Mji wafurahia mtoto wa kwanza baada ya miaka 28

PAGAN

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
11,780
19,323
Mji mmoja kaskazini mwa Italia unasherehekea kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza tangu mapema miaka ya 1980.

Meya wa mji wa Ostana, ulioko eneo lenye vilima la Piedmont, anasema kuzaliwa kwa mtoto huyo ni “kutimia kwa ndoto” ya jamii ndogo inayoishi katika mji huo.

Idadi ya watu katika mji huo imeshuka sana katika kipindi cha miaka 100 iliyopita, na walikuwa wamesalia watu 84 pekee na ni nusu yao pekee huishi katika mji huo bila kuhamahama, Gazeti la La Tampa linasema.

Mtoto Pablo, aliyezaliwa katika hospitali moja mjini Turin amefikisha idadi ya watu mjini humo hadi 85 sasa.

Meya Giacomo Lombardo anasema mji wa Ostana ulikuwa na watu 1,000 mapema miaka ya 1900 lakini wakaanza kupungua baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

"Watu walipungua zaidi kuanzia 1975, ambapo ni watoto 17 pekee waliozaliwa kati ya 1976 na 1987, ambapo mtoto wa mwisho – mvulana- alizaliwa,” anasema.

Tangu wakati huo, hakuna mtoto mwingine aliyezaliwa hadi sasa mji huo ulipompokea Pablo.

Mji huo unajaribu kukabiliana na hali ya kushuka kwa idadi ya watu kwa kuunda nafasi za kazi.

Wazazi wa Pablo, Silvia na Jose, walikuwa wamepanga kuhamia ng’ambo miaka mitano iliyopita lakini ripoti zinasema waliamua kukaa baada ya kupewa kazi.

Sherehe kubwa imeandaliwa mjini Ostana, kusherehekea kuzaliwa kwa Pablo, na kwa mujibu wa La Stampa, sanamu ya korongo imewekwa kwenye lango la kuingia mji kwa heshima yake. [BBC]

160129052505_ostina_italy_512x288_wikimediafrancocranco56.jpg
 
Mwenye utaalamu atuambie kwanini hawazaani ?

Duc in Altum
 
Watu walikua wanahama mji kutokana Na ugumu WA Maisha eneo Hilo, coz mpaka mtoto huyu anazaliwa hawakuzidi 90, tena Serikali ya mji ilibuni kazi ambazo zikafanya hata wengine wabaki, otherwise mji ungebaki Mahame, familia ya mtoto yenyewe ilitaka kuhama 5 years a go, baada ya kupewa ajira Na serikali ya mji ndo ikaamua kubaki!
 
wampeleke babu slaa na babu mwenzie mwanakijiji wakaende na wake zao wakaje mji maana mapenzi wameazia uzeeni ni kuzaa kila siku baada ya mika mitano mji utakuwa full
 
Ingekuwa ni bongo wangesema huo mji wachawi wamezidi
Na inawezekana miaka 30 mbeleni huo mji watabaki wa 4 tu.
 
Hao wazazi wataweza tunza mtoto kweli?!!

Maana mahitaji ya mtoto itakuwa issue,
 
Mwenye utaalamu atuambie kwanini hawazaani ?

Duc in Altum
ni kutokana na umri wa wakaazi wa eneo hilo, inawezekana wakaazi waliibakia baada ya wengi wao kuhama ama kwenda kupigana vita,
walikua na umri mkubwa na pia inawezekana idadi ya wanaume ilikua chache.
pia katika eneo hilo kumekosekana uhamiaji na badala yake kutakua na wahamaji.
 
Mi nafikiri kuna tatizo kwenye enviroment wanazoishi mfano: Maji wanayo tumia kupikia na kunywa, miamba inayo zunguka eneo hilo inaweza kuwa inatoa hewa yenye asili ya madini hatarishi, udongo unao zunguka maeneo wanayo lima nafaka,matunda,viazi nk udongo unaweza kuwa na madini yenye matatizo.

Haiwezekani wakazi wote wakawa na matatizo ya infertility wakati sio ndugu/inbreeding.
 
natafakari walivyokuwa wanatumana wenyewe kwa wenyewe ...........natafakari pia oidadi ya wanawake na wanaume ili nijiridhishe
 
Miji Kama hii ipo kwenye maeneo ya Ulaya ya kusini, nchi za mediteranian. Sababu kubwa Ni uchumi. Wahamiaji hawawezi kuhamia hapo na vijana wazawa wenye nguvu wote wanahama kwenda kwenye neema. Hapo rhumba kali.
 
Mi nafikiri kuna tatizo kwenye enviroment wanazoishi mfano: Maji wanayo tumia kupikia na kunywa, miamba inayo zunguka eneo hilo inaweza kuwa inatoa hewa yenye asili ya madini hatarishi, udongo unao zunguka maeneo wanayo lima nafaka,matunda,viazi nk udongo unaweza kuwa na madini yenye matatizo.

Haiwezekani wakazi wote wakawa na matatizo ya infertility wakati sio ndugu/inbreeding.
Mkubwa hii ni assumption,lakini naweza iamini hii kuliko hata habari yenyewe! It sound 0.5%
 
Back
Top Bottom