Mjikumbushe Mzumbe High School

Kweli mdau umetukumbusha mbali....mi nilikuwepo pale miaka ya 1995. Nakumbuka wengi wa hao waalimu...enzi zetu Headmaster alikuwa Mr Msuka...as a matter of fact..hiyo ilikuwa statement yake ya kufungulia speech parade.
Kuna mwalimu mmoja tulikuwa tunamwita Chuck Norris.....nimesahau jina lake aisee.

Msamiati wa Uchi wa Shangazi mnaukumbuka? Morris dereva alikuwa anajiita form six-combination PCO..hahahaaaaa!!!

Mzumbe imewatoa wengi sana aisee....siku hizi hamna special anymore....nakumbuka si tulikuwa special wa mwanzo mwanzo..tehetehetehe.....!!!

Msamiati wa Mongwe ulikuwa una maanisha kuwa umechacha...huna hela.
 
Duh!Wadau mmenifanya nimecheka sana kwa ofisi maana mmenikumbusha misamiati iliyokuwa imeshanitoka kabisaa
 
Kwa wale mliyosoma miaka ya 2000's mnakumbuka kuosha macho mida ya jioni baada ya kula msuli?
 
kujikumbusha siyo mbaya ni nzuri pia inajenga mahusiano makubwa miongoni mwa watu hivyo wala msiwapinge hata mimi ambaye sijasoma huko na furahi sana kusoma hizi past kwani zina nikumbusha mbali sana
 
Mi namkumbuka emily patrick t.o 2003, sebastian maganga t.o2004 na wengineo jamaa walikuwa vichwa mbaya
 
Duh, ama kweli nimekumbuka mbali sana. Inaonekana brother mimindiokile ulikuwa unakaa KIJIJI cha MIRAMBO BWENI No 3, kwa sababu Church man, Kijana wa Mzinga Jeshini, Shukuru, Karadoga wote hawa walikuwa bweni hilo. Nami naomba niwakumbushe wana Mzumbe vita ya kugombea wachezaji wa football.....Phinias Phares amepangiwa Mirambo, itakuaje achezee SHAABAN ROBERT nk... Namkumbuka brother mmoja tulimwita ZINJATHROPOUS kutokana na kujaaliwa vinyweleo vingi mwilini. Ingekuwa vema kama kupitia JF tutatambuana uwepo wa kila mwanaMzumbe na kuunganisha mawazo yenye kujenga. ALUMNI ni wazo jema kabisa. Naukumbuka wimbo wa shule......... "Malezi ya Mzumbe, elimu yake ni kamilifu ya kitanzania daima mbele nyuma mwiko" kupitia wimbo ule tulitoa ahadi "vijijini pia na mijini matunda yake yaonekana" yaah those good old days. Nawakumbuka brother MKUMBO Mitula, John Mongela alikuwa Katibu wa KIJIJI cha Mirambo, James Bwana Sports Chairman na bonge la Midfield wa Mirambo. Brother PITA BILA M/Kiti wa kiji Mirambo. Mnaukumbuka wimbo wa BAGENDA ADUMU? Tumlinde na tumuenzi katika Mzumbe? Duh ni mengi ya kukumbuka.
 
Duh! Kweli nimezeeka. Nimejaribu kufuatilia thread hii labda nitakuta majina ya jamaa niliokuwa nao A level 1979/81 pale Mzumbe "Shule ya Wanaume' sijayaona. Kuna mmoja kamtaja Judge Makaramba. Huyo tulikuwa naye pamoja na akina SAIDI SAIDI BAHROON (marehemu) alikuwa akipiga soka wacha mchezo! Pia kulikuwa na wanasoka wengine mahiri kama akina FINTAN DUMA 'Super Six', MAULIDI, JUMA CHEGENI (Kipa). Kulikuwa pia na timu kali sana ya basketball ikiundwa na akina ALFRED BINADAMU, MWANJAPAHI, ABDUL TEKELO, NYANDUGA, RUGARABAMU, MWITUMBA, na wengineo nimewasahau kwa majina. Ni miaka mingi mno imepita! Ilikuwa ni enzi za Headmaster COSMAS GANDAWEGA. Nitafurahi sana kujua waliko baadhi ya washikaji wa enzi hizo. Namkumbuka pia CHARLES KENYELA (sasa RPC Kiinondoni) wakati huo akiwa Form Five. Halafu kulikuwa na vijana watundu sana 'O' Level akina ANTHONY NAKATI, MOHAMED KIGANJA, RABDI MARIJANI, OMARI KIJAZI, TIBANYENDERA, HUSSEIN MACHOZI, (sio huyu mwanamuziki) na wengine wengi.
 
Nimekumbuka mbali sana,miaka ile ya 91-93 ,yule mpishi shangazi,mr KABARE mwl wa BIOS ,mr NDALU CHEM,MAMA MWIYENGE na usmart wake,Marehem Mkomboti na Mr ABOOD bus.Graduation wakaja DAKAWA ikawa issue kwa KILEI,wale F.6 WA 93 mnakumbuka ugali na mahomeboys(DAGAA KAUZU),Vipi ule mchakamchaka c ulikuwa poa kiafya. Kweli mzumbe vimepita vichwa ,wakowapi RAMADHAN ZONGO,BENO CHELELE, na wengine wengi, NAUNGA MKONO WAZO LA KUWA MZUMBE EX BLOG
 


Brother Mimindiokile umenikumbusha sana Kijiji cha MIRAMBO hasa bweni namba 3. Church man, Karadoga, Shukuru, Clemence Mwashambwa na wengi uliowataja nilikuwa nakaa nao katika bweni hilo. Huenda nikawa nafit ktk utambulisho wako wa Mtoto wa Mzinga Jeshini...............Kuna muungwana amemtaja brother Ndezi, Bob Ndezi, nasikitika kusema kuwa nilimkuta home kwao Igunga, anaonekana kutatizika na matatizo ya ufahamu kwa sasa, nilimsababhi na kumkumbusha kuhusu Mzumbe lakini hatukua ktk frequence moja. Jamaa wa pembeni wakasema anasumbuka na matatizo ya akili. Mungu amsaidie apone. Yako mengi ya kukumbuka kuhusu MZUMBE. Wazo la kuwa na Alumni ni zuri sana, litatuunganisha na kutoa mchango wa kuisaidia shule kwa namna moja ama nyingine.
Mungu ibariki Mzumbe
 

Kwenye red and his wife are no more in this world!!!!!!!!!
 
mmenikumbusha mbali sana mimimnilikuwa mzumbe kwa miaka sita 1995-2000 nilikuwa mkwawa namba nne namkumbuka mwalimu minja alitutandika darasa zima form one A kisa kumkumbushia muda wa kipindi chake cha english ulikuwa bado; tunawakumbuka enzi hizo mwalimu mkumbo ,bitwale, T.D.K. MSUKAhead master,mwasha marehemu wibonele, kabale(mganda) wazumbe wengi ni madaktari,mainjinia na wahasibu,tuache chuki binafsi kama ulishindwa kuachieve ulipokuwa mzumbe usitake kuwaaminisha watu kama wazumbe walikuwa wanpewa paper,katika darasa letu la PCB tulikuwa 25 ishirini wote tulikwenda muhimbili,2 walikwenda abrod na wawili walikwenda mlimani kuchukua bicom
 
Minja bado yupo.
Sapila,Mtawajibu,Malale,Mtesigwa wamepata Kuwa Head Master kwenye shule za Kata.
Matekele yuko Mzumbe University anapigisha vijana elimu.

Sapila du nimemmiss. Minja anawakumbuka almost wanafunzi wote aliowafundisha. Those days. Those days!!
 
jamani mimi nawakumbuka GREYSON NYANTAMBA,LUSEKELO KIBONA,BENJAMIN AMOS,ASAJILE JOHN,JOSIAH NOMBO,DANIEL NGONDYA,KWAME etc
 

Wengine ni Yohana Punguja, Mathew Maziku, Fikiri Charles, Batandika Mtaganya, Nkuba, Paul Daud.
 

Hahahah......Sasa mtwambie Jamii ya waTanzania mnaisaidiaje baada ya kupata elimu iliyotukuka? Maana wengi wa hawa watu ndo wamekuja kuwa zao na kizazi cha mafisadi Tanzania yetu ya leo.
 
Daaah! My Goosebumps Have Erected Mlipotaja IDM, Mongwe, Salo
Kilakala, Kilima Hewa, Nk
By The Way Nilikuwa Member Wa Mkwawa 4 Mpaka Namaliza A-level
Mvua Ikinyesha Ilo Tope Ni Kero
Indeed Mzumbe Was Unforgettable
Place To Every Person Who Ever Lived There.
Viva Mzumbe Secondary
School Song- Shule Yetu Mzumbe
 
Intake Yetu Tulikuwa Na Hawa Giants Of Ages
Hudson Walter Kitambawazi,Ntuli Kelvin Mwamukonda, Lucas Ferran Kweka, Hussein Hamza Hussein, Patrick Henry Mtui, Misana Masami Manyege, Godfrey Jordan Mahai, Lameck Liheta, Ibrahim Ramadhan, Ibrahim Mdalingwa, Aidan Alexander Kitaly, Gilbert William Shechambo, Samuel Safari Mbughi, Francis Mlelwa, Dastan Mbunda , Kelvin Peter Mruma, Innocen Ngonyani Kasuti, Jordan Seimu, Prosper Mkongwa, Hatibu Diwani, Daud Ndunguru, Sadam Mpacha, Mathias Raphael, Everest Madata, Israel Kihanga, Maige Joseph Maige, Stanslaus Frolence, Francis Ndiwayi, Kasian Kayombo.
 
Msabila Right Now Ni Lecturer Wa Mzumbe University Pia Mwenyekiti Wa Bodi Ya Mzumbe Sekondari.
 
Bubu Msemaovyo ...You have made my day! Leo ujasema ovyo! By the way, jina lako na unayoyasema hayaendani! Good memories are good things to cherish, najua HuXiang yapo yaliyokupata hata hataki kusikia majina kama bonge la mwanasoka wa enzi hizo na mwanasheria mzuri wa leo 'James Mbwana' au mzamiaji wa kilakala (mtoto wa mama, na rafiki yangu) na mkuu wa mkoa wa leo Mr John Mongela just to name a few! Wengine tunakumbuka mengi na sio kwa sifa wala sio kwa yaliyokupata HuXiang!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…