Mjumbe tume ya Nchimbi aibiwa Guest | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjumbe tume ya Nchimbi aibiwa Guest

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by TIQO, Sep 14, 2012.

 1. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Kamati hiyo iliyofika Iringa kwaajili ya kufanya uchunguzi kuhusiana na kesi ya mauaji ya Mwandishi wa Habari wa channell ten na Mwenyekiti klabu ya waandishi wa habari Iringa iliyokuwa imefikia katika hotel moja mkoa wa Iringa. Wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kuibiwa Ipad na kiasi cha fedha Tsh laki 700.
  Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo mmoja Kati ya wajumbe wa tume hiyo ameamka na kujikuta mtupu Bila ya Ipad yake yenye nyaraka nyeti za kumwezesha kufanya uchunguzi huo kuibwa.
  Chanzo cha taarifa hizi kinaeleza kuwa katika hoteli hiyo kuwa alikuwepo mpangaji katika chumba cha jirani ambaye alikuwa na master keys zilizoweza kufungua mlango huo na kuiba vitu hivyo.
  Inadaiwa kuwa Kamati hiyo pamoja na kuundwa na waziri mwenye dhamana ya mambo ya ndani ya nchi ila bado imekuwa ikifanya kazi katika mazingira hatari zaidi baada ya kuwepo kwa habari kuwa imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu zaidi na makachero wa polisi.
  Hata hivyo habari Kutoka ndani ya jeshi la polisi ambazo zinafanyiwa kazi na jeshi la Polisi mkoani Iringa zinadai kuwa Kamati hiyo iliondoka asubuhi ya jana kuelekea Nyololo kuanza kufanya kazi yake ya kiuchunguzi kuhusiana na tukio hilo la mauji ya mwandishi yaliyotokea mnamo tarehe 2 September mwaka huu.

  Source; Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima
   
Loading...