Mji wa Iringa katika mwonekano mzuri

Wadanganye watoto bro!!! usifikiri watu ku google hawajui,haya ndo matatizo ya div 5,hata geography imekupiga chenga


Nadhani hili ni tatizo lako, ungeendelea kusoma mabandiko yangu katika mada hii usingehitimisha kwa kunitunishia misuli eti division 5, hii division 5 ndo imekuzindua usingizini wewe mwenye division one imeshindwa kuniamsha niliyelala. Hahaha! JF hadi raha!
 
Miaka zaidi ya kumi sijapita huko. Nice place, weather, food.

Mwezi uliopita nimebahatika kupita huko, Kitonga wamejitahidi kuijenga vizuri, gari itashindwa kupanda mlima kwa ubovu wa gari yenyewe lakini barabara ni bomba sana. Kwa siku zijazo wangeipanua kuwa pana zaidi kuwa na njia mbili kila upande maana magari makubwa yakishatangulia kwa mwendo pole hakuna pa kulipita wakati upende mwingie nako magari ya mwendo pole bila kikomo.
 

Mgololo nakupenda kwa moyo wote
 
Kuna milima inaitwa nyang'olo ndo balaa,kwa nchi hii hakuna njia ina milima kama ile na si kitonga mkuu,hii njia ipo karibia na mtera njia ya Dodoma Iringa...aliyewahi kupita njia hiyo atakubaliana nami..
 

Hii Sio Iringa ni La Paz, Bolivia
 
Aaah Iringaaaaa!! Baridiiiii! Karibia kila mtu anamjua mtu. Hehehe. Hakuna siri hapo kama bweni tu. Wazungu kila wakija wanagoma kuondoka. Ila pana wenyewe sio kuingia kichwa kichwa.
 
Eh jamani watu wameshupalia na Bolivia hio! BAAAASSSIIIIII tumejua na aliyetuma kakiri. Ebo! Mnataka nini tena waswahili?
 
Shika adabu yoko we mtoto! kamuulize mama yako mzazi kama mimi sio baba yako wa kufikia!

Hili kosa la kumhusisha mama yangu ktk maongezi yetu ndo lilikupa ban siku ile bado hujakoma?
 

Mkuu kuna milima haijulikani nayo ni mikali kuliko Kitonga. Ukiwa unatoka Makao mkuu ya wilaya ya Mpwapwa unaingia vijijini huko karibu na mpaka na Wilaya ya Kilosa, huko wanaishi wahehe sana napo kuna mlima mkali. Ukienda Madibila ukitokea Mafinga, ukisahapita vijiji vya Sadani na Igomaa napo kuna mlima mkali. Huu mlima wa Kitonnga ni wa kawaida, wala hautishi labda kwa wale ..... Sekenke napo pako kawaida sana
 

Yanapishana kupita kawaida
 
Hata kitonga hakuna lami ni nondo zimetandazwa chini na zege likamwagwa anzia mwanzo wa mlima hadi mwisho nilishuhudia mwenyewe nadhani ujenzi ulianza 2004 kama sikosei.
Hili ndilo nililokuwa naliwaza siku nyingi juu ya pale kitonga ahsante kwa kuliweka bayana,ingawa kwa mwaka huo sina uhakika may be 1994
 
Hili ndilo nililokuwa naliwaza siku nyingi juu ya pale kitonga ahsante kwa kuliweka bayana,ingawa kwa mwaka huo sina uhakika may be 1994

Kwa nini kutumia mate hali wino upo? Nimepita mara nyingi hapo Kitonga na mara ya mwishonimepita mwezi uliopita September mwaka huu, licha ya ushuhuda huo kuna picha katika bandilo langu hapo juu kuonyesha madhari ya milima ya Kitonga na barabara ya lami. Jaribuni kupitia mabandiko mbalimbali katika mada ili kupata taswira isiyowaacha na maswali yasiyojibika.
 
Hujasoma na kuelwa nilichoandika, namaanisha barabara ya Kitonga ni ya lami lakini hii ya latin ameriaka si ya lami.

Acha ubishi wewe bara bara ya mlima kitonga sio lami ni zege tupu mwanzo hadi mwisho wa mlima na kuna car parking za kutosha tu kushoto na kulia.
 
Hili ndilo nililokuwa naliwaza siku nyingi juu ya pale kitonga ahsante kwa kuliweka bayana,ingawa kwa mwaka huo sina uhakika may be 1994

Hapana namaanisha mwaka waliofanya maboresho yani walipoitoa ile lami wakapanua bara bara na kuweka zege na kingo baadhi ya kona yani sasa hivi haunyati na una overtake vizuri tu iwe kupanda au kushuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…