Mjeshi aliyemchapa Trafiki,aenda nyea debe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjeshi aliyemchapa Trafiki,aenda nyea debe!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mpandafarasi, May 21, 2009.

 1. Mpandafarasi

  Mpandafarasi Member

  #1
  May 21, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mjeshi aliyemchapa Trafiki,anyea debe!

  Jeshi letu la Wannanchi (JWTZ), limenasa na kumtupa lupango Koplo Steven Sagana, kwa kuhusika na kosa la kuongoza kichapo kwa askari wa Usalama Barabarani, Sajini Thomas, juzi Dsm.

  Koplo Sagana na wenzake walitenda shambulio hilo la kikatili kwenye mataa ya Ubungo...ambapo ni makutano ya barabara za Morogoro, Mandela....kwa madai ya kucheleweshwa na Trafiki huyo aliyekuwa akiongoza magari katika eneo.

  Taarifa ilidodonshwa kwa vyombo vya mijinews na Kurugenzi ya Habari ya jesho hilo,ilisema kuwa jeshi hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini limeunda timu ya pamoja kuchunguza na kubaini undani wa mazingira ya tukio hilo ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wote waliohusika.

  “Hatua za awali za kinidhamu zilizochukuliwa na JWTZ kufuatia tukio hilo baya ni pamoja na kumkamata na kumburuza ndani Koplo Steven Sagana wakati wakibainishwa wenzake waliohusika na tukio hilo,” ilisema taarifa ya JWTZ ambayo ilieleza kusikitishwa na kitendo hicho cha utovu wa nidhamu kilichofanywa na askari wake.

  “Tunapenda kuwahakikishia wananchi kuwa JWTZ itaendelea kuchukua hatua mbalimbali kudhibiti nidhamu ya wanajeshi wote, kuimarisha ushirikiano na vyombo vyote pamoja na wananchi kwa ujumla sambamba na kuwa tayari wakati wote kutekeleza jukumu la ulinzi wa taifa letu pamoja na majukumu mengine mbalimbali,” iliongeza taarifa ya Jeshi hilo.

  Source: Darhotwire.com
   
 2. mlokole

  mlokole Member

  #2
  May 22, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 14
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 3
  Kutupwa lupango kwa Koplo Steven Sagana kumeonyesha wazi kuwa yeye ni kondoo wa muhanga kwani katika kulipuka kwa mabobu Mbagla mmoja wa mkubwa wa jeshi alisikika akisema kuwa wanajeshi wetu wana nidhamu panapokuwa na mkubwa wake basi huwa mdogo anasikiliza amri, na kwa kuthibitisha hayo hata katika ushahidi wa kesi ya mauwaji inayomkabili zombe na wenziwe. sasa kama palikuwa na mkubwa wao mwenye cheo cha Luteni Canal na akaweza kuwaondoa hao wanajeshi basi wazi wazi inaonekana kuwa walikuwa wakitekeleza amri ya mkubwa wao ambaye ni LUTENI CANAL. Sasa yeye ndiye anapaswa kuwekwa lupango kwanza kabla ya hata huyo Kondoo!!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  For a foolish person like him, thats the best place he

  deserves...!

  Hiyo mambo ya kuwa MBUZI WA SADAKA yatafuatia

  baadaye kama thread ingine.

  But at least by now any dog has been locked up! Kudos!
   
 4. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hii inavunja sheria ya natural justice na habeas corpus. Huwezi kumtupa mtu ndani kabla ya ku-prove mashtaka yake!! mnakuwa kama Guantanamo Bay bwana!
   
 5. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Sasa ku-prove mashtaka yake yapi tena? Si amempiga Traffic Officer watu wakiwa wanamuona???
   
 6. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #6
  May 23, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  ..,..
  He is not a fool but fooled by his superior!
  According to military personnel,there is what they call SUPPORT your superior even though you disagree.These means you have to act immediately to the boss' order or even on his mood.
  That Lt col must get his due share of what his subordinate did
   
 7. u

  urithiwetu Senior Member

  #7
  May 23, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kinachofanyika ni usanii tu wa danganya toto, huyo Luteni Kanali ndiye alikuwa mkuu wa msafara, na alipaswa kukamatwa pamoja na wengine wengi. Walioshuhudia waliona wanajeshi wengi wakimchangia huyo Polisi, sasa kwanini akamatwe huyo Koplo mmoja tu?

  Wakamatwe wote na washtakiwe Mahakama ya kiraia kwani walifanya kosa nje ya eneo la Jeshi.

  Huyo Koplo anatolewa kama kafara tu. Hakuna lolote la maana lililofanyika so far.
   
 8. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Wakuu mie sina comments nyingi sana lakini siku hiyo mimi pia nilikuwa ubungo nikitokea mwenge kwenda kimara jioni. Sina hakika wajeshi wetu walikuwa wanatoka wapi kwenda wapi lakini honestly traffic aliyekuwepo alituboa maana alikuwa anaruhusu magari upande mmoja tu wa morogoro kwenda city centre na mjini kwenda morogoro. Wengine tulibaki zaidi ya nusu saa bila kuruhusiwa. Pia traffic huyo alionekana kutumia simu ya mkononi kusoma messages mbele ya watu waliokata tamaa ya kusimama na kusubiri. Mimi simhukumu yeyote lakini naomba haki itendeke kwa kuangalia pia mazingira, yawezekana maafande walichukua hatua kuingilia kati uzembe kama huu.
   
 9. Robweme

  Robweme Senior Member

  #9
  May 24, 2009
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 178
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Si yule traffic mwembamba mrefu eti, yule anayependelea foreni ya kutoka kimara na kituo cha daladala ubungo au sio yeye.Kama ni yeye basi walimpiga kidogo wangetoa meno maana jamaa uwa anapendelea magari yanayotoka kimara/morogoro zaidi ya njia zote.Lakini nasikia madreva wa daladala huwa wanampatia kidogo halafu anaachia njia.Mtoeni meno wakati mwingine
   
 10. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Huenda traffic alikuwa na shida lakini hekima na busara si kumshambulia kwa mateke na magumi hadharani! Zipo taratibu za kulalamikia swala kama hilo si ubabe walio utumia. Let them face it, kwanza wamezidi ubabe wao hata hupiga raia wasio na hatia mitaani!
   
 11. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #11
  May 26, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama unaelewa kitu kinaitwa natural justice mzee. Huruhusiwe kuweka mtu ndani bila kumsomea mashtaka. Sema bongo kwa sababu ya kuburuzwa ndo maana hamuwezi kuona hichi kitu. Mshatikiwa yeyeto (the accused) lazima apelekwe mahakamani kabla ya kuwekwa ndani. Polisi wanaruhusa ya kumshika kwa masaa tu. Kama hawatafungua mashtaka, basi ni sharti wamuachie huru!
   
 12. Kyakya

  Kyakya JF-Expert Member

  #12
  May 26, 2009
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 397
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Mtu ameonwa kabisa anamchapa askari alafu wamwachie aende zake! Du! We kweli Mtoto.
   
 13. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #13
  May 26, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wabongo kwa kuunda kamati ndio wenyewe ndugu zangu. Ameshakamatwa na mashtaka yake yanafahamika kwanini tena tume au ndio kujitafunia tu
   
 14. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  We nawe ni nanga? Wewe umeshasikia kitu kinaitwa imprisonment without trial? hichi ndo chenyewe, ndo maana nikasema ni sawa na guantanomo bay. Hata kama watu millioni moja walimwona akitenda kosa, ni lazima mtu asomewe mashtaka kabla ya kutupwa jela! UNAELEWA HILO? Ndo maana kuna writ inaitwa habeas corpus. Katafute jinsi inavyotumika ndo utaelewa nina maana gani!
   
Loading...