Mjomba jitathmini upya, Urais si lele mama

activisty

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
315
Reaction score
107
Nilishawahi kusema hapo awali wakati wa Jk kwamba uraisi si lele mama.Na sasa narudia tena wakati huu wa Mjomba Magu, na ninaomba wanajamii na umma kwa ujumla utambue Kinachonituma, kusema haya ni uteuzi wa wakuu wa mikoa, amri yake katika kuwaapisha(amri kwa maana ya hotuba)uchaguzi wa zanzibar na hali halisi ya maisha ya mtanzania wa chini kwa sasa.

Nauliza ni vigezo vipi vinatumika kuteua wakuu wa mikoa? Lakini niende mbali kabisa na kuuliza nini maana ya uchaguzi? Nini maana ya uteuzi? Kwa nini wananchi tuchague kuanzia wenyeviti wa mitaa, madiwani, wabunge ambao kimsingi wanazidiwa nguvu na wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa, ambao wanateuliwa na mtu mmoja tu ambaye tumemchagua sisi?

Nini kazi hasa ya wakuu wa wilaya? Wakurugenzi wa halmashauri n.k? Nini kazi zao ikiwa ndani ya wilaya kuna majimbo ambayo kimsingi yanawakilishwa tayari na watu ambao tumewachagua kwa jina la demokrasia?

Kwanini nafasi hizo zipo, na kwanini zisiondolewe kupunguza mlolongo wa viongozi katika mkoa ambao kwa msingi majukumu yao ni machache na yanaweza kusimamiwa na mbunge? Wakuu wa wilaya ni wa nini?

Twende kwa wakuu wa mikoa. Kwanini wanateuliwa? Ni kwanini basi kwa kuwa ndio wasimamizi wa mkoa mzima wasichaguliwe na wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa maana ya madiwani na wabunge wa mkoa husika ili kuruhusu ufanisi na kuongeza kasi ya utendaji katika mikoa na baadaye taifa kwa ujumla?

Yote nauliza kwenu wana jamii na umma kwa ujumla, mtathimini na mpate majibu. Uongozi si lele mama jitathimini.

Katika hayo yote tukumbuke nguvu ya vijana na kama lengo ni ulinzi, tunavijana wanajeshi wenye mafunzo mazuri na wanaoweza kuisimamia mikoa hiyo inayoitaji ulinzi wa karibu na pia wapo wengine ambao wanaweza pata mafunzo hayo na wakafanya kazi nzuri tu.Tuache wastaafu wapumzike. Uongozi si lele mama jitathimini.

Kauli/amri ya kusema kwamba vijana wanaocheza pool table wakamatwe na walimishwe kwa lazima ni kauli ya kimabavu na ni kauli ya kupingwa na vijana wote hapa nchini.

Nauliza tu, ni vijana wangapi ambao wanamaliza vyuo kila mwaka na wako mitaani hawana ajira?

Ni jukumu la nani basi kuwapatia ajira? Yale mashamba kule morogoro ambayo yametekwa na vigogo huku yakitelekezwa bila kuendelezwa je, ni jukumu la nani sasa kuwagawia vijana hawa wayafanyie kazi?

Vile viwanda vilivyotokomea, ukosekanaji wa pembejeo, ruzuku n.k, ni jukumu la nani kuweka mambo sawa hapo vijana wapate ajira?

Nauliza tena hizo pooltable pia ni ajira za vijana hao hao. Vijana wanaajiriwa ili waziendeshe, na wengine kutumia mchezo huo kugawana kile kidogo kinachopatikana. Sasa je vijana hawa waende wapi?

Hapo hapo mnadai kodi, je ni jukumu la nani kuwasaidia vijana hawa? Uongozi si lele mama jitathimini.

Matumizi ya mabavu zanzibar ati kwa jina la uchaguzi. Nauliza hivi kweli uchaguzi huo unaenda kufanywa kwa faida ya nani? Ikiwa chama kilichoshinda uchaguzi huo hakishiriki uchaguzi huo?

Je, wazanzibar wameamua au wameridhia uchaguzi huo? Nini jukumu la rais wa jamhuri ya muungano ambayo ni tanganyika na zanzibar? Nini jukumu lako mjomba? Kwa majibu uliyoyatoa hapo awali niseme tu mjomba, urais si lele mama,jitathimini.

Mwisho mjomba nimesikia na kuona ukipewa sifa nyingi za kiutendaji, lakini mjomba maisha halisi ya mtanzania wa chini yapo pale pale, wafanyakazi serikalini ni watumwa sasa, wafanyakazi wa umma wanatenda kazi zao kwa hofu sasa si kwa hiari na si kwa matakwa ya kisheria.

Najiuliza hofu hizo zitadumu hadi lini, jibu sina. Kilo ya sukari, unga, mchele, maharage bei ni ile ile, kipato ni kile kile, maisha ni yale yale. Nauli ya dala dala ni ileile, nauli ya mwanafunzi ni ile ile, elimu bure nini faida au hasara zake?

Kawaulize wanafunzi wa vijijini ambao walishazoea kunywa uji shule.saa nne na kula ugali mchana saa nane na kutoka shule saa kumi na moja jioni wakiwa vizuri kabisa, ila sasa wazazi wamesikia elimu bure, wamegoma kuchangia chakula wakijua kila kitu ni bure, huku anaeteseka ni mwanafunzi yule ambaye nyumbani baba na mama ni walevi, akitoka hakuna chakula akirudi hakuna chakula zaidi ya kusikiliza ugomvi kati ya wazazi wake, huku wadogo zake wanne waliofatana wakikesha na kulia njaa. Lakini niulize sifa na pongezi hizo ni nani anaekupa?

Ni watanzania hawa hawa au? Akifukuzwa mkurugenzi wa bandari inanisaidia nini mimi mtanzania ambaye bahari yenyewe sijawahi kuiona? Bidhaa? Je nazimidu kuzinunua kwa kipato changu?

Niseme tu sipingani na kufukuzwa viongozi wabadhirifu ila niseme tu wanaoitaji kuguswa kwa sasa ni watu ambao wana impact kwa wa watanzania ambao asilimia kubwa ni masikini.

Watafutie masoko wakulima wa pamba, kahawa, sambaza wataalam, sambaza pembejeo, ruzuku, wabane wafanyabishara walaghai, wape ajira vijana wa wazazi ambao wameuza adi mashamba yao kuwasomesha watoto wao, sasa wamemaliza na hawana ajira na wapo kijijini pale kwa wazazi wao huku wakiongeza mzigo wa familia.

Hao ndio wanaitaji kuguswa, hao ndio waliokupa kura zao huku wakiwa hawajui kusoma wala kuandika, pengine hao ndio waliokuchagua bila hata kuisoma ilani ya ccm.hospitali sio muhimbili tu,Wala sio mwananyamala tu na Tanzania sio dar es salaamu tu.

Urais/uongozi si lele mama, Jitathimini...

By mwanaharakati huru Activistyi@yahoo.com
 
Jaman Watanzania tumepata raisi mzuri Africa nzima wanaona juhudi zake.. Tumpe ushirikiano wa kutosha
Mtoa maada nimekuelewa lakini nikutoe wasiwasi tupo na dira nzuri tumpe muda raisi anachukia rushwa sana.. Tumwombee raisi amejipa kazi ngumu atapigwa hadi na chama chake
 
Juhudi zipi?
 
Juhudi zipi?
Kuongezeka kwa makusanyo ya kodi kutoka
Mwezi wa 8 mwaka 2015=billion 850
Mwezi wa 9 billion 875
Mwezi wa 10 billion 767
Mwezi Wa 11 billion 799
Mwez Wa 12 trillion 1.2
Mwezi wa 1 trillion 1.3
Mwezi wa 2 trillion 1.2
Kufuta safari za nje
Kukemea ufisad
Wala rushwa kesi zao Zipo mahakamn
 
Kuongezeka kwa makusanyo ya kodi kutoka
Mwezi wa 8 mwaka 2015=billion 850
Mwezi wa 9 billion 875
Mwezi wa 10 billion 767
Mwezi Wa 11 billion 799
Mwez Wa 12 trillion 1.2
Mwezi wa 1 trillion 1.3
Mwezi wa 2 trillion 1.2
Kufuta safari za nje
Kukemea ufisad
Wala rushwa kesi zao Zipo mahakamn
Una uhakika na data zako?
 
umeandika mengi ila point ya msingi ni hii rais akubali kutumbua jipu la katiba mpya
bila hilo, tutasaga magoti hapa kwa sala na maombi yasiyojibika milele
 
umeandika mengi ila point ya msingi ni hii rais akubaoi kutumbua jipu la katiba mpya
bila hilo, tutasaga magoti hapa kwa sala na maombi yaisyojibika kabisa
Eh X malikia wa MMU upo? Sijakusikia kitambo......
 
Kuongezeka kwa makusanyo ya kodi kutoka
Mwezi wa 8 mwaka 2015=billion 850
Mwezi wa 9 billion 875
Mwezi wa 10 billion 767
Mwezi Wa 11 billion 799
Mwez Wa 12 trillion 1.2
Mwezi wa 1 trillion 1.3
Mwezi wa 2 trillion 1.2
Kufuta safari za nje
Kukemea ufisad
Wala rushwa kesi zao Zipo mahakamn

utaamuka tu we ota ndoto nyevu
 
Unamuasa R
Nilishawahi kusema hapo awali wakati wa Jk kwamba uraisi si lele mama.Na sasa narudia tena wakati huu wa Mjomba Magu, na ninaomba wanajamii na umma kwa ujumla utambue Kinachonituma, kusema haya ni uteuzi wa wakuu wa mikoa, amri yake katika kuwaapisha(amri kwa maana ya hotuba)uchaguzi wa zanzibar na hali halisi ya maisha ya mtanzania wa chini kwa sasa.

Nauliza ni vigezo vipi vinatumika kuteua wakuu wa mikoa? Lakini niende mbali kabisa na kuuliza nini maana ya uchaguzi? Nini maana ya uteuzi? Kwa nini wananchi tuchague kuanzia wenyeviti wa mitaa, madiwani, wabunge ambao kimsingi wanazidiwa nguvu na wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa, ambao wanateuliwa na mtu mmoja tu ambaye tumemchagua sisi?

Nini kazi hasa ya wakuu wa wilaya? Wakurugenzi wa halmashauri n.k? Nini kazi zao ikiwa ndani ya wilaya kuna majimbo ambayo kimsingi yanawakilishwa tayari na watu ambao tumewachagua kwa jina la demokrasia?

Kwanini nafasi hizo zipo, na kwanini zisiondolewe kupunguza mlolongo wa viongozi katika mkoa ambao kwa msingi majukumu yao ni machache na yanaweza kusimamiwa na mbunge? Wakuu wa wilaya ni wa nini?

Twende kwa wakuu wa mikoa. Kwanini wanateuliwa? Ni kwanini basi kwa kuwa ndio wasimamizi wa mkoa mzima wasichaguliwe na wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa maana ya madiwani na wabunge wa mkoa husika ili kuruhusu ufanisi na kuongeza kasi ya utendaji katika mikoa na baadaye taifa kwa ujumla?

Yote nauliza kwenu wana jamii na umma kwa ujumla, mtathimini na mpate majibu. Uongozi si lele mama jitathimini.

Katika hayo yote tukumbuke nguvu ya vijana na kama lengo ni ulinzi, tunavijana wanajeshi wenye mafunzo mazuri na wanaoweza kuisimamia mikoa hiyo inayoitaji ulinzi wa karibu na pia wapo wengine ambao wanaweza pata mafunzo hayo na wakafanya kazi nzuri tu.Tuache wastaafu wapumzike. Uongozi si lele mama jitathimini.

Kauli/amri ya kusema kwamba vijana wanaocheza pool table wakamatwe na walimishwe kwa lazima ni kauli ya kimabavu na ni kauli ya kupingwa na vijana wote hapa nchini.

Nauliza tu, ni vijana wangapi ambao wanamaliza vyuo kila mwaka na wako mitaani hawana ajira?

Ni jukumu la nani basi kuwapatia ajira? Yale mashamba kule morogoro ambayo yametekwa na vigogo huku yakitelekezwa bila kuendelezwa je, ni jukumu la nani sasa kuwagawia vijana hawa wayafanyie kazi?

Vile viwanda vilivyotokomea, ukosekanaji wa pembejeo, ruzuku n.k, ni jukumu la nani kuweka mambo sawa hapo vijana wapate ajira?

Nauliza tena hizo pooltable pia ni ajira za vijana hao hao. Vijana wanaajiriwa ili waziendeshe, na wengine kutumia mchezo huo kugawana kile kidogo kinachopatikana. Sasa je vijana hawa waende wapi?

Hapo hapo mnadai kodi, je ni jukumu la nani kuwasaidia vijana hawa? Uongozi si lele mama jitathimini.

Matumizi ya mabavu zanzibar ati kwa jina la uchaguzi. Nauliza hivi kweli uchaguzi huo unaenda kufanywa kwa faida ya nani? Ikiwa chama kilichoshinda uchaguzi huo hakishiriki uchaguzi huo?

Je, wazanzibar wameamua au wameridhia uchaguzi huo? Nini jukumu la rais wa jamhuri ya muungano ambayo ni tanganyika na zanzibar? Nini jukumu lako mjomba? Kwa majibu uliyoyatoa hapo awali niseme tu mjomba, urais si lele mama,jitathimini.

Mwisho mjomba nimesikia na kuona ukipewa sifa nyingi za kiutendaji, lakini mjomba maisha halisi ya mtanzania wa chini yapo pale pale, wafanyakazi serikalini ni watumwa sasa, wafanyakazi wa umma wanatenda kazi zao kwa hofu sasa si kwa hiari na si kwa matakwa ya kisheria.

Najiuliza hofu hizo zitadumu hadi lini, jibu sina. Kilo ya sukari, unga, mchele, maharage bei ni ile ile, kipato ni kile kile, maisha ni yale yale. Nauli ya dala dala ni ileile, nauli ya mwanafunzi ni ile ile, elimu bure nini faida au hasara zake?

Kawaulize wanafunzi wa vijijini ambao walishazoea kunywa uji shule.saa nne na kula ugali mchana saa nane na kutoka shule saa kumi na moja jioni wakiwa vizuri kabisa, ila sasa wazazi wamesikia elimu bure, wamegoma kuchangia chakula wakijua kila kitu ni bure, huku anaeteseka ni mwanafunzi yule ambaye nyumbani baba na mama ni walevi, akitoka hakuna chakula akirudi hakuna chakula zaidi ya kusikiliza ugomvi kati ya wazazi wake, huku wadogo zake wanne waliofatana wakikesha na kulia njaa. Lakini niulize sifa na pongezi hizo ni nani anaekupa?

Ni watanzania hawa hawa au? Akifukuzwa mkurugenzi wa bandari inanisaidia nini mimi mtanzania ambaye bahari yenyewe sijawahi kuiona? Bidhaa? Je nazimidu kuzinunua kwa kipato changu?

Niseme tu sipingani na kufukuzwa viongozi wabadhirifu ila niseme tu wanaoitaji kuguswa kwa sasa ni watu ambao wana impact kwa wa watanzania ambao asilimia kubwa ni masikini.

Watafutie masoko wakulima wa pamba, kahawa, sambaza wataalam, sambaza pembejeo, ruzuku, wabane wafanyabishara walaghai, wape ajira vijana wa wazazi ambao wameuza adi mashamba yao kuwasomesha watoto wao, sasa wamemaliza na hawana ajira na wapo kijijini pale kwa wazazi wao huku wakiongeza mzigo wa familia.

Hao ndio wanaitaji kuguswa, hao ndio waliokupa kura zao huku wakiwa hawajui kusoma wala kuandika, pengine hao ndio waliokuchagua bila hata kuisoma ilani ya ccm.hospitali sio muhimbili tu,Wala sio mwananyamala tu na Tanzania sio dar es salaamu tu.

Urais/uongozi si lele mama, Jitathimini...

By mwanaharakati huru Activistyi@yahoo.com

Unamuasa Rais ajitathmini?? Hivi hayo uliyoandika hapo juu ni MALALAMIKO YAKO NA KUTOKURIDHIKA KWAKO au ni Ushauri wenye tija?? Mimi naona ni malalamiko tu ambayo hayana ushauri wowote wa maana. Unaona raha tu kuandika na kulalamika, hivi wewe binafsi umekua na mchango gani katika maendeleo ya nchi yako katika kipindi cha miezi 5 iliyopita??
 
Back
Top Bottom