Mjengwa uso kwa uso na simba wa mikumi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjengwa uso kwa uso na simba wa mikumi!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by jamadari, Feb 24, 2010.

 1. jamadari

  jamadari JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 295
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Jumapili ya Februari 20 sitaishi nikaisahau. Nilifika Mikumi National Park Jumamosi alasiri kwa mapumziko ya usiku mmoja kabla ya kuendelea na safari yangu ya Dar nikitokea Iringa. Usiku wa kuamkia Jumapili simba waliunguruma karibu kabisa na Mikumi Wildlife Camp nilikofikia banda namba 9 lijulikanalo kama Kongoni. Niliamka kunako saa kumi na mbili. Mmoja wa wafanyakazi wa kambi hiyo akaniambia simba watatu wako umbali wa mita mia tano kutoka kambini. Nikaenda haraka kuwaangalia; dume mmoja na majike mawili. Nikapiga picha kadhaa. Simba dume alionyesha kukasirika sana, aliniangalia kwa macho makali Kisha akanifokea, akijiandaa kurukia mlango wa gari. Nikafunga kioo na kuondoka haraka sehemu hiyo. Nikarudi kambini na kwenda moja kwa moja kupata kikombe changu cha chai. Nikiwa njiani kurudi kwenye banda langu, majira ya saa moja na nusu asubuhi, ghafla nikamwona simba yule dume akinijia akitokea banda namba kumi liitwalo Kanga. Nywele zilinisisimka,nilitamani ardhi ipasuke. Hakukuwa na mtu mwingine yeyote. Sikupiga kelele, maana ningemchanganya zaidi simba yule. Nikabaki nikimwangalia simba yule machoni huku nikirudi kinyumenyume kurudi ilipo ofisi ya mapokezi. Kamwe usimgeuzie simba kisogo. Ukimtazama machoni anaweza kugeuka na kutafuta njia nyingine, simba ni mnyama mwenye kuona haya. Na hakika, simba alitoka kwenye njia niliyokuwa nikiifuata na kuelekea kwenye banda lingine mkono wa kulia, aliachana na mimi. Haraka nikakimbia kuwajulisha baadhi ya wafanyakazi wachache waliokuwapo pale kambini. Kazi ikawa kuwataarifu kwa haraka wageni wote ( watalii) waliokuwapo kambini pale kuwa ' kambi imevamiwa na simba watatu'. Simba dume ameondoka banda namba 10 na kuwaacha majike wake wawili wakiwa mlangoni. Nikiwa na wafanyakazi watatu wa kambi hiyo, tukajipanga kwa haraka kuhakikisha wageni wote walio mabandani wanabaki ndani ya mabanda hayo kwa usalama wao, na walio nje kwenye restaurant watafute haraka sehemu za kujihifadhi. Maana simba walianza kupita banda moja baada ya jingine. Tukaanza kufuatilia nyendo za simba wale pale kambini ili kuhakikisha usalama wa wageni. Niliweza pia kupiga picha nyingi za karibu. Simba dume ndiye aliyeanza kuondoka eneo la kambi baada ya nusu saa na kuwaacha majike wawili. Hao majike tulifanikiwa kuwadhibiti kwa kutumia mlio wa gari na kuwasukuma umbali ambao uliruhusu wageni kutoka mabandani na walio nje kwenda kuchukua mizigo yao. Niliondoka Mikumi huku kukiwa na taarifa za kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa simba wale kurudi tena eneo la kambi hiyo. Kwa picha zaidi za tukio hilo, tembelea; http://mjengwa.blogspot.com/
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 43,134
  Likes Received: 27,105
  Trophy Points: 280
  MJ pole sana.
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  ..and so?
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,387
  Likes Received: 5,752
  Trophy Points: 280
  Great adventures.....kumbukumbu nzuri ya ujasiri na utalii....
   
 5. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Duh! Aisee pole sana
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Lazima nywele zikusisimke Mkuu na shukuru Mungu sana uliwahi kumuona kabla hajakuvamia. Ukiwa maeneo ya mbuga za wanyama inabidi uwe extra careful ama unaweza kujeruhiwa vibaya sana au hata kukutana na umauti.
   
 7. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pole kwa yaliyokukuta na hongera kwa ujasiri
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Feb 24, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160

  Nimeshika pumzi yangu, nahisi ningekuwa mimi ningepiga yowe kubwa, ama ningekufa kabla hajanifikia.
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 42,088
  Likes Received: 37,426
  Trophy Points: 280
  Aisifuye mvua imemnyea.
  Nimeipenda sana mbinu ya kuangaliana na simba.
  Bora wewe uliikumbuka hiyo, maana nadhani mimi wangekuta soli za safari boot yangu tu, maana niliisahau nikiwa mdogo.
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 42,088
  Likes Received: 37,426
  Trophy Points: 280
  so what?
   
 11. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Amaaaa, kumbe Mjengwa ndiye Jemadari? Nilimfahamu sana kwenye Tanzanet enzi hizo. Unaona hadithi za babu zinavyosaidia? Kumtazama simba usoni ana haya sana. ndiyo maana akimtafuna mtu anauacha uso na viganja vya mikono na mikguu. Tumbo na minofu huenda sambamba navyo.
   
 12. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  pole lakini ilikuwa very gud adventure
   
 13. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  it sounds like a movy...anyway pole sana Mjengwa.
   
 14. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  01.jpg

  03.jpg

  02.jpg

  11.jpg

  16.jpg
   
 15. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #15
  Feb 24, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  3.jpg

  04.jpg

  13.jpg

  22.jpg
   
 16. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  inaogopesha lakini nice adventure
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...