Mjinga sio yule asiye na elimu tu bali hata mwenye elimu na kushindwa kuitumia

Elisha Chuma

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
275
262
Kila mtu anazaliwa na akili na uwezo wa kutambua mambo, lakini unapopokea elimu ni kuongeza maarifa ya kulitambua jambo kwa undani zaidi, usijifungie kwenye chumba cha makaratasi ya uthibitisho kuwa ndio elimu yako, ila tumia uwezo na maarifa kuwa ndio elimu yako.

IMG_20210707_060314_495.jpg
 
Kwamba asiyekua na elimu ni mjinga?

Kinyume cha neno mjinga ni mwerevu/enye maarifa. Elimu sio maarifa bali ni njia moja wapo ya kupata maarifa.

Ulimaanisha nini labda ulipotumia neno elimu?
 
Kwamba asiyekua na elimu ni mjinga?

Kinyume cha neno mjinga ni mwerevu/enye maarifa. Elimu sio maarifa bali ni njia moja wapo ya kupata maarifa.

Ulimaanisha nini labda ulipotumia neno elimu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio asiekuwa na elimu ni mjinga.

Mjinga ni mtu asiekuwa na eulewa ama maarifa ya kitu,ujinga sio tusi ni hali ya kawaida kwa kila mtu.

unaweza kuwa mwerevu hapa ila ukawa mjinga kule ni hali ya kawaida, sasa ikiwa umepata elimu (Maarifa) ukishindwa kuitumia ni mjinga pia.

Na pia Elimu sio njia mkuu, ni kile unachokipata na kikabaki kichwani kwako

shule ,vyuo nk hizo ni njia ya kupata elimu, ila sio Elimu ni njia ya kupata shule.
 
- Ukiulizwa " Una Elimu gani?" jibu litakua tofauti na ukiulizwa " Una Maarifa gani?".

- Mfano unaweza usiwe na elimu ya uongozi lakini ukawa na maarifa ya uongozi hivyo usiwe mjinga kwenye uongozi. Elimu sio maarifa.
 
Back
Top Bottom