Mjue Peter Mollel Gumbo aka Pierre Konki Mzee wa Liquid ambaye wengi hawafahamu vizuri

Halafu huyo piere ana bahati sna muacheni atusue tu alishaanguka na ghorofa keko kutoka ghorofa ya 5 kashuka nalo mpaka chini na hakuchunika hotel ilikuwa inaitwa chang'ombe village wala hajaruka alikuwa floor ya juu kabisa.
4415CC56-4B4D-452E-97B1-08CC116119F9.jpeg
si huyu?
 
Huyo ni fundi seremala mzuri tu...anachonga fenicha vizuri sana maeneo ya Keko maghorofani hapo.

Siku ya kudondoka kwa iliyokuwa Chang'ombe Village (sasa National Hotel), Peter alikuwa ndani ya jengo akirekebisha moja ya milango ya vyumba vya hoteli ghorofa ya tano..

Vigae vilivyoezekea hoteli vilianza kudondoka kimoja kimoja na jengo kuanza kucheza ndipo yeye aliruka kutoka ghorofa ya 5 kupitia dirishani...alitua salama juu ya kifusi cha mchanga!

Kimo chake kilimsaidia hakuumia hata chembe kwani 'centre of gravity' yake iko chini kama ya mtoto!





Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma humu nimeona namna gani baadhi ya watz wanajidai wajuaji kumbe ni hopeless kabisa. Dunia ya sasa kutengeneza pesa ni first priority na how hapa ndio waafrika bado tumelala. Somo la marketing ni muhimu kwa wengi humu.
 
Jamaa ni fundi Selemara huyo na sio mzululaji.
Jioni ndio unaweza kumkuta pale Sigara au Giraffe au Liquid akipumzika baada ya kazi za mchana kutwa.
Mimi namfaham kabla hajadondoka na gholofa la Chang'ombe Village.
Alipata tenda ya kufunga milango kwenye hilo gholofa.
Msidhanie hana fani na kuwa ni Mlevi tu.
Huyo ni Star
Msimchukulie Poa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha...ha...ha
Ni kweli, ukikaa na huyu mjamaa ni tabasamu tu. Ukimwangalia unaflahi, hiyo ni fani pia.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndiyo hivyo mkuu, kuna kitu pia ukikaa naye au ulimwangalia unaweza kujifunza.

He is very positive, anayafurahia maisha yake tu, hana taarifa na mtu.

Na nzuri zaidi anafanya watu wanaomwangalia wapate furaha, na haigizi, inatokea moyoni kabisa.
 
Kila mtu ana talanta yake! Haiwezekani wote wakawa wasanii, ma professor, doctor nk. Hata Yule aliyeokoa mtoto ufaransa ghafla alikuwa maarufu na akapata uraia wa ufaransa. Kila mtu ana namna yake ya kutokea!
 
Back
Top Bottom