Sio kweli. Moja ya nyoka mpole na mstaarabu ni black mamba(koboko).
Mara ya mwisho kumuona live ni Oktoba 2024 njiani. Mara baada ya kumuona nilisimama umbali wa mita 7 au 8 hivi. Kuonesha sio mshari,alikaa kwa takribani dakika 5 akiwa ametulia palepale. Kisha baadae alianza kuondoka taratibu.
Pia,kwa sie wakulima wa tumbaku tunakutana nao mara nyingi sana kwenye mabani ya kuchomea tumbaku kwani sehemu hizo zinakua na utulivu hasa nyakati za kiangazi na pia ni mawindo yao ya mijusi na panya. Zoezi la ukataji kuni za kuchomea tumbaku nalo hutukutanisha na nyoka huyu hatari kwani hupendelea kuishi kwenye miti mikubwa yenye mapango.
Nyoka hatari ambaye mkionana tu huanza kutengeneza mashambulizi ni Cobra (swila) ambaye ni mweusi. Yeye akikuona hata kama ni nyoka mdogo lazima kwanza ainue kichwa,mdomo wake hutanuka na kuanza mashambulizi kwa kutema mate.
Utofauti wa cobra na black mamba (swila na koboko) ni kua, swila ni mweusi na mkorofi hata usipomchokoza ,pia sumu yake si kali sana kama ya koboko. Lakini koboko yeye mara nyingi ni mtaratibu,ila ukimchokoza balaa lake sio la kitoto. Anakimbia mno, sumu kali sana ambayo inadaiwa kuua binadamu chini ya dakika 20 endapo atachelewa kituo cha afya. Black mamba hua na rangi ya kijivu au kijani. Anaitwa black mamba sio kwa kwasababu ya rangi yake,bali rangi ya mdomoni mwake ndio nyeusi.