Mjomba wangu kadhalilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Bunda kwa kupigishwa magoti mbele ya viongozi wenzake

danymTZ

JF-Expert Member
Jan 17, 2014
375
568
Mtendaji wa kata ya kitengule wilaya ya bunda ndg. Deus Bwire ameamrishwa na mkuu wa wilaya ya Bunda bi. Lidya Bupilipili kupiga magoti mbele ya viongozi wenzake kwenye kikao.

Hili tukio lilitokea mnamo tarehe 2/10/2018 ambapo mkuu wa wilaya aliwataka watendaji wa vijiji ambao hawakuudhuria kikao waripoti kesho yake ofisini kwa mkuu wa wilaya.

Ndipo mtendaji wa kata aliposimama na kuwatetea watendaji hao kuwa walichelewa kupata taarifa ndiyo maana hawakuudhuria katika kikao hicho.

Baada ya maelezo hayo mkuu wa wilaya hakuridhishwa nayo na akamtaka mtendaji huyo kupiga magoti,kitendo ambacho alitii kwa muda wa nusu saa akiwa amepiga magoti. Mtoa taarifa hii ni muathirika mwenyewe Ndg. Deus Bwire ambaye ni mjomba wangu wa damu na haya hapa chini ni maneno yake aliyoyatoa,nanukuu"Mimi Nina miaka zaidi ya hamsini na nina watoto tisa na wajukuu,lakini kitendo cha kupigishwa magoti mbele ya kundi la viongozi wenzangu kama mtoto wa darasa la pili ni kunidhalilisha na hadi sasa sipo sawa."

KWA MAMLAKA ZA UTEUZI:
Mheshimiwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuri amekuwa akiwachukulia hatua mbalimbali viongozi wanaofanya makosa mbali mbali ikiwemo ufisadi na uzembe na mengineyo.Sijawahi kumuona Mh Rais akimdharirisha kiongozi yeyote hadharani mbele ya wananchi au viongozi wengine.

Rais huwa anatumbua hadharani ambapo ni jukumu lake kisheria lakini siyo kufikia hatua kama aliyofikia huyu mkuu wa wilaya ya bunda. Zipo adhabu anazoweza kutoa kiongozi kwa mtumishi ambazo zipo kisheria lakini siyo za kudharirisha kama hizi.

Nataka nitumie Uzi huu kuwaomba viongozi wetu hasa wakuu wa wilaya na mikoa kufuata sheria pindi wanapowachukulia hatua mbali mbali watumishi wa Serikali.

Pia nimuombe Mh Rais awaagize viongozi hawa wafuate sheria pindi wanapotekeleza majukumu yao ili haya mambo yasiwe kama mazoea kwani yanakatisha tamaa watumishi wengi sana.

Mjomba wangu ameumia na pia sisi ndugu zake tumeumizwa na jambo hili. Hata kama alikosea mbele ya mkuu wa wilaya lakini hakustahiri kupewa adhabu ya kadharirishwa kiasi hiki.

Nawasilisha
IMG-20181003-WA0000.jpg
 
Nina imani kubwa sana na Mh Rais wangu. Naamini atawaonya hawa viongozi wafuate sheria. Ombi langu wala siyo kufukuzwa kwa huyu mkuu wa wilaya bali Mh Rais awaonye hawa viongozi wafuate sheria katika kushughurikia watumishi.
 
Sithani kama hicho kitendo kingewezekana katika wilaya za Tarime na Serengeti. Hata hivyo, wilaya hizo hazijawahi kuwa na DC Mmama au Mdada.
 
Mtendaji wa kata ya kitengule wilaya ya bunda ndg. Deus Bwire ameamrishwa na mkuu wa wilaya ya Bunda bi. Lidya Bupilipili kupiga magoti mbele ya viongozi wenzake kwenye kikao.

Hili tukio lilitokea mnamo tarehe 2/10/2018 ambapo mkuu wa wilaya aliwataka watendaji wa vijiji ambao hawakuudhuria kikao waripoti kesho yake ofisini kwa mkuu wa wilaya.

Ndipo mtendaji wa kata aliposimama na kuwatetea watendaji hao kuwa walichelewa kupata taarifa ndiyo maana hawakuudhuria katika kikao hicho.

Baada ya maelezo hayo mkuu wa wilaya hakuridhishwa nayo na akamtaka mtendaji huyo kupiga magoti,kitendo ambacho alitii kwa muda wa nusu saa akiwa amepiga magoti. Mtoa taarifa hii ni muathirika mwenyewe Ndg. Deus Bwire ambaye ni mjomba wangu wa damu na haya hapa chini ni maneno yake aliyoyatoa,nanukuu"Mimi Nina miaka zaidi ya hamsini na nina watoto tisa na wajukuu,lakini kitendo cha kupigishwa magoti mbele ya kundi la viongozi wenzangu kama mtoto wa darasa la pili ni kunidhalilisha na hadi sasa sipo sawa."

KWA MAMLAKA ZA UTEUZI:
Mheshimiwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuri amekuwa akiwachukulia hatua mbalimbali viongozi wanaofanya makosa mbali mbali ikiwemo ufisadi na uzembe na mengineyo.Sijawahi kumuona Mh Rais akimdharirisha kiongozi yeyote hadharani mbele ya wananchi au viongozi wengine.

Rais huwa anatumbua hadharani ambapo ni jukumu lake kisheria lakini siyo kufikia hatua kama aliyofikia huyu mkuu wa wilaya ya bunda. Zipo adhabu anazoweza kutoa kiongozi kwa mtumishi ambazo zipo kisheria lakini siyo za kudharirisha kama hizi.

Nataka nitumie Uzi huu kuwaomba viongozi wetu hasa wakuu wa wilaya na mikoa kufuata sheria pindi wanapowachukulia hatua mbali mbali watumishi wa Serikali.

Pia nimuombe Mh Rais awaagize viongozi hawa wafuate sheria pindi wanapotekeleza majukumu yao ili haya mambo yasiwe kama mazoea kwani yanakatisha tamaa watumishi wengi sana.

Mjomba wangu ameumia na pia sisi ndugu zake tumeumizwa na jambo hili. Hata kama alikosea mbele ya mkuu wa wilaya lakini hakustahiri kupewa adhabu ya kadharirishwa kiasi hiki.

NawasilishaView attachment 885246
Huko bunda afadhali kidogo kule Tarime DC ndiyo balaa yeye huwabambikia kesi hata kuwapiga kupitia Polisi, huko mara kuna chuki kubwa inajengwa toka kwa wananchi dhidi ya kamati za Ulinzi na usalama za ma DC, lakini cha ajabu kwa Serikali hii ya magufuli yeye hupenda yule DC anayetesa wananchi hasa akisikia DC kawafanyia unyama wapinzani hufarijika sana na hupandishwa cheo na kuwa RC, usije kushangaa hao ma DC wakapandishwa vyeo
 
Sithani kama hicho kitendo kingewezekana katika wilaya za Tarime na Serengeti. Hata hivyo, wilaya hizo hazijawahi kuwa na DC Mmama au Mdada.
Tarime DC yeye hutumia Polisi kuwapiga na kisha kuwakamata hapo hapo kuwabambikia kesi kwa kasi ili wakose mda wa kulalamika au kuandamana kupinga unyanyasaji wake.
 
Back
Top Bottom