Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,535
MHANGA WA KUJICHOMA MOTO HADI KUFA (SELF-IMMOLATION)
Tangu kuzaliwa kwa dola za kisiasa, historia ya Ulimwengu imerekodi kumbukumbu chungutele za mbinu anuai ambazo wananchi wamezitumia kukabiliana na watawala manyang’au, katili na wasiojali maslahi yao. Wapo waliofanya migomo, maandamano na mapinduzi ya kuzing’oa tawala za kifashisti. Wapo pia waliofanya migomo ya kula, kutumia sanduku la kura na harakati nyinginezo kupinga sera kandamizi.
Katika njia zote ambazo historia imerekodi, mhanga wa kujichoma moto hadi kufa (Self-immolation) ndiyo harakati inayoonekana kuwa ngumu na inayogusa hisia zaidi kuliko zote. Katika Self-immolation, mtu anayepinga sera fulani hujichoma moto hadharani (mala nyingi kwa kutumia mafuta ).
Licha ya kufungamanishwa na historia ya kale ya Uhindu, tukio la kwanza la Self-immolation lililopata umaarufu duniani kote lilitokea nchini Vietnam mwaka 1963 ambapo mtawa wa kibudha, Quang Duc alipojichoma moto hadi kufa katikati ya mtaa wenye watu wengi wa Saigon ili kupinga vitendo vya ukandamizwaji wa watu wenye imani ya kibudha wakati wa utawala wa Ngo Dinh Diem.(Tazama picha ya kwanza).
Mwandishi wa kimarekani aliyeshuhudia kujichoma kwa Quang Duc aliripoti
‘’..Miale ya moto ilivuma kutoka katika mwili wa binadamu huku mwili wake ukiisha taratibu na kichwa chake kuwa cheusi. Eneo zima lilitawaliwa na harufu ya nyama ya binadamu inayoungua. Nyuma yangu nilisikia mayowe ya wa-vietnam walioanza kukusanyika kwa wingi(lakini walizuiwa kumuokoa Quang Duc na watawa wengine wa kibudha waliokuwepo eneo hilo). Nilitunduwaa kwa mshangao nisijue kama nilie, kuchukua habari au kuuliza maswali..nilishindwa hata kuwaza..(kwa namna ya kustaajabisha), alivyoendelea kuungua, hakuinua mwili wala kutoa kilio..’’
Akizungumzia tukio hilo, rais J.F.Kennedy ambaye serikali yake ilikuwa mdhamini mkuu wa serikali ya Diem alisema kwa huzuni..’’Hakuna habari picha ambayo imegusa hisia za watu duniani kama hii’’. Tukio la kujichoma moto kwa Quang Duc lilimlazimisha Rais Diem kukaa mezani na viongozi wa kibudha kutafuta suluhu.
Baada ya tukio la Quang Duc, utaratibu wa kujichoma moto kupinga ukandamizaji ukashika kasi sehemu nyingine za Ulaya Mashariki, Uarabuni na nchi nyingine za Asia. Kumbukumbu ya karibuni zaidi ni ya ‘’Mmachinga’’ wa Kitunisia aliyeamua kujichoma moto hadi kufa baada ya kunyanyaswa na kupokonywa biashara yake na polisi. Tukio hilo lilikoleza chuki za wananchi dhidi ya serikali ya Beni Ali na vuguvugu lilipokuwa kali, aliachia ngazi. Upepo wa mabadiliko ukashika kasi hadi nchi nyingine za kiarabu na kusababisha kile kilichoitwa ‘’Arab Spring’’.
PICHANI
1. Mtawa wa Kibudha Quang Duc akijichoma moto hadi kufa katika mitaa ya mji wa Saigon, Vietnam.
2. Moyo wa Quang Duc ambao haukuungua ukiwa umehifadhiwa kwenye makumbusho.
3. Ryszard Siwiec akijichoma moto kupinga uvamizi wa Soviet nchini Czechoslovakia. Tukio lake lilifanyika uwanjani na kutazamwa na watu zaidi ya 100000. Japo wanausalama walifanikiwa kuzima moto, alifariki akiwa hospitali.
4. Maandamano nchini Ufaransa kumuunga mkono Mohamed Bouazizi , mmachinga aliyejichoma moto kupinga ukandamizaji wa wanausalama wa Tunisia.
Cc : Mpalestina Mchizi