Mpandafarasi
Member
- Dec 7, 2008
- 57
- 11
Mjeshi aliyemchapa Trafiki,anyea debe!
Jeshi letu la Wannanchi (JWTZ), limenasa na kumtupa lupango Koplo Steven Sagana, kwa kuhusika na kosa la kuongoza kichapo kwa askari wa Usalama Barabarani, Sajini Thomas, juzi Dsm.
Koplo Sagana na wenzake walitenda shambulio hilo la kikatili kwenye mataa ya Ubungo...ambapo ni makutano ya barabara za Morogoro, Mandela....kwa madai ya kucheleweshwa na Trafiki huyo aliyekuwa akiongoza magari katika eneo.
Taarifa ilidodonshwa kwa vyombo vya mijinews na Kurugenzi ya Habari ya jesho hilo,ilisema kuwa jeshi hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini limeunda timu ya pamoja kuchunguza na kubaini undani wa mazingira ya tukio hilo ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wote waliohusika.
Hatua za awali za kinidhamu zilizochukuliwa na JWTZ kufuatia tukio hilo baya ni pamoja na kumkamata na kumburuza ndani Koplo Steven Sagana wakati wakibainishwa wenzake waliohusika na tukio hilo, ilisema taarifa ya JWTZ ambayo ilieleza kusikitishwa na kitendo hicho cha utovu wa nidhamu kilichofanywa na askari wake.
Tunapenda kuwahakikishia wananchi kuwa JWTZ itaendelea kuchukua hatua mbalimbali kudhibiti nidhamu ya wanajeshi wote, kuimarisha ushirikiano na vyombo vyote pamoja na wananchi kwa ujumla sambamba na kuwa tayari wakati wote kutekeleza jukumu la ulinzi wa taifa letu pamoja na majukumu mengine mbalimbali, iliongeza taarifa ya Jeshi hilo.
Source: Darhotwire.com
For a foolish person like him, thats the best place he
deserves...!
Hiyo mambo ya kuwa MBUZI WA SADAKA yatafuatia
baadaye kama thread ingine.
But at least by now any dog has been locked up! Kudos!
Wakuu mie sina comments nyingi sana lakini siku hiyo mimi pia nilikuwa ubungo nikitokea mwenge kwenda kimara jioni. Sina hakika wajeshi wetu walikuwa wanatoka wapi kwenda wapi lakini honestly traffic aliyekuwepo alituboa maana alikuwa anaruhusu magari upande mmoja tu wa morogoro kwenda city centre na mjini kwenda morogoro. Wengine tulibaki zaidi ya nusu saa bila kuruhusiwa. Pia traffic huyo alionekana kutumia simu ya mkononi kusoma messages mbele ya watu waliokata tamaa ya kusimama na kusubiri. Mimi simhukumu yeyote lakini naomba haki itendeke kwa kuangalia pia mazingira, yawezekana maafande walichukua hatua kuingilia kati uzembe kama huu.
Sasa ku-prove mashtaka yake yapi tena? Si amempiga Traffic Officer watu wakiwa wanamuona???
Sidhani kama unaelewa kitu kinaitwa natural justice mzee. Huruhusiwe kuweka mtu ndani bila kumsomea mashtaka. Sema bongo kwa sababu ya kuburuzwa ndo maana hamuwezi kuona hichi kitu. Mshatikiwa yeyeto (the accused) lazima apelekwe mahakamani kabla ya kuwekwa ndani. Polisi wanaruhusa ya kumshika kwa masaa tu. Kama hawatafungua mashtaka, basi ni sharti wamuachie huru!
Mtu ameonwa kabisa anamchapa askari alafu wamwachie aende zake! Du! We kweli Mtoto.