Mjue Bertha akili mingi!..

Mjue Bertha akili mingi!..

Wick

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
8,312
Reaction score
12,200
Kuna kipindi kalizuka kaujumbe fulani kwenye E-mails za watu kuwa bimdada fulani anajitambulisha yeye ni muivory coast na amekimbia machafuko nchini kwao na wazai wake wameuliwa lakini baba yake alikuwa tajiri na ndugu zake wanataka mdhulumu utajiri hivyo anaomba msaada wako ili aweze kumlipa mwanasheria wake. Ukimsaidia akashinda kesi mtakuja gawana ule utajiri, sasa kuna wajinga wakawa wanasaidia bana kumbe 'Kekundu'.Kama hujui hiyo ishu kuna mwanamama yeye aliifanya Karne ya 19 huko (miaka ya 1800s).
***************************************************************************************************************
Karne ya 19 miaka ya 1851 alizaliwa Mwanamama mmoja matata na tapeli sana aliyeitwa Bertha Heyman au kwa jina jingine "Big Bertha"au "Confidence Queen". Unaambiwa bimdada alikuwa anajiamini balaa, akianza kukupiga maneno lazima utaingia line kumpa anachotaka. Hebu fikiria huyo mama aliweza muibia mtu akiwa jela, jamaa akatoa pensheni yake yote kumpa bimdada!. (ikiwa umewahi angalia series ya Sherlock Holmes, season 4 episode ya 13 na 14 kuna yule dada yake sherlock-Eurus Holmes alikuwa anaweza kukuconvince mpaka ukafanya anachotaka).
Huyu bimdada historia inasema alizaliwa huko Prussia, mwaka 1878 akahamia Marekani. Aliolewa mara mbili lakini mpaka anaanza kazi yake alikuwa kashaachika!. Style yake ya kuibia watu ilikuwa anajifanya bonge la dada la kitajiri aliyerithi utajiri ingawa kwa wakati huo anatafuta njia za kuweza kupata mirathi ili aweze utumia vizuri utajiri wake. Ukiangalia confidence anayotumia kukuambia na muonekano wake lazima uingie line kumsaidia iwe kumpa hela au hata kumruhusu akae hotelini kwako (si unajua akipewa urithi wake atalipa!).
Kuna kipindi alikuwa anakaa hoteli za kitajiri anapewa hadi wahudumu spesho kwa ajiri yake, hapo pote anawaambia wenye hoteli alivyo maarufu sehemu fulani na utajiri wake ulivyo mkubwa+anavyotaka kuutumia, watu wanaelekea kibrah!. Alipokuja kamatwa akahojiwa hela alizokuwa anatapeli watu alipeleka wapi, bimdada akawaambia alikuwa anawapa masikini waweze ishi na wao. Pia alikuwa anapenda sana wale watu wanaojiona hawawezi ibiwa. ina maana ukijifanya mtoto wa mjini mbele yake anadeal na wewe akuonyeshe nani wa mjini zaidi, ila ukiwa mshamba hata hajishughulishi na wewe!.
"The moment I discover a man's a fool I let him drop, but I delight in getting into the confidence and pockets of men who think they can't be 'skinned.' It ministers to my intellectual pride."
Baada ya watu kuanza shtuka wanapigwa na bimdada ikabidi wakamreport Polisi na hapo ndipo purukushani na polisi zikaanza sasa!. Ikawa ni kukamatwa na kufungwa jela kawaida kwake!.
Bimdada moja ya tukio alilowahi piga mpaka akakamatwa unaambiwa alikuwa anasafiri kwa treni toka Chicago akakutana na Kondukta wa ile treni, konda akajifanya mjanja bimdada akaona amkomoe sasa akampiga maneno yule konda kwamba yeye ni bonge la dada wa kitajiri na ana bonge la jumba halina msimamizi kama vipi konda aache ile kazi aende nae akalisimamie kwa ajiri yake!. Halafu akamwambia sema hapo ana tatizo linahitaji kufanyiwa mchakato kidogo na agent wake sema hela zimeisha na mpaka kufatiria itamchukua muda kama vipi konda ampe hela zake, kumzuga zaidi konda akapelekwa kwenye moja ya majengo maza akajisifu la kwake!. Konda bwana akaingia line akafanya vyote![emoji2].
Kesi yake nyingine ilikua alimtapeli mfanyabiashara mmoja huko London, wakati huo ana kesi tena ya kumuibia bibi kizee saa za dhahabu na fedha wakati wapo safarini. Hizo zote hazijaisha wakati anatoka mahakamani kusikiliza kesi zake, akakamatwa tena alimtapeli mfanyabiashara mwingine fedha. Ikabidi mahakama imfunge kifungo cha miaka miwili jela.
Wakati yupo jela akapata rafiki, yule rafiki kujikuta mjanja, bimdada akaona isiwee tabu akarudi kazini akampiga maneno mfungwa mwenzie, jamaa akatoa hela yake yote aliyokuwa amejiwekea akiba ya maisha yake yote. Wakili aliyekuwa anamuwakilisha mwanamama nae hakuachwa nyuma alipigwa maneno na yeye, baadae bimdada akamtapeli na dalali wa soko la hisa Marekani - Wall Street kiasi cha hisa za kutosha kupitia hela feki. Kwenda mahakamani ikabidi apigwe miaka 5 jela tena!.
Huyo ndiye mwanamama mmoja matata sana aliyesumbua watu na akili ya ziada kuwaibia wanaojifanya watoto wa mjini!. Ambaye marekani haimsahau, hadi kwenye baadhi ya matangazo anawekwa picha zake!
Bertha_Heyman_500.jpg

Wabongo tumeibiwa karne ya 21 lakini idea kamili kuna mtu aliifanya karne ya 19 kikamilifu.
Cc: Da'Vinci hearly Jolie Jolie Shunie
 
Back
Top Bottom