Mjue boomslang, Nyoka hatari sana wa kijani

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
22,856
Reaction score
32,659
Nyoka wa Boomslang anajulikana kwa sumu yake kali sana, inayojumuisha hemotoxins ambazo huzuia damu isiweze kuganda. Kung'atwa na nyoka huyu kunaweza kusababisha kupasuka kwa mishipa ya damu hivyo kusababiasha damu kuvuja ndani na nje ya mwili, na damu inaweza kutoka sehemu zote za mwil zenye uwazi mfano pua, fizi, na mashimo mengine ya mwili.

Licha ya kuwa boomslang ni mdogo na kuwa na tabia ya kuwa aibu, boomslang ni mmoja wa nyoka hatari zaidi kwa sababu ya athari zake kama matibabu yatachelewa inaweza kusababisha kifo kutokana na sumu yake.

**************

The boomslang snake is known for its highly toxic venom, which contains hemotoxins that prevent blood from clotting. A bite from this snake can cause internal and external bleeding, with blood potentially oozing from the nose, gums, and other body openings.
Despite its small size and shy nature, the boomslang is one of the most dangerous snakes due to the delayed yet deadly effects of its venom.

Nyoka hawa wa kijani hupatikani ukanda wa RUNGWE, mwakaleli sana ....japo ni mara chache kusikia wameng'ata watu .....labda umkanyage .....hutimua mbio sana
1749597980170.jpg

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
hawa nyoka ni wambea wambea wanakaa sana juu ya miti mmekaa zenu chini utashangaa kitu tiii, na kukiwa a mziki ndio kabisaaaaa
Unaemzungumza wewe ni green mamba (koboko wa kijani)..

Samahani kuna mtu yeyote anajua dawa ya black mamba(koboko mweusi)
 
Huyo mshikaji koboko anazingua, ana sumu kali, mkionana kwa macho tu anakukimbilia, huwez kimbia ukamuacha, akidonoa yaani ni kichwani tu,
"YAANI NI MAJANGA JUU YA MATATIZO"
Sio kweli. Moja ya nyoka mpole na mstaarabu ni black mamba(koboko).
Mara ya mwisho kumuona live ni Oktoba 2024 njiani. Mara baada ya kumuona nilisimama umbali wa mita 7 au 8 hivi. Kuonesha sio mshari,alikaa kwa takribani dakika 5 akiwa ametulia palepale. Kisha baadae alianza kuondoka taratibu.

Pia,kwa sie wakulima wa tumbaku tunakutana nao mara nyingi sana kwenye mabani ya kuchomea tumbaku kwani sehemu hizo zinakua na utulivu hasa nyakati za kiangazi na pia ni mawindo yao ya mijusi na panya. Zoezi la ukataji kuni za kuchomea tumbaku nalo hutukutanisha na nyoka huyu hatari kwani hupendelea kuishi kwenye miti mikubwa yenye mapango.

Nyoka hatari ambaye mkionana tu huanza kutengeneza mashambulizi ni Cobra (swila) ambaye ni mweusi. Yeye akikuona hata kama ni nyoka mdogo lazima kwanza ainue kichwa,mdomo wake hutanuka na kuanza mashambulizi kwa kutema mate.

Utofauti wa cobra na black mamba (swila na koboko) ni kua, swila ni mweusi na mkorofi hata usipomchokoza ,pia sumu yake si kali sana kama ya koboko. Lakini koboko yeye mara nyingi ni mtaratibu,ila ukimchokoza balaa lake sio la kitoto. Anakimbia mno, sumu kali sana ambayo inadaiwa kuua binadamu chini ya dakika 20 endapo atachelewa kituo cha afya. Black mamba hua na rangi ya kijivu au kijani. Anaitwa black mamba sio kwa kwasababu ya rangi yake,bali rangi ya mdomoni mwake ndio nyeusi.
 
Mapondo Mapoka ongea yote kuhusu koboko lakini huwezi kunishawishi lolote kwamba koboko mpole labda wa huko kwenu..huyu mwamba hapana aisee..
nliwahi kushuhudia timbwili lake hata mm nilinusuruka, sina hamu nayo..
ni nyoka mwenye akili kuliko nyoka wake..ni mpole kama hamjaonana naye macho kwa macho!
Ni HOSPITALI GANI HYO AMBAYO HAPA TANZANIA INA DAWA LA KUTIBU MADHARA YA SUMU ZA KOBOKO?
 
Huyu nyoka ni mwamba kweli, ndio maana sio rahisi kuonekana hovyo. Kuna aina mbili za koboko,black mamba na greeni mamba. Yawezekana ambaye tunamuona ukanda wetu ni either green au black mamba. Ila marafiki nyingi huku huyu nyoka ukimuona na ukamchokoza hua ni mkorofi sana. Ukiwahishwa kituo cha afya angalau unaweza kusogeza masaa ya kuishi. Kupona ni nadra sana labda kwa waganga wa tiba za asili.
 
Sio kweli. Moja ya nyoka mpole na mstaarabu ni black mamba(koboko).
Mara ya mwisho kumuona live ni Oktoba 2024 njiani. Mara baada ya kumuona nilisimama umbali wa mita 7 au 8 hivi. Kuonesha sio mshari,alikaa kwa takribani dakika 5 akiwa ametulia palepale. Kisha baadae alianza kuondoka taratibu.

Pia,kwa sie wakulima wa tumbaku tunakutana nao mara nyingi sana kwenye mabani ya kuchomea tumbaku kwani sehemu hizo zinakua na utulivu hasa nyakati za kiangazi na pia ni mawindo yao ya mijusi na panya. Zoezi la ukataji kuni za kuchomea tumbaku nalo hutukutanisha na nyoka huyu hatari kwani hupendelea kuishi kwenye miti mikubwa yenye mapango.

Nyoka hatari ambaye mkionana tu huanza kutengeneza mashambulizi ni Cobra (swila) ambaye ni mweusi. Yeye akikuona hata kama ni nyoka mdogo lazima kwanza ainue kichwa,mdomo wake hutanuka na kuanza mashambulizi kwa kutema mate.

Utofauti wa cobra na black mamba (swila na koboko) ni kua, swila ni mweusi na mkorofi hata usipomchokoza ,pia sumu yake si kali sana kama ya koboko. Lakini koboko yeye mara nyingi ni mtaratibu,ila ukimchokoza balaa lake sio la kitoto. Anakimbia mno, sumu kali sana ambayo inadaiwa kuua binadamu chini ya dakika 20 endapo atachelewa kituo cha afya. Black mamba hua na rangi ya kijivu au kijani. Anaitwa black mamba sio kwa kwasababu ya rangi yake,bali rangi ya mdomoni mwake ndio nyeusi.
Umeelezea vizuri kabisa kuhusu koboko
 
Koboko anajificha sana. Sasa ikitokea akajua umemuona basi anaanza vita. Lakini yeye anatambua uwepo wa adui hata kilometer 2 kabla hujamfikia.... Cobra huyo swila yeye anajihami kwa ukubwa wake, swila ni mkubwa mara tatu ya koboko na ana silaha ya mate. Hao nyoka nimeua sana.
 
Sio kweli. Moja ya nyoka mpole na mstaarabu ni black mamba(koboko).
Mara ya mwisho kumuona live ni Oktoba 2024 njiani. Mara baada ya kumuona nilisimama umbali wa mita 7 au 8 hivi. Kuonesha sio mshari,alikaa kwa takribani dakika 5 akiwa ametulia palepale. Kisha baadae alianza kuondoka taratibu.

Pia,kwa sie wakulima wa tumbaku tunakutana nao mara nyingi sana kwenye mabani ya kuchomea tumbaku kwani sehemu hizo zinakua na utulivu hasa nyakati za kiangazi na pia ni mawindo yao ya mijusi na panya. Zoezi la ukataji kuni za kuchomea tumbaku nalo hutukutanisha na nyoka huyu hatari kwani hupendelea kuishi kwenye miti mikubwa yenye mapango.

Nyoka hatari ambaye mkionana tu huanza kutengeneza mashambulizi ni Cobra (swila) ambaye ni mweusi. Yeye akikuona hata kama ni nyoka mdogo lazima kwanza ainue kichwa,mdomo wake hutanuka na kuanza mashambulizi kwa kutema mate.

Utofauti wa cobra na black mamba (swila na koboko) ni kua, swila ni mweusi na mkorofi hata usipomchokoza ,pia sumu yake si kali sana kama ya koboko. Lakini koboko yeye mara nyingi ni mtaratibu,ila ukimchokoza balaa lake sio la kitoto. Anakimbia mno, sumu kali sana ambayo inadaiwa kuua binadamu chini ya dakika 20 endapo atachelewa kituo cha afya. Black mamba hua na rangi ya kijivu au kijani. Anaitwa black mamba sio kwa kwasababu ya rangi yake,bali rangi ya mdomoni mwake ndio nyeusi.
Wewe ni mporipori halisi umeielezea vizur sana
 
Picha
 
Wiki iliyopita kwa mara ya kwanza niigata na nyoka nikiwa nyumbani ... nyoka mdogomweusi hivi tumbo jeupe ...yule mjinga nilimuua baada ya kunigonga ila ana sumu kali sna nilienda hospital ila hawakua na ant venom usiku ule hadi kufika asubuhi misuli ya mwili mzima ilikua inauma huku guu limevimba na kuuma haswa ..nilhama hospital hadi mloganzila kesho yake ndo kupata ant venom kwa 300k ila God iz good sijapona vizuri ila naendelea vema ..nimetangaza vita na nyoka popote ntakapomuona nyoka NAUA
 
Huyo ni hatari ila hajamfikia Colin Diep
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom