Mjue Alberto Fujimori Rais mtata wa zamani wa Peru mwenye uraia wa nchi mbili Peru na Japan

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939
alberto-fujimori-3.jpg


Alberto Fujimori alianza vuguvugu la kisasa na hatimae kuwa mwanasiasa mkubwa chini Peru, katika kugombea nafasi ya Urais na kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi wa Rais ambapo ushindi wake uliwastua watu wengi duniani kiasi cha kumpa jina kwamba ni Rais wa kwanza kutoka bara la Asia kuongoza nchi iliopo Amerika Kusini. Uchumi wa Peru ulianza kudorora na alifanya mabadiliko katika katiba ya nchi yake kitendo kilicholaaniwa na jumuiya za kimataifa lakini wananchi wa Peru walifurahia mabadiliko hayo na ndipo alipofanya mabadiliko makubwa katika nyanja mbalimbali za kiuchumi

Alberto Fujimori alikua Rais wa 62 wa nchi ya Peru iliopo Amerika kusini Mashariki, aliongoza Peru kutoka mwaka 1990- 2000 alijaribu kuijenga kiuchumi, vuguvugu la mtikisiko wake kisiasa lilianza mwaka 1997.

Mwaka 1997 gazeti moja jipya na maarufu sana nchini Peru liitwalo caretas lililoripoti uraia wa Alberto Fujimori kwamba Alberto Fujimori alizaliwa katika mji wa Kawachi Kumamoto nchini Japan, hivyo alikua ana uraia wa nchi mbili yaani Japan na Peru, kuna taarifa zilizodai wazazi wa Fujimori walimzaa Alberto nchini Japan, vilevile ziliibuka habari zilitolewa na gazeti hilo kwamba kwamba wazazi wake yaani baba yake mzazi Naochi Minami Fujimori na mama yake mzazi Matsue Inomoto walihamia nchini Peru mwaka 1934 wakiwa na watoto wawili akiwemo Alberto, lakini pia kuna habari tatanishi kwamba Alberto Fujimori alizaliwa nchini Peru tarehe 28 Julai 1938 hivyo kuongeza utata, alikuja kupata kashfa ya rushwa na uvunjani na ukiukwaji wa haki za binaadamu mwaka 2000, hivyo mwaka 2000 alikimbilia Japan, akiwa japan alijaribu kujiuzulu urais wa Peru kwa kutumia mawasiliano ya njia ya Fax, bunge la congress la Republican nchini Peru lilikataa kujiuzulu kwa Rais huyo akiwa nje ya nchi mpaka arudi nchini Peru ili apigiwe kura ya kutokua na imani nae ili kuendelea kupewa heshima kama mstaafu.

Rais Fujimori akiwa nchini Japan alisafiri kwenda nchini Chile ndipo alipokamatwa na maafisa wa Peru akiwa bado ni Rais na kurudishwa nchini Peru hivyo kufunguliwa mashtaka kadhaa ikiwemo ya rushwa, uvunjaji na ukandamizaji wa haki za binaadamu, kesi yake ilirindima kwa muda mrefu, ndipo mwaka 2007 alihukumiwa miaka 5 baada ya kukutwa na hatia katika makosa ya rushwa, mwaka 2009 alisomewa mashtaka ya uvunjaji wa haki za binaadamu nchini Peru na kukutwa na hatia hivyo kuhukumiwa kwenda jela miaka 25
 
Back
Top Bottom