Mjue Mtemi Mkwawa wa uhehe na Wahehe

Kuna haja, tena haja kubwa sana!!! Ya kurejea historia ya taifa letu... labda tutajirudi ustaarabu wa kusaidiana, kuheshimiana na kuepuka choyo, chuki, ufisadi nk.
Tena kama movie industry ya Tanzania ikaamua kushirikiana na watafiti wa Historia ili kutengeneza movie za hawa wababe wa miaka ile waliokataa hbari za kuuza utu na heshima yao kwa the so called investors. Waliofanya hata kama ilikuwa kipindi chao yanastahili heshima kubwa mpaka leo hii.
 
Yale mafuvu 83 yaliyobakia ndo inakuwaje? Ngoja niende Bremen Museum kuwauliza.
Isike naye alijilipua. Ile yeye ni baruti nadhani hawakupata kitu. Kinjiketile ilikuwaje? Kaburi lake lipo?

Kuna mdau naye ameuliza hilo swali kihivi "And if this is a historical fact, why did we reclaim only Mkwawa’s skull? What about the others?" baada ya kupata taarifa hii:

I was able to get the reference given by Allen Roberts about Chief
Mkwawa'a skull. The story is hallowing, indeed. The Germans had 2000
skulls of colonial/conquered people at the Bremen Museum . They were all
arranged by cephalic order. Out of this collection there were besides
Mkwawa's, 82 skulls from German East Africa (modern Tanzania ).

According to Edgar Winans, the person who severed Mkwawa's head did so
in order to collect the monetary reward which the Germans had announced
for his capture before he committed suicide. Von Prince, the Commanding
Officer at Iringa, kept the head as a souvenir but later sent it to
Germany , apparently for unknown reasons.

Be that as it may, the massive collection of skulls collected by the
Germans demands some explanation. There must have been some policy in
place that encouraged this kind of enterprise in the conquered
territories.


Chanzo: H-AFRICA@H-NET.MSU.EDU
 
Zitto muulizie na huyo Dinosari wetu wa Tendaguru ambaye anawaingizia Wajerumani mamilioni ya fedha za Kitalii. Karl Lyimo anashauri tusidai arudishwe Tanzania maana hatutamtunza vizuri ila tudai tuwe tunagawana mapato nao. Vyovyote vila ni wetu!
 
According to Edgar Winans, the person who severed Mkwawa's head did so
in order to collect the monetary reward which the Germans had announced
for his capture before he committed suicide. Von Prince, the Commanding
Officer at Iringa, kept the head as a souvenir but later sent it to
Germany , apparently for unknown reasons.

Be that as it may, the massive collection of skulls collected by the
Germans demands some explanation. There must have been some policy in
place that encouraged this kind of enterprise in the conquered
territories.

Chanzo: H-AFRICA@H-NET.MSU.EDU

Serikali yetu ya sasa inaweza kutusaidia ili tuwaelewe Wajerumani.
La sivyo ni sahihi kabisa sisi kudai hawa jamaa kuomba radhi kwa vitendo vilivyodhalilisha utu wa binadamu na watawala wetu wa wakati huo.
Ubalozi wa Ujerumani upo hapa, ni vyema tukapata maoni yao.
 
hii thread imeniweka kichwa fresh sana juu ya askari wetu huyu alikua kamanda mzuri sana sio kama makamanda wetu wa sasa
 
Historia ni tamu sana. Nimesoma Tosamaganga na nimekwenda sana Kalenga. Ninapata hisia kali sana ninaposoma historia hii.

Ushujaa huu wa kina Mkwawa umepotelea wapi?

Mkuu zitto ushujaa upo ila tu watz bado tunalindana, we ngoja tu utaona moto wake siku si nyingi, Kina ngosha wameanza, wapole watanashati lkn moto wake si kitoto....CDM juuuu
 
Mkwawa au kwa jina defu Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga (1855 – 19 Julai 1898[SUP]1[/SUP]) alikuwa chifu na kiongozi mkuu wa Wahehe katika Tanzania wakati wa upanuzi wa ukoloni wa Ujerumani wakati wa mwisho wa karne ya 19. Mkwawa aliongoza upinzani wa Wahehe dhidi ya Wajerumani.

Upanuzi wa Wahehe


Jina la Mkwawa ni kifupi cha Mukwava ambalo ni kifupi cha Mukwavinyika iliyokuwa jina lake la heshima likimaanisha "kiongozi aliyetwaa nchi nyingi". Mkwawa alizaliwa mnamo mwaka 1855 mahali palipoitwa Luhotakaribu na Iringa mjini. Alikuwa mtoto wa chifu Munyigumba aliyeaga dunia mwaka 1879.
Babake Munyingumba aliwahi kuunganisha temi ndogo za Wahehe na makabila ya majirani kuwa dola moja. Aliiga mfumo wa kijeshi wa Wasangu waliowahi kuwa kabila lenye nguvu waliowahi kujifunza mfumo huu kutoka Wangoni na impi za Shaka Zulu. Hadi miaka ya 1870 eneo la Wahehe ilipanushwa mbali kuanzia kusini hadi katikati ya Tanzania ya leo.
Baada ya kifo cha chifu mzee watoto walishindana kati yao juu ya urithi wake huku mpwa wa Mkwa bwana Mwambambe Mwalunyungu aliyekuwa msaidizi na wa karibu wa Mnyigumba akikalia utawala huo kwa mabavu,
Msuguano huo ulimfanya Mkwawa kuitoroka Iringa na kwenda uhamishoni Morogoro ambako alikaa kwa takribani miaka miwili na kuhamia Mpwapwa Dodoma. Hali ya utawala wa Mwambambe Mwalunyungu haikuwavutia wazee wa kihehe ambapo waliandaa uasisi na wakatuma mmoja wa askari aende Mpwapwa akanuite Mkwawa arudi kuchukua himaya.
Jambo hilo lilimfanya mkwawa aingiwe na hofu kuwa angeuawa na Mwambambe, lakini wazee walimhakikishia kuwa watamuunga mkono, kweli Mkwawa alirudi na vita ikaanza ambapo katika mapigano askari wa Mwambambe walikuwa wakiasi kadiri mapigano yalivyosonga, na baadae Mwambambe akakimbia nakujificha kwenye kichaka kiitwacho (lugegele)
Ikumbukwe kuwa Mwambambe alikuwa na uwezo wa kudaka mkuki inayomlenga zaidi ya kumi, hivyo kila askari wakijaribu kumcho na mkuki alikuwa akidaka na kuwaua askari hao na mkuki huohuo, mwisho askari mmoja aliyeitwa Mwakilufi, aliushika mkuki nakujaribu kama anajichoma vile kisha akaufyatua kwa spidi ya hali ya juu na ukampata kifuani na kutokeza mgongoni Mwambmabe,
Hakika ilikuwa ni vita ya kimizimu, baada ya hapo Mwambe aliongea maneno haya "Be mnyakilambo, ndakulile kiki pe ukumbulaga de?" (kijana nilikulia nini unaponiua hivi?) Yule askari Mwakilufu alijibu, "Walye nda unoge be" (ulikula hivyohivyo bwana)
Baada ya kumuua Mwambambe walimla nyama pale pale tena mbichi, Mkwawa alimwambia yule askari atambe kidogo kuonyesha ujasiri wake, hapo yule askali akaanza, vava mwakilufi,vasengidunda,vamaseto,vamwalumato, vamwaluhala, vamwamyinga, vasemdapo, vamwamgimwa, vamwachalamila, vamwachavala, vamwamalangalila, nk
Sasa Mkwawa akawa ameshinda na akawa kiongozi mpya wa Wahehe. Aliendelea kupanusha utawala wake. Hadi mwisho wa miaka ya 1880 alitawala sehemu muhimu za njia ya misafara kati ya pwani na Ziwa Tanganyika. Misafara hii iliyobeba bidhaa za nje kama kitambaa, visu na silaha kutoka pwani ikirudi na watumwa na pembe za ndovu ilipaswa kumlipia hongo ikanunua pia wafungwa wa vita zake. Hapo athiri na uwezo wake wa kulipa jeshi kubwa ikapanuka.
Mkwawa na upanuzi wa Wajerumani

Tangu miaka ya 1885 Wajerumani walianza kuunda koloni yao katika Tanzania bara. Mwaka 1888/89 utawala wao ulitikisihwa na vita ya Abushiri lakini baada ya kushinda upinzani wa Waafrika wa pwani Wajerumani walilenga kuimarisha utawala wao juu ya sehemu za bara.
Mkwawa aliwahi kusikia mapema habari za Wajerumani akajaribu kuwasiliana nao lakini bila kuelewana. Aliamua kujenga boma imara lenye kuta za mawe kwenye makao makuu yake huko Kalenga karibu na Iringa. Katika mwezi wa Februari 1891 alituma wajumbe kwa kambi la Wajerumani huko Mpwawa wakapokelewa na gavana Mjerumani. Wakati huohuo Mkwawa aliendelea kutuma askari zake hadi Usagara iliyotazamiwa na Wajerumani kama eneo lao. [SUP][1][/SUP] Katika kipindi hiki gavana mpya Julius von Soden alifika Dar es Salaam. Hakuwa na mamlaka juu ya mkuu mpya wa jeshi Emil von Zelewski aliyepokea amri zake kutoka Berlin moja kwa moja. Baada ya kusikia habari za mashambulio ya Mkwawa katika Usangara aliomba na kupata kibali cha "kuwaadhibu Wahehe".
Mapigano ya Lugalo

Katika mwezi wa Julai 1891 von Zelewski aliongoza kikosi cha maafisa Wajerumani 13 na askari Waafrika hasa kutoka Sudan 320, pamoja na wapagaji 113. Walikuwa na bunduki za kisasa, bunduki za mtombo na mizinga midogo. Zelewski aliwadharau Wahehe kama washenzi ambao walikuwa na mikuki na pinde tu. Kwa hiyo hakuuona haja ya kutuma wapelelezi wa awali. Njiani aliangamiza vijiji alivyokuta na katika mwezi wa Agosti alipoona Wahehe 3 waliomkaribia aliagiza kuwaua bila kuongea nao. Kumbe walikuwa mabalozi wa Mkwawa aliyetaka kujadiliana na Wajerumani.
Tarehe 17 Agosti 1891 Zelewski na jeshi lake walipita kwenye manyasi marefu karibu na Lugalo. Mkwawa alikuwa alimsububiri na Wahehe 3,000 walionyamaza hadi Wajerumani waliotembea kwa umbo la safu ndefu walikuwa karibu kabisa wakawashambulia. Wajerumani walikosa muda kuandaa silaha zao wakashtushwa kabisa. Sehemu kubwa ya askari waliuawa katika muda wa dakika chache pamoja na jemadari von Zelewski. Sehemu ya kombania ya nyuma ilirudi nyuma na kusimama kwenye kilimo kidogo walipoweza kutumia bunduki la mtombo wakajitetea na kuua Wahehe wengi. Sehemu hii ilijumlisha maafisa 2 na maafande 2 Wajerumani waliweza kukimbia na kujiokoa pamoja na askari 62 na wapagaji 74.
Kipindi cha vita dogo

Baada ya mapigano Mkwawa alihesabu wafu wake waliokuwa wengi. Alikataza bada za kilio kwa sababu alitaka kuficha idadi ya askari waliokufa. Akaelewa sasa ya kwamba silaha za Wazungu zilikuwa hatari alituma tena mabalozi kwa gavana von Soden walioeleza ya kwamba Wahehe walikuwa walijitetea tu dhidi ya shambulio walitaka amani. Lakini madai ya Wajerumani yalikuwa magumu eti kuwaruhusu wafanyabiashara kupita bila matata na kutoshambulia majirani tena.
Mkwawa hakuwa tayari kuahidi yote akachelewesha mikutano. Wakati huu kamanda mpya Mjerumani Tom von Prince alijenga boma jipya la Wajerumani katika Uhehe na Mkwawa alijibu kwa kusambulia vikosi vidogo vya jeshi la kikoloni. Gavana Soden alidai kutoendelea na mapigano. [SUP][2][/SUP]. 1893 gavana von Soden aliondoka Afrika na gavana mpya von Schele alitaka kulipiza kisasi akaamuru mashambulio dhidi ya Mkwawa.
Anguko la Kalenga

Mwezi wa Oktoba 1894 von Schele aliongoza kikosi cha maafisa Wajerumani 33 na askari Waafrika pamoja na wagajai zaidi ya 1000 kuelekea Kalenga. Walikuwa na mizinga 4 na bunduki bombomu. Walipofika mbele ya Kalenga Wahehe walijisikia salama kutokana na kuta imara lakini Wajerumani walijipanga kilomita kadhaa nje ya mji wakaanza kufyatulia mizinga yao na kuua watu ndani ya mji. Wakati wa giza kwenye asubuhi wa 30 Oktoba 1894 askari wa jeshi la Schutztruppe walipanda ukuta katika sehemu ulipodhoofishwa tayari na kuingia mjini. Hadi jioni walikuwa waliteka mji wote. Gombora na mikuki ya Wahehe hazikuweza kushindana na bombomu za Wajerumani. Mkwawa mwenyewe aliamua kukimbia pamoja na 2000 – 3000 askari lakini kabla ya kukimbia alimwua mganga mzee aliyewahi kutabiri ya kwamba atawashinda Wajerumani waliokuja. Gavana von Schele aliandika taarifa kwa serikali ya Ujerumani "tulizika maadui 250, wengine walichomwa katika nyumba zao, wanawake na watoto 1500 kutekwa nyara" [SUP][3][/SUP].
Mkwawa alijificha msituni pamoja na askari zake akasubiri. Gavana von Schele alishindwa kuendelea na mashambulio wa sababu gharama za vita zilishinda makaisio yake na wabunge wa upinzani katika Reichstag huko Berlin walipinga vita ya kikoloni; walikataa kuongeza makisio na kiongozi wa wasoshalisti August Bebel aliita mtindo wa kuchoma mji na kuteka nyara watoto na wanawake "ushenzi mkuu".
Amani fupi

Baada ya kuondoka kwa Wajerumani Mkwawa aliweza kurudi na kujenga tena nyumba mahali pa Kalenga. Katika Septemba 1895 Mkwawa alikuwa tayari kujadiliana na Wajerumani na tar 12 Oktoba walipatana amani. Wajerumani walimkubali Mkwawa kama chifu wa Wahehe , Wahehe waliahidi kukabidhi gobori zote, kuonyesha bendera ya Kijerumani na kuwaruhusu wafanyabiashara na wasafiri kupita Uhehe. Mkwawa alimwagiza mjomba wake kutia sahihi akakataa mwenyewe akisema hii ingemwua. Hata hivyo miezi kadhaa baadaye alitafuta msaada wa Wajerumani kwa shambulio dhidi ya Wabena.
Afisa mmoja Mjerumani aliyefika Kalenga mpya alizuiliwa kuingia na kumwona chifu akaambiwa alipe hongo ya bundiki 5 wa kuingia katika eneo la Mkwawa. Hapo maafisa wa jeshi la Wajerumani waliolinda mpaka ambao bado walitafuta nafasi ya kulipiza kisasi kwa Lugalo waliamua chifu alivunja mkataba. Kapteni Tom von Prince alijenga boma jipya karibu na Kalenga alianza kuwasiliana na machifu wadogo wa Wahehe. Mkwawa alijaribu kujenga mapatano na majirani lakini Wabena na makabila mengine walikumbuka vita na mashambulio ya awali kutoka Uhehe walipendelea kushikamana na Wajerumani. Mkwawa aliwaua machifu wawili wahehe waliowahi kukaa na von Prince lakini aliona hawakuwa wa pekee waliosita kumtii tena. Alipata habari ya kwamba mdogo wake Mpangile alishikamana na Wajerumani. Wakati wa Septemba 1896 Wahehe waligawanyika na sehemu kubwa ya viongozi waliochoka vita ilikuwa tayari kuwakubali Wajerumani.[SUP][4][/SUP]. Wajerumani waligawa eneo lao. Wasangu walirudishwa katika eneo lao la awali wakarudi kutoka Usafwa katika mji mkuu wa Utengule Usangu. Mpangile alisimikwa kama kiongozi mpya wa Uhehe penyewe lakini baaa ya siku 50 alisimamishwa na kuuwa na Wajerumani waliomshtaki eti anamsaidia kakaye kisiri.
Mafichoni na kifo

Mkwawa alikuwa aliondoka sehemu za Iringa mwezi wa Agosti 1896 alipoona mgawanyiko. Alifuata mwendo wa mto Ruaha akilindwa na wenyeji waliokuwa tayari kumficha na na kumlinda dhidi ya vikosi vya Wajerumani waliomtafuta. Disemba 1896 alihamia milima ya Uzungwa alipojificha. Kutoka hapa alitelemka mara kwa mara kwenye mabonde alipopata vyakula na kushambulia vikosi vidogo vya askari vya Kijerumani.
Katika Julai 1897 kikosi kikubwa cha Wasangu pamoja na Wahehe chini ya uongozi wa Wajerumani walikuta kambi la Mkwawa mlimani wakashambulia lakini Mkwawa aliweza kukimbia. Mwaka 1898 Mkwawa aliendelea kujificha kwenye misitu akiongozana na watu wachache sana. Aliishi hasa kwa njia ya kuwinda. Wakati wa Julai 1898 aliongozana na wavulana 4 pekee halafu Wazungwa 2 mume na mke. Tarehe Julai 16 Wajeumani waliowahi kusikia habari zake walimkuta huyu mama Mzungwa alipotafuta chakula wakamkamata akawaambia Mkwawa alielekea kusini na alifika sehemu inaitwa Mrambarasi.. Wakamfuata na tar 18 Julai Mkwawa alimwua mume Mzungwa kwa hofu ya kusalitiwa. Aliendelea na wavulana 2 tu walioitwa Musigombo na Lifumika. Watoto waliogopa angeweza kuwaua pia. Hapo Lifumika aliamua kukimbia asubuhi ya tar 19 Julai. Lakini siku ileile alipotelemka kutoka mlimani alikutana na kikosi cha Wajerumani akakimbia lakini wakamshika wakamlazimisha kuwaambia habari za Mkwawa. Kijana alimwambia sajenti Mjerumani kuwa chifu alikaa mgonjwa mahali kwa umbali wa masaa 3.
Walimlazimisha kuwaongoza. Njiani walisikia kwa mbali sauti ya bunduki, risasi 1. Wakaendelea na baada ya masaa mawili walikuta maiti za Mkwawa na kijajana mwingine. Inaonekana waliwahi kujiua na sauti ya bunduki ilikuwa Mkwawa aliyejipigia risasi.[SUP][5][/SUP]
Fuvu la Mkwawa

Kichwa cha mtemi kinasemekana kilikatwa na Wajerumani na kutumwa Berlin kilipohifadhiwa katika makumbusho, awali Berlin na baadaye Bremen.
Waingereza waliochukua utawala wa koloni mwaka 1918 baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia walitaka kuonekana kama mabwana wema. Mkuu wa serikali ya kikoloni ya Tanganyika alipendekeza kurudisha fuvu kwa sababu Wahehe walishirikiana na Waingereza wakati wa vita. Hivyo kuna kipengele 246 katika mkataba wa Versailles kinachosema: "Katika muda wa miezi 6 baada ya kuthebitishwa kwa mkataba huu … Ujerumani itakabidhi fuvu ya Sultani Mkwawa iliyohamishwa kutoka Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na kupelekwa Ujerumani kwa serikali ya Mfalme wa Uingereza."
Wajerumani walikataa habari za fuvu hii na Waingereza waliamua ya kwamba ilishindikana kuikuta. Lakini baada ya vita kuu ya pili ambako Ujerumani penyewe ilivamiwa na wanajeshi wa Uingereza gavana Twining wa Tanganyika alikumbuka habari za fuvu akatembelea Ujerumani na kutazama mafuvu ya makumbusho ya Bremen.Katika mkusanyiko wa fuvu 2000 zilikuwa 84 zenye namba zilizoonyesha zilitoka kiasili katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hapa alizipanga kufuatana na ukubwa na kutazama zile zilizokuwa na vipimo vya karibu na ndugu za Mkwawa aliowahi kupima kabla ya safari yake. Hapa aliteua fuvu yenye shimo kwa sababu taarifa ya kale ilisema Mkwawa alijiua kwa kujipigia risasi kichwani.
Fuvu hii ilipelekwa Tanganyika tarehe 9 Julai 1954 na kuhifadhiwa katika jengo la makumbusho ya Mkwawa kwenye kijiji cha Kalenga
Marejeo
0. Kitabu kiitwacho Mtemi Mkwawa na wahehe. kiliandikwa na Wiliam Malangalila

  1. ↑ John Iliffe, A modern history of Tanganyika, 1979, uk 108
  2. ↑ Iliffe uk. 109-110
  3. ↑ David Pizzo, "To devour the land of Mkwawa": Colonial violence and the German-Hehe War in East Africa, 2007, uk 173
  4. ↑ John Iliffe, A modern history of Tanganyika, 1979, uk 113 / 114
  5. ↑ John Iliffe, A modern history of Tanganyika, 1979, uk 115 /116
 
Ha ha ha ha ha ha Mkwavinyika....Muhehe akupenda kutawaliwa!kaka Yericko unaweza nitumia kwa inbox?
 
Yericko Nyerere

Nataka kujua wanyakyusa walitoka wapi na kwanini wanyakyusa hawana chifu wa aina ya Mkwawa katika historia ya makabila ya Tanzania? Halafu haya majina ya mwalunyungu mwambambe mbona kama ya kinyakyusa? hivi nani aliyeanza kuwepo maana naona mkwawa alikua na himaya kubwa mpaka mbeya inakuwaje hapo wanajamvi?
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: tz1
Hayo majina si ya Kinyakyusa ni ya kihehe...wahehe wana "prefix" ktk majina yao ya ukoo ktk kutambulisha "masculine gender na femine gender"....kwa wanaume majina ya ukoo htanguliwa na "Mwa" wakati wanawake htanguliwa na "Se".....e.g Mgimwa: Mwamgimwa & Semgimwa.....(2)Mgulunde...Mwamgulunde & Semgulunde....(3)Kivike....Mwakivike & Sekivike...(4)Ng'ingo....Mwang'ingo....Seng'ingo (5)Mtema...Semtema....Mwamtema e.t.c ...Wakati Wanyakyusa hawana iyo,Mhehe anayeitwa Kivike unaweza kumuita pia Mwakivike,lakini Mnyakyusa anaitwa Mwakyembe huwez kumwita "Kyembe"...halafu ukøo wa Mnyakyusa anayeitwa Mwakatobe ipo hivo kwa mwanamke na Mwanamume e.g Jimmy Mwakatobe na Jesca Mwakatobe,wakati kwa Muhehe ukoo wa MPONZI(Mfanö) itakuwa Jimmy MWAmponzi na Jesca SEmponzi
 
Mkuu Yeriko...habari hii ni kweli ila imepotoshwa kwa upande aliofia...hakufia milima ya udzungwa...aliufata mto ruaha kuelekea magharibi mwa Iringa, alifika sehemu inaitwa Mrambarasi.. sehemu hiyo kulikuwa na jiwe kubwa na ndani kuna pango hapo alikuwa na vijana uliowataja pamoja na kijana mwingine anaitwa MUSATIMA ambaye alikuwa amemkimbia padri kule Tosamaganga baada ya kumbatiza na kumwita MUSA...Sehemu hiyo mpaka leo kuna kaburi lake na mwaka 1998 hayati baba wa Taifa na spika wa kwanza wa Tanzania hayati Adam Sapi Mkwawa walilitembelea kaburi la mzalendo huyu baada ya kutimiza miaka 100..
 
Kwa kweli mahali alipofia bado panaleta kitendawili...lakn ukiwa mdadisi kwa wazee wanakwambia Mkwawa hakuwah kupatikana ima yu hai au amekufa!inasemwa na Wazee kuwa baada ya kuwa ile "Lipuli" yake imevamiwa Kalenga ye alipasua Mbuga,akapita magharibi ya Iringa ya leo ambapo zamani ndo ilikuwa BOMA la Mjerumani(ndo mana Muhehe leo akikwambia "ndibita kuboma= nakwenda mjini) akambaa mpaka Milima ya Nduli na kuibukia maeneo ya Uzungwa sehemu za Mapanda....mtu mmoja alikuwa anaitwa Mwambata ndo alikuwa anampelekea Ng'ombe kwa ajili ya nyama,badae Wajerumani wakagundua,wakamkamata Mwambata na kumwambia awapeleke alipo Mkwawa akakataa katakata,wakamkamata na kumnyönga hadharani sehemu inayofahamika mpaka leo kama Kitanzini(iliyoendelea kutumika kunyongea wapinzani wa Utawala wa Wajeruamani).Kumbe alipojua Mjerumani kateka hìmaya yake alitoka na askari wawili na kumua mmöja ambapo Wajeruman walikuja kujua n "Mkwawa" na kwa kuwavùnja ngùvu Wahehe walitangaza kwa ngûvu kuwa Mkwawa kafa ili watawalike kwa urahìsi....ikumbukwe kuwa sehemu kubwa ya hìstoria imeandikwa na wazungu kuna vitu wali-skip ili kutomkweza Mwafrika
 
Mkuu Yeriko...habari hii ni kweli ila imepotoshwa kwa upande aliofia...hakufia milima ya udzungwa...aliufata mto ruaha kuelekea magharibi mwa Iringa, alifika sehemu inaitwa Mrambarasi.. sehemu hiyo kulikuwa na jiwe kubwa na ndani kuna pango hapo alikuwa na vijana uliowataja pamoja na kijana mwingine anaitwa MUSATIMA ambaye alikuwa amemkimbia padri kule Tosamaganga baada ya kumbatiza na kumwita MUSA...Sehemu hiyo mpaka leo kuna kaburi lake na mwaka 1998 hayati baba wa Taifa na spika wa kwanza wa Tanzania hayati Adam Sapi Mkwawa walilitembelea kaburi la mzalendo huyu baada ya kutimiza miaka 100..
Asante mkuu kwa kunikumbusha, imenilazimu kuhariri historia hii kule Wikipedia nimeona wamekosea sana
 
Jamaa alijitumbukiza mtoni na mwili wake haukupatikana,inasemekana kile kichwa walichokata wajerumani sio cha mkwawa ila ni cha askari wake!
 
Yale mafuvu 83 yaliyobakia ndo inakuwaje? Ngoja niende Bremen Museum kuwauliza.
Isike naye alijilipua. Ile yeye ni baruti nadhani hawakupata kitu. Kinjiketile ilikuwaje? Kaburi lake lipo?

Mkuu vp matokeo ya Bremen Museum walisemaje? Tafadhali lets share
 
Pamoja na kuwa na uwezo mkubwa wa kivita mtwa Mkwawa alikuwa ni mwanadiplomasia hodari,kabla ya kupambambana na wajerumani alituma wajumbe watatu in response julai 30 1891 wajerumani waliwaua wajumbe wale watatu na kuchoma moto vijiji,zaidi na hapo ni chifu mkwawa aliyejaribu kuwashawishi watala wa kingoni na kinyamwezi kuunganisha nguvu ili kupambana na wajerumani,kwa bahati mbaya hili halikufanikiwa,vp kama lingefanikiwa? ni wazi wajerumani wangepata upinzani mkubwa kabla hata ya vita vya majimaji.NI HAKI KUJIVUNIA SHUJAA HUYU.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom