Ukienda kwenye soko la hisa Dar es Salaam utaijua zaidi.

4. CWT watupatie taarifa ya kesi aliyofungua mama Hellen Mbezi na wakili Tarimo dhidi yao pale MCA mwaka 2013. Kesi hii ni muhimu sana kwa mstakabali wa maisha ya MWALIMU Tanzania, but it was cooked behind teachers ignorance.

5. Ufafanuzi wa kisheria juu ya application of the law of agency fees in Tanzania, sababu walimu wamekua wakiibiwa kwa kutumia misapplications.

6. CWT watupatie Anual Financial Reports za Mwalimu Bank maana ni haki ya wanahisa.

7.CWT watupe maelezo ya kisheria yanayoonyesha Walimu ndio wamiliki wa MWALIMU BANK,na nafasi ya walimu katika maamuzi ya Benki hiyo

8. CWT watueleze iwapo wao ni trade union au professional body ya walimu, ili kuondoa utata uliopo kwenye documents zao, wanazijua hizi.

9. CWT wamekuwa wakipokea zaidi ya DOLA ELFU 90 KILA MWAKA kutoka Denmark kwaajili ya kusaidia WALIMU "professional awareness", watuonyeshe mchanganuo wa pesa hizi--wao wanazijua walianza kuzivuna ruzuku hizi mwaka 1998.

10. CWT watupe majibu ya AUDITING ILIYOFANYWA NA PROFESA ASSAD MWAKA 2017

11. TUMTAKE MSAJILI wa vyama Tanzania Mama Uisso atueleze kwanini hajakifuta chama cha CWT mpaka sasa wakati HAWAJAWAHI kutoa "Authorised Budget" kama inavyoelekeza na sheria, na yeye kapewa kazi yakuvifuta vyama visivyofata sheria.

HAYO NI MACHACHE TU..MWALIMU HAWEZI KUJIBIWA HAYA BILA KUTUMIA MAHAKAMA ILIYO HURU NA HAKI,it is very wrong and falacy to take these things easy !!

NASHAURI KUUNDA TIMU YA WANASHERIA ILI KUDAI HAYA. NA GHARAMA YAKE TUNAWEZA KUTUMIA MILIONI 50, yaani kila Mwalimu achangie Shilingi 500/=, walimu laki moja wanatosha.

TOA MAONI YAKO!

Imeandikwa na Farai Alfred



Sent using Jamii Forums mobile app
Ha ha ha
1. Chama cha waalimu ni chama peke yake cha wafanyakazi kilichoweza kuunganisha wenye taaluma hiyo kwa mapana yake nchi nzima. Hakuna chama kilichofaniliwa hivyo. Mfano madaktari wana vyama vingi hivyo rahisi kugawanyika
2. Hakuna chama hapa tz ambacho kimewatetea wanachama wake kama CWT
3. CWT ndio chama ambacho hata serikali ilikuwa anapay high attention
4. CWT postive implication zake zilifika mpaka kwa wasio wanachama wake. Kwa mfana nakumbuke mwaka 2000 CWT ilitishia mgomo nchi nzima kama serikali isipolipa walimu uhamisho, likizo nk. Serikali iliamua kulipa kwa wote waliokuwa wanadai hata wasio waalimu.
Nimecheka kwa sababu wajanja wamefanikiwa kuifanyisha makosa ili kuibua hasira, kutoridhishwa na ugomvi ya wanachama wake, hatimaye kukiua. Hii inafanana na ujanja uliotumika kuisambaratisha chama cha siasa cha NCCR miaka iliyopita.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CWT Ni janga la taifa y aani faida yake uwepo wake Ni sawa na kutokuwepo. Mi naona kuwa na chama kimoja Cha wafanyakazi HIVI CWT WILAYA NA KATIBU WAKE WANAKAZI GANI? MNATAFUTIA NDUGU ZENU AJIRA KISA HELA YA MWALIMU HAINA MWENYEWE. AUDIT REPORT SIJAWAHI IONA . HUU NI UJAMBAZI NA UHUNI KAMA WENGINE
 
Karibia viongozi wore waandamizi (kuanzia ngazi ya wilaya) ni wana CCM damu damu.
Nimeweka neo 'karibia' makusudi ikimaanisha >99%.
Naamini nimeeleweka.
 
REFORMATION NI MUHIMU CWT


Wiki Jana 15 may 2020 kulikuwa na uchaguzi wa viongozi cwt ngazi ya wilaya shinyanga DC
Kwakweli CWT kimekuwa siyo chama Cha kutetea maslahi ya walimu Bali ni cha wachumia tumbo kutokana na mchakato wako ulivyoendeshwa! It's shame! U haguzi uliojaa rushwa, uchaguzi ambao uongozi uliokuwepo ulipanga Nani awe kiongozi wa chama hicho, haiwezekani viongozi wa CWT waandae malazi ya wapiga kura, chakula, vinywaji for 2 days , hivi unataraji tutapata viongozi wazuri katika chama hiki?

CWT shinyanga dc ni uozo mtupu, haijawahi kushuhudiwa Hali hii, baada ya uchaguzi Kuna kiongozi aligombea nafasi ya mkoa na kwa njia ileile aliyotumia alishinda lakini nafasi ya ngazi ya wilaya tayari aliandaliwa mtu ambaye kamati imekubaliana awe huyo headmaster wa shule Fulani, je, tutafika,
CWT ni jipu linalosubiri kutumbuliwa , na mtumbuaji ni mkuu wa nchi.

Cwt wanagawa t-shirt siku 10 baada ya sherehe za Mei mosi? Hii syndicate ya baadhi ya watu, na kwa manufaa yao ya kulindana ili kuchumia tumbo




Sent using Jamii Forums mobile app
 
CWT Ina katiba na namna ya kutoa maoni ili yawasilishwe na kujadiliwa katika mkutano mkuu,sidhani kama Kuna mwalimu aliewahi fanya hili,zaidi mkiona uchaguzi wagombea mnafanya ajenda kupondana ili kupata nafasi afu mnasahau ahadi zenu zote

Pigeni kampeni kistaarabu walimu acheni kujidhalilisha,mapungufu yote hayo hamyaoni Hadi wakati wa uchaguzi?!?!?
 
Mwakilishi wa shule moja ya msingi aliandikiwa barua ya kutenguliwa kushiriki mkutano mkuu kwa kukosa sifa siku 1 kabla ya uchaguzi CWT shy DC na hii ilitokana na mwakilishi huyu kuwa na msimamo thabiti alipoambiwa awasilishe salary slip 3 na barua iliyoandikwa kwake ni kupitia kwa mkuu wa shule ambapo ni kinyume na katiba , pia mkuu wa shule aliteua mwakilishi mwingine kinyume na katiba
Hivyo uchaguzi kukiukwa kwa kiwango Cha hali ya juu,

Mwakilishi huyo alirusha barua hiyo kwenye group Fulani la WhatsApp na ndipo taarifa hii ilipothibitika na huu ni uonevu mkubwa, kwani anastahili kulipwa stahiki zake Kama mwakilishi halali, pili mwakilishi aliyeteuliwa. Na mkuu wa shule alipiga kura kinyume na katiba inayotaka mwakilishi achaguliwe na wanachama katika kituo Cha kazi
Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CWT Ina katiba na namna ya kutoa maoni ili yawasilishwe na kujadiliwa katika mkutano mkuu,sidhani kama Kuna mwalimu aliewahi fanya hili,zaidi mkiona uchaguzi wagombea mnafanya ajenda kupondana ili kupata nafasi afu mnasahau ahadi zenu zote

Pigeni kampeni kistaarabu walimu acheni kujidhalilisha,mapungufu yote hayo hamyaoni Hadi wakati wa uchaguzi?!?!?
Hiki ndicho kipindi cha watu kutoa ya moyoni na hakuna anayejua nani atakuwa kiongozi hvyo wagombea wanatakiwa wachukue hili kama changamoto kli wajue oa kuanzia....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau mwenye fomu ya kujitoa CWT na kujiunga chama kingine anitumie tafadhali
 
Back
Top Bottom