Mjumbe wa NEC ya CCM akamatwa kwa ujangili

Mjumbe wa NEC ya CCM akamatwa kwa ujangili

Spanishboy

Senior Member
Joined
Apr 24, 2011
Posts
118
Reaction score
65
OPERESHENI Okoa Maliasili inayoendelea Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma imemkumba Mjumbe wa mkutano Mkuu wa CCM taifa (Mnek) Sultani Ajili Kalolo na kuhojiwa kwa zaidi ya Masaa 8 kwa tuhuma za kushiriki katika vitendo vya ujangili wa Tembo.

Tukio la kukamatwa kwa Mneki huyo lilitokea Oktoba 13 mwaka huu huku Wilaya hiyo ikiwa na kumbukumbu ya kukamatwa kwa Bunduki zaidi ya 300 na Risasi 667 katika oparesheni hiyo ya okoa maliasili iliyobatizwa jina la "wazee wa tinted".

Katika tukio hilo Mjumbe huyo wa mkutano Mkuu wa CCM taifa (Mnek) Ajili Kalolo alikamatwa akiwa Nyumbani kwake eneo la Shule ya msingi Muungano majira ya asubuhi na ilipofika saa 12 jioni Kikosi kinachosimamia operesheni hiyo kiliwaruhusu ndugu zake kumdhamini kwa masharti ya kwenda kuripoti kituo cha Polisi Jumatano ya wiki hii.

Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusdedith Nsimeki pamoja na kudai kuwa yeye siyo msemaji wa Operesheni hiyo Iakini alikiri kuwepo kwa tukio hilo la kukamatwa kwa Kalolo na kuongeza kuwa watu wanaokamatwa ni waliohusika katika matukio ya ujangili pamoja na madalali wa biashara ya meno ya Tembo.

"unajua mimi siyo msemaji wa Operesheni hiyo, lakini ninazo taarifa za Kushikiliwa kwa muda kwa kiongozi huyo wa ngazi za juu katika Chama cha Mapinduzi" alisema Kamanda Nsimeki na Kuongeza kuwa hali hiyo imetokana na Kiongozi huyo kutanjwa kuwa ni miongoni mwa Majangili wa Tembo.

"opereshini hii inatekelezwa kisheria, hivyo haiwezi kumuonea aibu kiongozi ama mtu maarufu" alisema kamanda Nsimeki na kuongeza kuwa watu wote wanaokamatwa ni wale wanaotajwa kuwa miongoni mwa wahusika wa namna moja na matukio na vitendo vya kijangili hivyo operesheni hiyo haitawaonea watu wasio husika.

Kamanda Nsimeki aliendelea kueleza kuwa Operesheni hiyo iliyopewa jina la okoa maliasili inayoendelea Wilayani Tunduru, Mkoani Ruvuma pia inaendelea katika Wilaya ya Namtumbo katika Kijiji cha Likusenkuse na Lipalamba Wilayani Mbingalengo likiwa ni kukomesha vitendo vya ujangili wa Tembo na maliasili nyingine za Tanzania.

Alisema Operesheni hiyo inayo husisha Vyombo mbalimbali vya Majeshi ya nchi yetu, wamo pia Askari wa jeshi la wananchi wa Tanzani, Usalama wa taifa, Uhamiaji na Polisi ambao kwa pamoja wanapitia taarifa mbalimbali na kuwakamata watu wote ambao wamekuwa wakitajwa kujihushisha na matukio ya ujangili.

credit: Tabianchi blog
 
Atahojiwa central ipi? Na nani?

Kwa kweli katiba mpya lazima kuwe na kipengele cha kukamata wezi wa mali za umma kama hawa watu. It hurts jambazi anakula nchi na kupewa heshima kwa wizi aliokuwa anaoufanya huku bado anatukejeli tu. Yaani Kikwete kwa usanii bwana, baada ya kuona Kinana alikuwa anaiba maliasili akamtoa kwa hasira na haibu, kwa adhabu kampa ukatibu mkuu wa CCM ili awe anaeneza sifa za chama na kumsifia Kikwete.
 
...mwenye mtandao mbona wanamuacha ...
 
Jeshi la Polisi limemtia mbaroni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Aggrey Kalolo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Deusidedit Nsimeki, alithibitisha kukamatwa kwa Kalolo kuhusiana na tuhuma za ujangili, lakini amekataa kueleza kwa undani tukio hilo kwa maelezo kuwa kuwa lipo kwenye kampeni maaalum ya kitaifa na kwamba alikamatwa siku kadhaa zilizopita.

CHANZO: NIPASHE
 
NDANI YA UTAWALA WA CCM HAKUNA WA KUMKAMATA MWENZAKE MAANA ALIYEKABIDHIWA CHAMA MTENDAJI MKUU WOTE TUNATAMBUA NI PRINCIPAL DENTIST...hawa wadogo ni associates tu..JADI HAIPOTEI HATA KWA KITUKUU Kitakapozaliwa...CCM NI MAAFA....ni MAJANGA!!
 
Akikamatwa Abdutembo Kindovu nitaridhika!! hao ni watumishi wake tu!!
 
NDANI YA UTAWALA WA CCM HAKUNA WA KUMKAMATA MWENZAKE MAANA ALIYEKABIDHIWA CHAMA MTENDAJI MKUU WOTE TUNATAMBUA NI PRINCIPAL DENTIST...hawa wadogo ni associates tu..JADI HAIPOTEI HATA KWA KITUKUU Kitakapozaliwa...CCM NI MAAFA....ni MAJANGA!![/QUOTE

HAHAHAHA ETI CHIEF DENTIST...SI UMALIZIE TU CHIEF DENTIST OF ELEPHANTS
 
NDANI YA UTAWALA WA CCM HAKUNA WA KUMKAMATA MWENZAKE MAANA ALIYEKABIDHIWA CHAMA MTENDAJI MKUU WOTE TUNATAMBUA NI PRINCIPAL DENTIST...hawa wadogo ni associates tu..JADI HAIPOTEI HATA KWA KITUKUU Kitakapozaliwa...CCM NI MAAFA....ni MAJANGA!!
Ukoo wa kambale, kila mmoja ana ndevu
 
Back
Top Bottom