Mjini wajanja wengi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjini wajanja wengi...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by jmnamba, Apr 13, 2012.

 1. j

  jmnamba Senior Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jana dada mmoja aliigonga gari ya mtu (kaka) kama ilivyo mbilinge-mbilinge za barabarani. Sasa dada baada ya kuona atalibeba hili kasheshe akamuambia yule kaka "...mimi naitwa Dina Marios... Nifuate ofisini..." Yule kaka kwa vile hakua akimfahamu kwa sura akaona okay tena mtu mwenyewe famous basi wakakubaliana iwe hivyo.

  Maskini wakati kila mmoja yupo ndani ya gari yake yule dada alichepuka pakuchepuka akapotelea anakojua yeye. Kwa vile kaka wa watu alikua anajia wapi ofisi za clouds zilipo ndio kuelekea. Kufika na kujielezea getini ndipo mlinzi akamuuliza kama anamjua huyo Dina Marios amuelezee na jinsi alivyovaa... Kaka wa watu mwisho wa siku akaambiwa "hivi tunavyoongea Dina Marios si ajabu by now ndio anamaliza kipindi... Wewe umeshaingizwa mjini.
  Habari ndio hiyo (niliisikia live toka kwa Dina mwenyewe).
   
Loading...