Shida ya utegemezi inakuwa kama kufungiana nira.
Kama ukiwa kijijini na unauwezo kwa kimaisha hata kuliko wale wa mjini, bado unadhani wewe huna uwezo. Cha kusikitisha bado utaishi kwa kutaka ufanyiwe vile unavyoona mtima wako unafurahi pasipo kujua mwenzio anaumia vipi ili kujaribu kukukwamua.
Ukiwa huna kazi ya elimu, hata kama upo mjini na unavyanzo vyote bora vya maisha, daima una amini kuwa wale wenye kazi ya kisomi ndio wenye wajibu wa kusaidia ndugu. Hata shida ya jumla ikitokea wewe unakuwa mwepesi kusema, wache wasomi watatatua...na ikiengemea kwa yule mwenye moyo, siku zote inazidi kula kwako hata kama una kipato kidogo.
Wapo wazazi na ndugu wa karibua ambao pia walikwisha fanya kazi, wanajua maisha yalivyo lakini unapojaribu kuwasaidia hata kwa kidogo au ukisema huweiz, wanakuwa wakali kama nyuki na kuona hufai kabisa.
Kuna tabaka jingine la wale ambao waweza kuwa ni ndugu au rafiki wa karibu, utamwonea huruma umasaidie, lakini inakuwa ni kama umempiga gamzi ya ulemavu wa akili. Itakuwa hata kununua mswaki wake ni shida kuu, lakini kama utaamua kuishi nae, hataki kufuata kanuni za jumla,anataka kujiamulia kila kitu kuanzia chakula, muda wa kulala, kazi za kusaidia nk. Ukimuonya, inakuwa ndo kisa hata kama uliishi nae miaka kumi ya wema, yote itafutika siku moja.
Kuna hawa wengine ambao hata kama yupo nje ya nchi, yeye kwake ni fahari kusema "ndugu yangu ni fulani" na atakuwa mwepesi kukusifia kwa kila jambo, hata akipata zake hawezi hata siku moja kusema anunue kibaba cha unga wala soda kuwapa watoto. Ukimjulisha labda siku umeishiwa kama anazo asaidie anakujibu "toka lini bahari ikaazima maji kisimani"...
Wapo wale ambao hawaridhiki kabsaaa na kile anachopewa, hajui una nini lakini ukimpa anapokea na badae utasikia mtaani miji neno kuwa hata kama yeye ni masikini hawezi kupewa msaada wa namna hiyo. Hili ni tabaka la wale ambapo yupo tayari kupokea nguo za ndani za mzungu akaziita mtumba kuliko kumvulia suluali au gauni lako atasema unampa makombo ya nguo na umemdharu..
Upo utegemezi mwingine ambao tunajitakia, kwa mfano mmekubalina na mwezio kumwitisha mdogo wako aje toka mjini ili asome na pia kuwasidia sehemu ya majukumu...baada ya muda, mwenzio nae anasema tumwitishe na mdogo wake wakati akiona kabisa hata pa kulala hakuana...inakuwa sasa ni kisa cha mvutano katika ndoa...Na hawa ndugu wakija, paengine huwa hata lile walilojia hawataki kufanya, ukiwatuma hata kazi ndogo tu wanajibu wao si ma-house boi/house-girl...wanataka kuwa na amri kila eneo kuliko mwenye nyumba.
Wapo wategemezi wangine ambao hatuwezi kuwabainin kirahisi, ni hawa ambao wanataka kila siku tuwe nao kwenye starehe nk. Lakini hata akiwa na kitita chake mfukoni, hawezi kutoa hata senti kununua soda..yeye kila siku hana tu....(aweza kuwa mume, mke, rafiki wa kike au kiume).