Mjue mbilia bel

Mjue mbilia bel

ashomile

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
2,915
Reaction score
2,981
MJUE MBILIA BEL

Mbilia Bel (Mbilia Mboyo, Marie-Claire), Marie Claire Mbilia Mboy, maarufu kama Mbilia Bel alizaliwa jijini Kinshasa, tarehe 14 Agosti, 1959 au Januari 10, 1959 tatizo linakuja kwa kuwa tarehe zote hizo mbili zimewahi kutajwa na yeye mwenyewe Mbilia. Mwaka 1977, akiwa na umri wa miaka 17 aliacha shule na kujiunga na kundi la mwanamke muimbaji maarufu wakati huo Abeti Masikini akiwa kama mcheza show. Baada ya miaka minne katika kundi hili alijiunga na Sam Mangwana katika maonyesho mbalimbali nchini Kongo, mwishoni mwa mwaka 1981 aliweza kufanyiwa usaili na Tabu Ley na siku hiyohiyo kuajiriwa katika kundi la Afrisa International na ndipo alipopewa jina la Mbilia Bel.

Mbilia alikuwa mzuri wa sura na umbo na sauti yake ya juu ‘soprano’ iliwezesha kundi la Afrisa kuanza kupata umaarufu mpya, wimbo wake wa kwanza ‘Mpeye ya Longo’ ambao tafsiri yake ni Roho Mtakatifu uliorekodiwa 1982 ulikuwa ukieleza kuhusu shida anazopata mwanamke aliyeachwa katika ndoa, na ulipendwa sana na wanawake wa Kongo wakati huo. Wimbo huo uliotungwa na Tabu Ley ulipendwa zaidi kwa kuwa ulikuwa unaimba matatizo ya mwanamke na ulikuwa unaimbwa na mwanamke, hatimae wimbo huo ulishinda tuzo la wimbo bora Zaire wa 1983, pia Mbilia akashinda tuzo la msanii mpya bora. Katika kipindi kile tasnia ya muziki wa Kongo ilikuwa ikitawaliwa na wanaume watupu kwa hiyo wimbo huo ulikuwa ufunguo kwa waimbaji wa kike wa Kongo na hatimae hata waimbaji wa kike hata hapa kwetu Tanzania. Kibao kilichofuata kilikuwa ni “Eswi yo Wapi” (Uliumizwa wapi?), huu ulikuwa wimbo ambao Mbilia na Tabu Ley walitunga kwa pamoja nao ukwa maarufu sana, kutoka na kuwepo kwa Mbilia umaarufu wa Afrisa ulikuendelea kukua na kuanza kuvunja ngome kongwe ya TP OK Jazz katika mauzo na umaarufu. Maonyesho ya Afrisa yalijaza sana na kivutio kikubwa kilikuwa Mbilia ambaye alikuwa anajua kulitawala jukwaa na mara nyingi alijiunga na na wacheza show wa Afrisa walioitwa Rocherreautes kutokana na jina la Tabu Ley Rochereau, na kucheza vizuri kazi ambayo ndio aliyoanzia katika ulimwengu wa muziki. Nyimbo kama “Mobali na ngai wana”, ambao unaweza kuutafsiri kama Mume wangu huyu, ambao ulitungwa na Tabu Ley na Roger Ezidi, ulitokana na wimbo asili wa Kikongo. Katika wimbo huu Mbilia alikuwa anamsifu mumewe kuwa mzuri na mwenye uwezo lakini pamoja na yote kamchagua yeye.
mbilia-bel-rfi.jpg
 
Nina Santuri mbili za Mbilia Bel akiwa na Afrisa International
 
Asante sana mtoa post, kwa uzi mzuri wa kutukumbusha juu Mwanamuziki Nguli Mbilia Bel. Mimi nilikuwa nakosea kumbe !!, nilikuwa nadhani ni Mbili Abeli.
 
Back
Top Bottom