Kimsingi CCM ilishakufa, inasubiri kuzikwa. Tatizo nani wa kuizika? Hapo ndipo wananchi wanapochanganyikiwa hawaoni mbadala wanalazimika kuendelea na ccm. Nashauri vyama vya siasa vitulie vijiangalie vina mapungufu wapi vijirekebishe visahihishe makosa.Chonde chonde vyama vya siasa msiwachukie watu wanaowasema vibaya hao ndio watu wazuri kwenu kwani wanawaonyesha mnapokosea msipowasikiliza mnapotea. Sio vizuri kumsikiliza sana yule anayekusifia kwa muda mwingi huyu anakudanganya kwani wewe siyo malaika hata usifanye makosa !!!