Mjue Simba

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249
Mwenye nguvu mpishe.

1. Simba ndiye paka mkubwa kuliko wanyama wote wa jamii ya paka na simba wa afrika wamekuwa maarufu kwa jinsi ya umoja, upendo na mshikamano wao na huishi kwa pamoja kwenye kundi la misifa na kundi moja la simba wanakadiriwa kuwa kati ya simba 10-40 wakiongozwa na mfalme wao.

2. Simba dume ndiye mlinzi wa kambi iluhali majike ndio wasakanyaji wa chakula (wawindaji) licha ya hayo, simba dume ndio wa kwanza kula na kwa wastani madume yanakula sana kuliko majike

3. Simba ni mmoja wa wanyama walio katika orodha ya hatari ya kutoweka kabisa duniani kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhifadhi IUCN

4. Simba wa kwanza walipatikana Afrika (sio Kenya), asia na Ulaya lakini yasemakana kwa sasa simba walio katika mazingira Afrika wanapatikana Afrika tu (sio Kenya) kweingineko wanaishia kuwaangalia simba kwenye mizingo yao wanyama (ZOO).

5. Ngurumo za simba zinafika/sikika umbali wa kilomita nane na daima atembeapo visigino vyake havigusi ardhi.

6. Simba wana uwezo wa kukimbia umbali wa mile 50/saa na kuruka futi hadi 36.

7. Simba hulala masaa 20 kwa siku na hasa anapokua ameshiba. Simba huishi kwa wastani wa miaka 10-14 mwituni, huku katika hifadhi huweza hata kufika zaidi ya miaka 20.

8. Simba mkubwa hula mara moja tu kwa wiki wastani wa kilo 20-35 za nyama kwa mlo mmoja kutegemeana.

9. Ingawa simba hujulikana kama mfalme wa pori, simba wengi huishi kwenye nyasi tu na hupenda sana nyasi kavu na ndefu (ellephant grassland), hata rangi ya simba huakisi rangi ya nyasi kama mbinu ya mawindo ubabe wa simba una wapinzani pia kama tembo (ingawa meno ya mbwa hayaumani)

10. Simba dume anafikia urefu wa mwili pamoja na kichwa wa sentimita 170 hadi 250; kimo cha mbegani ni 120 cm. Dume mkubwa anaweza kuwa na uzito wa kilogramu 225. Jike ni mdogo wake akiwa na urefu wa 140 hadi 175 cm, kimo cha mbegani cha 100 cm na uzito wa 150 kg. Simba dume anatofautishwa kirahisi kutokana na manyoya marefu ya shingoni ilhali jike hana.

Ila yote hapo juu hayahusiani kabisa na simba SSC ya Tanzania tafadhali

lion_running.jpg
 
Attachments

  • lion_running.jpg
    lion_running.jpg
    31.4 KB · Views: 132
Hapo namba sita kwenye uwezo wa kukimbia, nadhani kuna kukosea, unamaanisha mita 50/saa, au km 50/saa?
 
Bujibuji...............namanisha jump/leap kama una kiswahili fasaha hapo tafadhali

...........
leap
lēp/
verb
gerund or present participle: leaping
  1. jump or spring a long way, to a great height, or with great force.
    "I leaped across the threshold"
    synonyms: jump over, jump, vault over, vault, spring over, bound over, hop (over),hurdle, leapfrog, clear
    "he leaped over the gate"
    • move quickly and suddenly.
      "Polly leapt to her feet"
      synonyms: spring, jump, jump up, hop, bound
      "Claudia leapt to her feet"
    • jump across or over.
      "a coyote leaped the fence"
      synonyms: jump over, jump, vault over, vault, spring over, bound over, hop (over),hurdle, leapfrog, clear
      "he leaped over the gate"
 
Nimekuelewa vizuri mkuu..ila kuna sehemu nadhani haujagusia maisha ya simba dume maana huwa naona kuna umri ukifika anazingirwa na simba dume kadhaa kumuua au mmoja tuu ili apate ufalme wa kumiliki familia ndio maana yeye simba dume anaua simba dume watoto akijua wakikua watamdhuru.. Simba anapigwa na nyati dume vizuri tuu mpaka kufa..
 
Nimetafuta...nimekosa! hujasema kitu kuhusu simba kuwa na hirizi, ambayo tunaambiwa kabla hajala huwa anaitema, akimaliza kula anaimeza hirizi yake! Na kwamba hiyo hirizi ni dili sana kuipata!
 
ni kweli yapo mengi kuhusu simba na mbabe mwingine wa simba ni mbwa mwitu ambao hufanya timing ya kuwaua simba ili kupunguza ubabe na ku create spheres kwa mbwa mwitu ........asante kwa nyongeza
 
huyu mtoa mada ni yule afande sele wa morogoro?
maana jamaa nae anampenda simba kweli
 
Nimetafuta...nimekosa! hujasema kitu kuhusu simba kuwa na hirizi, ambayo tunaambiwa kabla hajala huwa anaitema, akimaliza kula anaimeza hirizi yake! Na kwamba hiyo hirizi ni dili sana kuipata!
si kabla hajala ni kabla hajalala...........imani hiyo imekita sana miongo mwa morani wa kimasa kwamba ukiipata unakua na nguvu kama simba na hata sauti yako ina unguruma kama simba ukiongea ila ni imani tu mkuu haipo hiyo utakuja hata na tochi humu
 
Nimetafuta...nimekosa! hujasema kitu kuhusu simba kuwa na hirizi, ambayo tunaambiwa kabla hajala huwa anaitema, akimaliza kula anaimeza hirizi yake! Na kwamba hiyo hirizi ni dili sana kuipata!
mada kama hii ililetawa humu

jamani kuna habari kwamba simba ana Hilizi, na kama ukimuua simba na ukiweza kuipata hiyo IRIZI than ukaimeza ni kwamba utakua na nguvu kama simba na utaweza kupambana na watu 40 ukiwa mikono mitupu yaani bila silaha. inasemekana kipindi cha nyuma MORANI wa kimasai walimeza sana hizi irizi ndio maana waliweza kupambana na simba na wakashinda. mwenye taarifa zaidi karibu

majibu

Simba hana hirizi ila huwa anacheua sana akitaka kufa. Anakuwa anatema mate kama anacheua.

Simba akitaka kunywa maji kuna kitu anatoa mdomoni kama size ya ndimu ni kiduchu lakini Sio sana hua Ndio ki Nacho msaidia kutoa sauti, akimaliza anakimeza tena, Sasa sijui kama Ndio hicho kukipata Sio kazi ndogo...

Hiyo kitu haipo ni uzushi tu japo Babu yangu alishawahi kunionesha na sikuiamini.
Na ile kitu si kwamba ukiimeza ndo unakua na nguvu kama simba, bali inasemekana unakuwa unaogopwa na watu kama jinsi simba alivyo kule mwituni.
Jinsi ilivyo ni kama nyasi laini sana zilizocheuliwa. Ni ya kijani na hata ukitafuna radha yake ni material ya nyasi.
Msipotoshwe na waganga.

Story za kishirikina katika zama hizi za sayansi na teknolojia hazina nafasi....na ndio maana ndugu zetu walemavu wa ngozi wanazidi kuangamia kwa sababu ya imani hiz
 
Nimetafuta...nimekosa! hujasema kitu kuhusu simba kuwa na hirizi, ambayo tunaambiwa kabla hajala huwa anaitema, akimaliza kula anaimeza hirizi yake! Na kwamba hiyo hirizi ni dili sana kuipata!
Bado tu unaamini katika ushirikina
 
Naona ugomvi na jirani zenu wanafiki umekomaa.

Eti wanapatikana afrika ila sio kenya.
 
Back
Top Bottom